CHADEMA wanaweza kuwa wanafanya makosa makubwa kama watakuwa wanachukulia kuhama kwa wabunge watakuchukulia kama kupoteza wananchama wao jimboni.
In fact, mara wahamapo wabunge hawa juhudi jimboni zinatakiwa ziongezwe mara dufu hata kama hawatashiriki kwenye chaguzi ndogo zitakazofuata.
Kuimarisha chama ndani ya majimbo hayo yaliyoachwa ni muhimu sana. Hawa wabunge walipata ubunge kwa vile wananchi wa maeneo hayo waliikubali CHADEMA. Kuondoka kwa wabunge hao haimaanishi kutokubaliwa kwa CHADEMA.
..Je, viongozi wanafanya jitihada zozote za kukabiliana na wimbi la wabunge kuhama?
..Kwa mfano Mh.Gekul amewatuhumu viongozi kutokuwa na msaada kujenga chama majimboni.
..Ni kweli wabunge wanashawishiwa. Lakini tutakuwa tunajidanganya tukiamini kwamba hakuna matatizo ndani ya CDM.
..Kwa maoni yangu CDM wanapaswa kufanya uchunguzi huru kubaini matatizo ya ndani ya chama.