Pauline Gekul, Mbunge wa Babati Mjini(CHADEMA) ajiuzulu na kujivua uanachama, ajiunga na CCM

Pauline Gekul, Mbunge wa Babati Mjini(CHADEMA) ajiuzulu na kujivua uanachama, ajiunga na CCM

69FECD9B-4C70-4B6C-81F5-52B4E620BFB1.gif
 
Aiseee!!!!!Mal....ya tangu lini akaridhika?

Nyie wanunueni tu ila hakuna chama cha siasa kilichowahi kukubalika kwa wananchi kisa kimenunua wanasiasa wa chama fulani.

Bora hata hizo hela mngetoa milioni 50 kwa kila kijijini angalau tungewaona mna akili.

Endeleeni kujaza maji kwenye gunia akili zikiwakaa sawa mtaacha huo ujinga.
2015 mliwanunua wanaccm kwa sh ngapi?
 
Ruzuku ziliwe na Mbowe halafu uchaguzi uchangiwe na wabunge ...huo ndio upuuzi
Bahati mbaya au nzuri ccm imeshindwa kutatua kero za nchi hii,no wonder hata watumishi wa uma wanastaafu bila kupewa mafao,barabara ya Ifakara ina muda sasa toka jiwe aweke jiwe la msingi,haitushangazi kuwa ccm inaingia katika maajabu kama ilivyo ajabu ya zimbabwe kushuka thamani ya kila kitu richa ya Mugabe kutolewa.
 
Siungi mkono hizi harakati za kujivua ubunge ila CHADEMA nnarudia tena jitafakarini, lipo jambo haliko sawasawa kubalini kunifanyia tathmini hali ni mbaya na itakula kwenu ....Endeleeni kubeza
 
Hiyo story ya kununua na kununuliwa ilishakosa kiki na wananchi wameshaishtukia tafuteni kisingizio kingine.
Kungekuwa na kura za maoni ccm ndio mtu apitishwe kugombea wangapi wangeunga mkono juhudi.

Ndio maana ya neno kununuliwa linatumika hapo. In exchange ya kuunga mkono juhudi utapita kugombea bila kupingwa ukizingatia pia utatangazwa mshindi kwa lazima. Hiyo ni biashara kamili.
 
Kuanzia leo tusiwaamini hawa wabunge wa chadema. Anayesema leo hawezi kuondoka chadema unashangaa weekend ijayo anaondoka. Hii haina haja ya kufanya vikao vya ndani ndani ya chadema, kwa sababu unakaa na mtu wakati mwenzako anapanga. Kuondoka
Binafsi natamani wanaotaka kuondoka waondoke wote hata leo wabaki walio serious na upinzani.
 
Back
Top Bottom