Zanzibar 2020 Pemba: Vyama sita vya siasa vyalaani vurugu za Alfajiri ya leo, waomba msaada wa IGP baada ya wananchi kukatwa mapanga

Zanzibar 2020 Pemba: Vyama sita vya siasa vyalaani vurugu za Alfajiri ya leo, waomba msaada wa IGP baada ya wananchi kukatwa mapanga

Kwanza huyu mgombea anamuhusu vipi na tukio hili?
Wewe kama Nani mpaka utoe maelezo ya kumwita IGP? Hivi vyama mamluki ni Bora mpigwe mapanga tu
 
..wakati wananchi wanadhulumiwa na kunyimwa haki zao hawazungumzi.

..wanakuja kuzungumza baada ya wananchi kuamua kuchukua sheria mikononi mwao.
 
Tukio hili ni la kupingwa vikali, Ni tukio baya na la kiuaji.
Vyombo vya Ulinzi na Usalama viwatafute wahusika na wapate hukumu kulingana na Sheria za nchi.
Watanzania tuzidi kudumisha Amani Upendo na siasa safi kipindi hiki cha Kampeni.
 
Wazanzibar mnatabia mbovu sana, sasa uko mwatako mwataka nini kama si tako??
Ninesoma vyooote ila nimekuwa attracted na jina la mtaa tu!! "Mwatako".

Jamaa wamevamia "Mwatako" eeeh! Wanatabia mbaya sana
 
Zanzibar mmeanza tena, serikali jaribuni kutenda haki, raia pia tutenda haki, haki ikitawala haya maovu yatapungua, lakinj haki ikiminywa amani itafifia, si jambo la kawaida mtu kuingia kwenye myumba ya Mungu na kufanya uovu wa kiasi hicho, ameshindwa kumuogopa Mungu. Serikali pia jitahidi kusaidia damu za raia zisimwagike hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu.
 
Ni muda sasa wa vyombo vya dola vi act aggressive na hao Wazenj mana kuwachekea ni kuzidi kuwapa kiburi
 
Vyombo vya ulinzi viwasake magaidi hayo
Wameshindwa kuwasaka waliompiga risasi tundu na wengine wataweza hao.

Kiufupi ccm haya mambo mnayataka yawepo nayatakuwepo. Subirini pemba ni sehem nyengine
 
Mgombea Urais Zanzibar, Ameir Hassan Ameir(Demokrasia, makini): Katika barua yetu ya tarehe 15 kumuomba msajili wa vyama vya siasa pamoja na IGP, tulimuelezea kwamba, kuna baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa hapa nchini kwetu Zanzibar, wameanza tabia ya kuanza kuwashajihisha wanachama wao au wananchi kuingia katika vurugu.

Kwa bahati mbaya, Alfajiri ya leo kuna taarifa kwamba kisiwani Pemba, Kangagani, katika mtaa wa Mwatako kuna baadhi ya wamevamiwa wakati wanataka kuingia Msikitini na wakapigwa mapanga. Ninalaani vikali kitendo hiki.

Mheshimiwa IGP damu imeshaanza kumwagika katika kisiwa cha Pemba. Kupitia press hii tunakuomba mheshimiwa IGP utoe watu wako waende kisiwa cha Pemba na kuwasaka wale wote wanaohusika na kitendo hiki kwani sisi viongozi wa vyama vya siasa maelngo yetu tuendeleze kufanya campaign kwa salama na amani, mimi naamini kuna maisha baada ya siasa.

Kama hatua hazijachukuliwa, basi tungemuomba Rais Magufuli, Rais Shein waahirishe uchaguzi kwa sababu hatuwezi kuingia katika uchaguzi ambapo kuna baadhi ya watu hawana hatia tayari washahatarishwa maisha yao.

====

PEMBA: BAADA YA KUSHAMBULIWA KWA WATU MSIKITI ALFAJIRI YA LEO

Kamishina Msaidizi wa Polisi Mkoani Pemba, Juma Sadi Hamis amethibitisha kutokea kwa tukio hilo alfajiri ya leo

Amesema mhalifu aliingia msikitini wakati wa Ibada na kuwashambulia kwa panga watu watatu kisha akatokomea kusikojulikana. Waliojeruhiwa ni Khakis Makame(62), Bakar Hassan(55) na Kombo Hamad Yusuf(73).

Majeruhi wawili wa tukio hilo wamelazwa Hospitali ya Kangagani na Mmoja hali yake si nzuri hivyo amesafirishwa kwa ndege kupelekwa Hospitali ya Mnazi Mmoja Unguja

Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta mhusika wa tukio hilo.

Wanafiki waliowekwa kwa ajili ya kuibeba ccm,wanaanza kuonesha unafiki wao
 
Ni kwa nini yanatokea mapema hivyo? Kama sababu ni kukatwa wagombea lawama kwa tume ya uchaguzi, mtaenguaje wangombea wa upinzani tu? Hamuoni aibu!
 
Watu wasio julikana wameingia Pemba sasa,si wangewapiga watu wa tume za uchaguzi ambao ndio wanastahiki kushikishwa adabu kwa kuvuruga mchana kweupe.
Watu wa tume waliofanya zulma itabidi walindwe sana sana kuliko anavyolindwa magufuli,watu wana asira na wapo tayari kwa lolote.
Watu wasio julikana wamekosea sana hapo au jamaa wanagombea kamati za msikiti
 
Back
Top Bottom