Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jeshi la Polisi liwasake mpaka liwapate; wasipopatikana, kesho na kesho kutwa watafanya uharifu mkubwa zaidiHayo ndiyo IGP Sirro anayayataka.
Vyombo vya ulinzi viwasake magaidi hayoHao ni "uhamsho masalia" kamata weka ndani watoka Hussein Mwinyi anamaliza awamu ya pili 2030! Twataka amani sie!
Ninesoma vyooote ila nimekuwa attracted na jina la mtaa tu!! "Mwatako".
Jamaa wamevamia "Mwatako" eeeh! Wanatabia mbaya sana
Vyombo vya ulinzi viwasake magaidi hayo
Nilifikiri wamekukata mapanga wewe kibibi si una miaka 73 au?Mungu ibariki Pemba
CCM haitakiwi Pemba
MwatakoCCM haitakiwi Pemba
Wameshindwa kuwasaka waliompiga risasi tundu na wengine wataweza hao.Vyombo vya ulinzi viwasake magaidi hayo
Wanafiki waliowekwa kwa ajili ya kuibeba ccm,wanaanza kuonesha unafiki waoMgombea Urais Zanzibar, Ameir Hassan Ameir(Demokrasia, makini): Katika barua yetu ya tarehe 15 kumuomba msajili wa vyama vya siasa pamoja na IGP, tulimuelezea kwamba, kuna baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa hapa nchini kwetu Zanzibar, wameanza tabia ya kuanza kuwashajihisha wanachama wao au wananchi kuingia katika vurugu.
Kwa bahati mbaya, Alfajiri ya leo kuna taarifa kwamba kisiwani Pemba, Kangagani, katika mtaa wa Mwatako kuna baadhi ya wamevamiwa wakati wanataka kuingia Msikitini na wakapigwa mapanga. Ninalaani vikali kitendo hiki.
Mheshimiwa IGP damu imeshaanza kumwagika katika kisiwa cha Pemba. Kupitia press hii tunakuomba mheshimiwa IGP utoe watu wako waende kisiwa cha Pemba na kuwasaka wale wote wanaohusika na kitendo hiki kwani sisi viongozi wa vyama vya siasa maelngo yetu tuendeleze kufanya campaign kwa salama na amani, mimi naamini kuna maisha baada ya siasa.
Kama hatua hazijachukuliwa, basi tungemuomba Rais Magufuli, Rais Shein waahirishe uchaguzi kwa sababu hatuwezi kuingia katika uchaguzi ambapo kuna baadhi ya watu hawana hatia tayari washahatarishwa maisha yao.
====
PEMBA: BAADA YA KUSHAMBULIWA KWA WATU MSIKITI ALFAJIRI YA LEO
Kamishina Msaidizi wa Polisi Mkoani Pemba, Juma Sadi Hamis amethibitisha kutokea kwa tukio hilo alfajiri ya leo
Amesema mhalifu aliingia msikitini wakati wa Ibada na kuwashambulia kwa panga watu watatu kisha akatokomea kusikojulikana. Waliojeruhiwa ni Khakis Makame(62), Bakar Hassan(55) na Kombo Hamad Yusuf(73).
Majeruhi wawili wa tukio hilo wamelazwa Hospitali ya Kangagani na Mmoja hali yake si nzuri hivyo amesafirishwa kwa ndege kupelekwa Hospitali ya Mnazi Mmoja Unguja
Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta mhusika wa tukio hilo.
Unaleta maneno watu hawana amani, na huwa wanasema amani ni tunda la haki!Hao washenzi wavunja amani watafutwe mpaka wapatikane, wasilijaribu dola