Pendekeza tozo nyingine Serikali ya Samia iichukue

Sasa amuweke nani??? Huo ni mfano wa ndoo iliyooza na kutu, hata ukiichomelea inatoboka kwengine. Viongozi wetu asilimia kubwa hafai kabisa na wala hawafai kuwa viongozi. Hawana vigezo, upeo, elimu wala hekima ya kuongoza. Lakini kwa kuwa ni wanachama wa Chama husika inabidi wapeane madaraka tu, sasa hakuna jinsi. Tutakwenda hivyo hivyo mpaka Mungu mwenyewe atakapotupa akili na maarifa ya kutambua kuwa ndoo ikishaoza inatakiwa itupiliwe mbali na tununue ndoo mpya.
 
Tozo ya mshikamano ya safari za Mama ughaibuni!
 
Kitendo Cha mwaka huu, kuletwa kwa Ct scanner machine kwenye hosp. Yetu ya mkoa na nkikumbuka ilikuwa mpaka uende mhmbili, kwakweli nitalipa Kodi na tozo zote kwa maendeleo zaidi ya Taifa langu.
 
Asubiri majibu 2025 !!harafu unapotaja nchi jirani kama kimbilio yawanaokuhoji maana yake unatangaza vita kwamba wawe wakimbizi katika nchi hiyo .kauli hii siyo sahihi kwa kiongozi .waelekeze kwa amani watu wataelewa.Viongozi wa serikali wanataikiwa kujua daima kuwa mwananchi ndiye boss wake.Hata hiyo kuongea ni kwa sababu umepata mshahara kutoka kwa huyo unayesema ahamie burundi.Nimwombe MH waziri aachane na kauli hii.Haijengi au kutetea hoja hata kidogo !!
 
Mwigulu is rubbish.
 
Hatuna cha kuwafanya hata hiyo 2025
 
... waweke tozo nyumba za kulala wageni sana sana mtu akija na pisi.
 
Sisi wananchi tunataka tozo iendeleee kutozwa na pia tunaishauri Serikali kupitia wizara ya Fedha iendelee kufanya utafiti maeneo mengine ambayo tunaweza kutozwa tozo kwani tunaona maendeleo yanayo patikana kutokana na tozo.
 
hakuna cha bure katika ulkmwengu huu, lazima tulipe tozo kwa maendeleo yetu.
unadhani maendeleo yataletwa bila tozo?! thubutu!!! hata hao wanao pinga tozo wanalifahamu hilo, ila nia yao ni kuona Serikali inashindwa kuleta maendeleo ya wananchi.
Hakuna nchi duniani iliyoendelea kwa kuwakamua tozo wananchi wake
Ni nchi corrupt ndio zinazoongoza kwa kuwakamua wananchi wao kwa tozo kwasababu matajiri Hawalipi kodi kwani wanakula na viongozi.
Mwigulu hafai kuwa waziri wa fedha anamuharibia Rais kwani he has presidential ambitions!
 
Mi naona watu wanaqngalia sana mechi kwenye Tv
Iwekwe Tozo maana wanakwepa kwa kutolipa viingilio
2. Boda boda hawatoi risti weka Tozo angalau kwa wiki walipe buku 2
3. Hawa wanaojiposti tik tok wekea Tozo au basi iweke kwenye simu zote smart

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
  • Akina Kinjekitile n.k wangefufuka leo na kuona maisha tunayoishi ili hali walituachia rasilimali kibao, wangeanzisha vita dhidi ya utawala.
  • Tunanakili mifumo ya mataifa yasiyo na rasimali kama Uingereza, Hispania, n.k
 
hakuna cha bure katika ulkmwengu huu, lazima tulipe tozo kwa maendeleo yetu.
unadhani maendeleo yataletwa bila tozo?! thubutu!!! hata hao wanao pinga tozo wanalifahamu hilo, ila nia yao ni kuona Serikali inashindwa kuleta maendeleo ya wananchi.
Kuna utofauti kati ya Tozo na Kodi
 
J
Kwani tozo Ina shida gani? Tatizo watanzania mnataka maendeleo lakini yanayokuja tu bila kuvuja jasho...kitu ambacho hakiwezekani

Mimi nasema tozo ziendelee kwa sababu angalau basi ndio mahali ambapo karibu Kila mtanzania utampata kwenye kuchangia maendeleo ya nchi yake
 
Huko nyuma hakukuwa na tozo zenye kulalamikiwa ila bado mashule,zahanati n.k vilijengwa na bado pesa zengine mafisadi walizipiga. Sasa ajabu unapotaka tuone kama vile Tanzania kulikuwa hakuna fedha za kuleta maendeleo na hizi tozo ndio suluhusho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…