Pendekezo: Majina ya viongozi yaondolewe miradi ya umma

Nadhani hii ulinilenga mimi ila umem quote mtu mwingine , Viongozi wakatili wa Tanzania hawana haja ya kuenziwa , hata kwenye vitabu vya Mungu tumekatazwa kumuenzi Shetani , viongozi wa Mataifa mengine wakienziwa kwao haimaanishi na sisi tuenzi wa kwetu ambao ni wezi .

 
Usimwamini mtu anayetumia kilevi hata kama ni babako,

Maana anaweza kuongea Yeye na POMBE ikaongea kumjibu au wote wawili, POMBE na MTU vikaongea Kwa pamoja ukashindwa kuelewa.
Humu JF naandika ya kwangu , siandiki ya mtu mwingine
 
Humu JF naandika ya kwangu , siandiki ya mtu mwingine
Namaanisha utofautishie wasomaji thread unazoandika Ukiwa umeelewa na thread unazoandika bila kilevi,

Maana we na Mzee mgaya, taabu sana sometimes.
 
Namaanisha utofautishie wasomaji thread unazoandika Ukiwa umeelewa na thread unazoandika bila kilevi,

Maana we na Mzee mgaya, taabu sana sometimes.
Siandiki jf nikiwa njwii , kwahiyo kila unachokisoma kutoka kwangu namaanisha .
 
Hiyo habari imeandikwa wapi ? kumbuka kwamba GEITA INAONGOZA KWA UKATILI DUNIANI , ikifuatiwa na Mogadishu , ya 3 ni Urus
Ebu saidia jamii ya kata ya Ikunguigazi, wilaya ya Mbogwe, Mkoa wa Geita kupaza sauti kamanda, ofisi za kusimamia haki na maendeleo ndio imetumika kunajisi haki

Mwalimu mkuu wa Buzigozigo S/M amempiga mimba mwanafunzi aliyekuwa kidato cha pili mwaka jana na kushindwa kufanya mtihani wake wa FTNA.

Cha ajabu diwani wa Magufuli ambaye pia ndiye m/kiti wa kamati ya Elimu katika baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Mbogwe, ameshirikiana na Mkuu wa shule ya sekondari Ikunguigazi na mtendaji wa kata hiyo kukwamisha sheria isichukue mkondo wake.

Wanamlinda mtuhumiwa kwa sababu ni mtumishi mwenzao hii haikubaliki eb tushirikiane taarifa imfikie waziri husika
 
Support! Ingawa dunia karibu yote inafanya hivyo, you are correct, majina ya watu yaondolewe. Tena jina la muuaji!
Lakini Kuna kitu huko USA kinaitwa JF Kennedy Airport. Nao wajitafakari
 
Stand ya mwendazake litumike jina la Mbezi Stand
kijazi ubungo liwe; Ubungo Interchange
Pale mfugale tazara liwe ; Tazara Interchange
pale soko la ndugai Dodoma iwe; Soko kuu la dodoma
Tuachane na majina ya watu kwani mengine ni ya kiwendawazimu!
 
Vitu vyepesi kama Hivi kujadili ni Matumizi mabaya Sana ya Akili, Iko wazi ktk worldwide politiks kuyapa majina ya viongozi miradi mbalimbali i.e Airport, Manowari za kivita, Kumbi za Umma, Kambi za Jeshi, Roads Na sio Big issue

unless Ubongo wako uwe na Changamoto ktk kufikiri.
 
Waliwahi kuteka yeyote au kuficha hela China ?
Soma vizuri hiyo orodha kisha kawaulize familia za watu wa Vietnam, wafungwa wa Guantanamo Bay, yatima wa Iraq na Afganstan, familia ya Patrice Lumumba, Che Guevara, familia ya Jamal Kashogi, watu .... n.k.
Orodha ni ndefu.
Tuhuma za kuficha pesa China na watu hawajachukuliwa hatua kisheria wakati mtu wa kuwalinda hayupo inabidi tumshangae anaye tuhumu wakati anayo nguvu ya kimamlaka na kikatiba kuhakikisha wahusika wanawajibishwa wengine wasirudie.
 
Nyerere na Karume majina yao yametosha kwenye maeneo yote.
Hao wengine hakuna haja ya kuenzi majina yao, ni ushamba na ulimbukeni ndio unawasumbua.
 
Mwa_ Philosopy mmoja alisema ukitaka watu waendelee kukumbuka hata baada ya kifo chako fanya jambo kubwa amabalo utakumbukwa siku nyingi baada ya kufariki :
Mfano Ma_Farao wa misri wanakumbukwa kwa kujenga mapiramid Miaka ya 4000_ 5000BC

Mwl. Nyerere tunamkumbuka kwa kupigania uhuru wa Tanzania na wa Nchi za kusini mwa Africa

Na Magufuli tunakumbuka kwa kudhubutu kubuni na kuanza ujenzi wa bwawa la Nyerere na Reli ya STG

Aandika vitabu kama Shakespear au Mwl. NYERERE hili wanazuoni wakukumbuke

au andika jina kwa kufanya miradi mikubwa ambayo tutakukumbuka nayo Baada ya kufariki na kuzikwa Makaburi ya VIP Kinondoni
 
Na wale walikuwa wamefurika uwanjani siku ya msiba wake ni mbu siyo watu?.Kwani wewe usipomkubali JPM basi ni lazima na watu wote wasimkubali!
Waliofurika pale si ni watu kama wewe, nimesema taja mtu mmoja mwenye akili na kujielewa aliyemkubali huyo shujaa wenu. Mimi kutomkubali Jiwe siyo lazima iwe sheria ya wote. Taj mmoja tu
 
Think well before sharing that nonsense ideas chief.. umeona tuu Magufuli bus stand? hujaona masoko, barabara and streets ambazo tunapitia umo kila siku? hii tunaita chuki binafsi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…