PostGE2025 Pendekezo Rahisi: Maneno 3 akiyasema Samia kesho yatazuia Maandamano yasiyo na Ukomo

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Mwanangu una akili na busara sana. Sijui kama. hao wanakuelewa. Ila pendekezo lako la tatu haliwezekani. Ni kama umjipiga mtama au kuharibu uhondo wote ulioanza nao. Ni uoni tu na ushauri.
 
Watu walivyo na uchu wa madaraka, hilo halitatokea!
Ujue behind the curtain ni JK na Mtandao, wakale wapi?
 
Mzee, hilo halitatokea.
Nywii nywii nywii ziende wapi?
Lakini either way, SHE IS FIXED!
Ije mvua lije jua!
Na waTanzania dont care what happens to her!
 
Mwanakijiji unazunguka sana. Wewe sema unataka mama ajiuzulu kitu ambacho hakiwezi kutokea hata ndotoni. Cha muhimu wale msiomkubali Mama Samia vumilieni hadi 2030. Lakini pia tunajipanga kumuongezea muda hadi 2035. Hayo mapendekezo yako yahifadhi uje umpe atakayekuwa Rais kupitia CHADEMA mwaka 2355.
 
Hayo yote uliyosema hawezi kuyafanya. Hata kusema pole jwa Waliopoteza Wapendwa wao halitayokea. Wala usitegemee kusia neno SAMAHAJI AU I AM SORRY.

MAZA ana kiburi sana.
Wabongo siku zote ni shida tu
Badala ya kulaumu chanzo cha balaa yote mnalaumu Rais na Askari na serikali yote.
Hao majambazi wasie anza kuchoma magari ya watu na kuvunja maduka na kuiba na kuchoma vituo vya polisi na kuchukua silaha zao na KUUA POLISI hivyo vifo vya wanyonge wasio na hatia vingetokea?
Lini hapa Tanzania Askari waliwahi kuingia tu kwenye nyumba ya mtu wakaanza kuua watu ovyo?

Acheni kupendelea ushetani. Mimi pia nimepoteza ndugu waliokuwa wana kwenda KUSALI MSIKITINI. Wamepigwa Risasi sababu walijikuta wako ktkt ya hilo kundi la majambazi.
Askari kala kiapo cha kulinda wananchi na mali zao . We ulitaka askari wote wauwawe ?
 
It takes Brain to decide so. Swali la kujiuliza hiyo Brain ipo?. Binafsi hiyo akili siioni si kwake tu, hata kwa wanamzunguka.
 
Dah!

Ni kama humjui Samia Suluhu Hassan.
Matumaini yako na mapendekezo yako yote hapa, hakuna hata moja atakalo, siyo tu kulizungumzia bali hata kuthubutu kulisogelea.

Samia Suluhu Hassan ni kielelezo halisi cha watu walaghai, wasiokuwa na hata chembe ya soni usoni kwake..

Ngoja nikukukmbushe machache yanayoweza kuamsha akili yako kama umesahau tabia mbovu kabisa za mtu huyu.
Anza na wakati anaingia kuchukuwa nafasi ya Magufuli, kwa gia ya hadaa kabisa ya "Kazi Iendelee"; wakati uleule akishaanza kushikiliwa na akina Roastam Azizi na mipango ya ile sinema yake ya utalii! Kama huoni hadaa hapa; huwezi kuona hadaa karibu zote alizozifanya kuwavuruga waTanzania.

"Kazi na Iendelee" huku akijinadi "kufungua nchi"! "Hapa Kazi Tu", na "Kazi iendelee" vinakutania wapi hapo?

Samia ni kama alikuwa akisubiri kwa hamu kubwa Magufuli aondoke ili atekeleze ajenda aliyokuwa tayari amaiandaa; maana, hata udongo kwenye kaburi la mtangulizi wake ulikuwa bado ni mbichi kabisa. Alikuwa na haraka ya kwenda wapi?

Ulaghai haukuishia hapo, bali kajifanya yeye anawajali sana waTanzania kuliko serikali aliyokuwa akitumikia akiwa Makamu wa Rais. Lugha tamu, na visauti vya kisanii katika zungumza yake kaviweka kazini kupumbaza waTanzania waone yeye alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa wakiumia kimya kimya wakati wapinzani wakipewa shuruba na mkuu wake.
Kwa hiyo kwa hadaa kubwa, kabuni anataka "Maridhiano na Mbowe".
Lakini katika hili pia ni vizuri kukumbusha kuwa tabia zake za kikatili zilishaanza kujitokeza; wakati anasisitiza Mbowe ni Gaidi, na magaidi wenzake walishawekwa gerezani; kama alivyosema yeye. Wakati akiyasema haya, alikuwa amepania kwelikweli kummaliza Mbowe na CHADEMA yake kupitia huko mahakamani,

Kesi ilipoanza kuonekana kuwa haina miguu, haraka haraka karuka vihunzi na kutafuta njia nyingine ya kumlaghai Mbowe kwa njia ya Mazungumzo ya Maridhiano; huku akijuwa wazi anampeleka tu Mbowe chakani.

Watu wanawasingizia wahafidhina wa CCM kuyakataa mapendekezo ya liyowasilishwa na CHADEMA; lakini ukweli wenyewe ni kwamba hiyo ilikuwa ni kazi ya Samia Suluhu Hassan; mtu usiyeweza kumwamini kwa lolote asemalo.

Kwa hiyo kama bado huamini kuwa Samia Suluhu Hassan ni mwanamke mwenye tabia mbaya kabisa, matukio ya hivi karibuni nayo bado unayo mashaka juu yake?
Kuanzia kwenye kujiteua mwenyewe kuwa mgombea pekee hadi kukataa kwa maksudi kabisa ushauri wa kufanyika marekebisho madogo ili uchaguzi uwe wa haki na huru; wewe unataka uambiwe kitu gani kuonyesha uovu mkubwa uliomjaa huyu mwanamke

Na katika yooote hayo niliyo eleza hapo juu, hakuna hata moja analojutia, wala kukubali tu kwamba (by hind sight) kuwa makosa yalifanyika!

Umemsikia lini akizungumzia kwa umakini wowote kuhusu waTanzania kupotea, kutekwa na kuuawa? hawa waliouliwa juzi yeye na machawa wake wanalaumu uharibifu wa miundombinu; kana kwamba watu wametoka tu majumbani mwao kwa hasira za kuwepo miundombinu hiyo!

Bila aibu, kiongozi wa nchi unasema vijana toka nje ndio waliokuja kufanya vurugu hapa; na kama hilo bado halitoshi, hao ni vijana waliolipwa kwenda kuandamana!

Sasa akina 'Mzee Mwanakijiji', bado wanayo mategemeo ya mtu wa aina hii kukubali na kujutia yote yaliyotokea. Ajutie kitu gani wakati kishafanikiwa lengo lake la kubaki madarakani kwa nguvu.
Anachotafuta sasa ni kuhakikisha panakuwepo na AMANI itakayoletwa na mitutu ya bunduki!

Haya mengine yooote, ni ulaghai ule ule kama ulivyofanyika wakati Bandari ikiuzwa

Na ni wazi kukomalia kote huku ni kuhakikisha mipango ya uharibifu zaidi kwa raslimali za nchi hii unafanyika katika huo muda atakaokuwa mtawala asiyehojiwa na yeyote.

Mkuu 'Mzee Mwanakijiji', mapendekezo yako ni mazuri kwa mtu aliye na ubinaadam ndani yake; siyo kwa mtu kama huyu Samia Suluhu Hassan.
Njia pekee waliyobaki nayo waTanzania kwa huyu shetani ni kumwondoa kwa nguvu; hakuna njia nyingine tena.
 
Kumsaidia muhalifu na wewe unakuwa muhalifu.
Ninakubaliana na wewe, ndio maana woote wanaokubali kutumika katika nafasi mbalimbali anazowateua, watu hao baada ya ukombozi wasiruhusiwe kushika nafasi nyinginezo tena. Hawa nao ni waovu vilevile.
 
Teh teh teh.
Hizo mbege mnazokunywa bila kula zina madhara mabaya sana.
Yaani unataka ASKARI alieua majambazi walikuwa wanavunja na kupora mali za RAIA wawajibishwe?

🤣🤣
Kumbe Hilo swala la 29 ndivyo linavyo someka kwa vibogoyo wa akili hapo ikulu na kwenye vyombo vya wauwaji wanaojiita wana usalama? BASI TUKUTANE ICC TU HAKUNA NAMNA
 
Uliandika vyema huko juu. Sasa hapa wewe unatakaje? Samia huyo huyo aendelee kwa vile tunaogopa gharama?
Kuna gharama kubwa kushinda gharama ya kuwa na Samia kuwa mtawala?

Ningekuelewa kama angalau ungependekeza njia mbadala, kama kuwepo na serikali ya mpito.
 
Hakuna gharama kubwa zaidi ya kuweka nchi katika amani. Nilimsikia mwemyekiti wa tume akisema gharama za vifaa pekee ni zaidi ya bilioni 300. Sasa unataka kulinganisa bilioni 300 na nchi kuingia ktk machafuko? Ni afadhali kuchoka hata trilioni 5 ila nchi ibaki salama. KUANZA UPYA SIO UJINGA
 

Very naive commentary....

Asking her to hold accountable police officers responsible for the massacre indicates that you think she was not involved.

A thoughtless, ass-kissing, clue-less viewpoint.

You DO NOT know what was the chain of command that ordered the carnage. Stop yapping.
 
Inasikitisha sana
 
Umechoka kumtetea?
 
Wahuni wanamshikilia mateka. Hawezi kusema chochote cha maana zaidi ya bla bla tu za hapa na pale.
Nawe bado unaamini hili la "kushikiliwa"?
Una maana bila ya "kushikiliwa" angeanya mambo tofauti na ilivyo sasa?

Unataka akuonyeshe alama zipi ili uamini kuwa yeye ndiye mhusika hasa, na siyo kushikiliwa na watu wengine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…