Pengo la Capt. John Komba halijazibika, tayari wimbo ungekuwa hewani muda huu

Pengo la Capt. John Komba halijazibika, tayari wimbo ungekuwa hewani muda huu

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,914
Reaction score
168,320
Captain John Komba alikuwa na kipaji chake Cha ajabu kabisa.

Alikuwa na uwezo wa kutunga wimbo mzuri sana, wenye ujumbe mzuri na wenye hekima za Hali ya juu Ndani ya dakika chache. Kwa Mara ya kwanza nilimsikia mwaka 1984 alipofariki Hayati Edward Moringe Sokoine.

Ndani ya muda mfupi alitunga wimbo wa maombolezo, ukaruka Radio Tanzania 🇹🇿 Dar es Salaam. Alifanya hivyo pia mwaka 1986 alipofariki Hayati Samora Machel.

Ndani ya muda mfupi aliliamsha bonge la dude, achana na dude linaloamshwa na mshindi wa tatu pale Kawe. Alipofariki Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ndio akatoa na album nzima kabisaaaaaàa.

Muda huu tunapomuombolezea mpendwa wetu Hayati BENJAMIN MKAPA Rais wa awamu ya tatu, tayari wimbo ungekuwa hewani.

Tanzania 🇹🇿 tumempoteza mwanamuziki mahiri.
Buriani Captain John Komba.
Buriani Benjamin Mkapa
 
😄😄😄Bujibuji kwamba 1984ulimskia😀😀..haukua na akili hiyo mzee baba usituchoshe hapa lol😄😄! Miaka 6 huez kumbuka mambo Kama hayo ...
Njoo PM nikuimbie wimbo wenyewe, nikusimulie wakati Nyerere anatangaza msiba wa Taifa ilikuwa ni saa ngapi, na Mimi nilikuwa wapi na dudu proof yangu.
Kila mtoto na akili Yake, wengine tuko extra smart ndio maana hata huku JF hatuna cha kufanya ila michezo ya kuigiza tu
 
Hahahahahhah
Hahahahhaa....uwiii haya buji..
 
Back
Top Bottom