Pengo la Capt. John Komba halijazibika, tayari wimbo ungekuwa hewani muda huu

Pengo la Capt. John Komba halijazibika, tayari wimbo ungekuwa hewani muda huu

Nakumbuka kipindi cha kampeni 1995, Capt vs Nyimbo za uswahilini za kumsifu Mrema...ilikuwa burudani tu.

Ameumaliza mwendo jasiri.

Mpaka sasa sijaona bandiko lolote la kuhusu INGEKUAJE kama msiba huu ungetokea wakati PRINSI yupo kwenye piki NA pale msibani watakapokuwa wamekaa wanene wa njii hii, atakuwa anachungulia kwa wapi ikiwa hata kwenye ile krimu ya chama hayupo? Nimewaza tu.
 
Captain John Komba alikuwa na kipaji chake Cha ajabu kabisa.

Alikuwa na uwezo wa kutunga wimbo mzuri sana, wenye ujumbe mzuri na wenye hekima za Hali ya juu Ndani ya dakika chache.

Kwa Mara ya kwanza nilimsikia mwaka 1984 alipofariki Hayati Edward Moringe Sokoine.

Ndani ya muda mfupi alitunga wimbo wa maombolezo, ukaruka Radio Tanzania 🇹🇿 Dar es Salaam.

Alifanya hivyo pia mwaka 1986 alipofariki Hayati Samora Machel.

Ndani ya muda mfupi aliliamsha bonge la dude, achana na dude linaloamshwa na mshindi wa tatu pale Kawe.

Alipofariki Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ndio akatoa na album nzima kabisaaaaaàa.

Muda huu tunapomuombolezea mpendwa wetu Hayati BENJAMIN MKAPA Rais wa awamu ya tatu, tayari wimbo ungekuwa hewani.

Tanzania 🇹🇿 tumempoteza mwanamuziki mahiri.
Buriani Captain John Komba.
Buriani Benjamin Mkapa
Very very true...!!!
 
Diamond ataimba Nini?
Anaweza kuimba
Yoyo Yoyo papuchi nakupenda
Papuchi utaniuwa,
Ooh eeehe Papuch ni tamu sanaa

Moyo unauma nakupenda Sana
Sweet sweet Papuch sikuachi tena

Utopolo mtupu vilaza hao
 
Kipindi cha corona kuna watu wakauchukua wimbo ule wa 'mgeni' wakaedit kuhusu corona. Lakini bado haujafikia original ya marehemu.
Baada ya kupata taarifa za kifo cha Mkapa kichwani unazunguka wimbo wa 'ndugu watanzania leo yametimia' naingia huku nakuta huu uzi. Kweli jembe angekuwepo angeshatoa wimbo.

Wapumzike kwa amani
 
kwa nini hivi vitoto tunyimbo twao beat zinafanana wimbo wa kwanza mpaka wa mwisho 😳 😳
 
CCM wenyewe wanajitahidi kuziba pengo la Komba kwa kuwaloga akili kizazi hiki cha bongo fleva kuwasifia.Wasanii wanaimba kila siku nyimbo za kusifia ila hamna hata iliyojitahidi kufika walau nusu tuu ya CCM mbele kwa mbele.
 
Acha na ile NAMBARI ONE EEEH NAMBARI ONE CCM
 
New-generation musicians are generally not capable of producing custom-made songs. Ni watunzi wa generic songs (mostly za mapenzi na mipasho)!
Mnawaonea bure tu hawa wanamziki wa sasa !!kamwe tusilinganishe vipaji na waigizaji...
 
"Sasa kumekuchaa",,,sasa kumekuchaa jogoo limeshawika Dodomaa.
"wembe ni uleule ushindiii",,wembe ni uleule ushindii.
"Tumejipanga mwaka huu wataisoma"
Ushindi wa CCM huwa unatoka angle tofautitofauti ikiwemo na nyimbo nzuri za hamasa.
 
Captain John Komba alikuwa na kipaji chake Cha ajabu kabisa.

Alikuwa na uwezo wa kutunga wimbo mzuri sana, wenye ujumbe mzuri na wenye hekima za Hali ya juu Ndani ya dakika chache.

Kwa Mara ya kwanza nilimsikia mwaka 1984 alipofariki Hayati Edward Moringe Sokoine.

Ndani ya muda mfupi alitunga wimbo wa maombolezo, ukaruka Radio Tanzania 🇹🇿 Dar es Salaam.

Alifanya hivyo pia mwaka 1986 alipofariki Hayati Samora Machel.

Ndani ya muda mfupi aliliamsha bonge la dude, achana na dude linaloamshwa na mshindi wa tatu pale Kawe.

Alipofariki Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ndio akatoa na album nzima kabisaaaaaàa.

Muda huu tunapomuombolezea mpendwa wetu Hayati BENJAMIN MKAPA Rais wa awamu ya tatu, tayari wimbo ungekuwa hewani.

Tanzania 🇹🇿 tumempoteza mwanamuziki mahiri.
Buriani Captain John Komba.
Buriani Benjamin Mkapa
Yeye hakutungiwa wimbo lakini, siyo poa kabisa!
 
Kwa swala la maombolezo hapa TZ wimbo wa Dr. Remmy Ongala Mtoro ndio wimbo wa muda wote.
Nakumbuka alipokufa mwalimu nyerere wimbo wa Remmy ulipigwa mara mbili tu! Mkapa akaupiga marufuku maana ukiusikiza vibaya unachoma kumoyo (hasa verse za "mbele ya kifo hautambi, kifo ni kiboko yao nk)

Yeye Nkapa ndio anaombolezewa kwa wimbo huo.

Tembeeni kifua mbele, korona imeisha.
 
Back
Top Bottom