Pengo la Capt. John Komba halijazibika, tayari wimbo ungekuwa hewani muda huu

Pengo la Capt. John Komba halijazibika, tayari wimbo ungekuwa hewani muda huu

Wasanii wasasa hata, wakitunga jumbe zao zinawahi kufubaa kama utamu wa bigijii,huenda kwa sababu wanatunga kwa malengo ya biashara zaidi kuliko kufikisha ujumbe kwa jamaa , kuelimisha , kukosoa, kupongeza pale panapo hitajika kweli kusifia ila sio sifa za unafiki!!cap john alikuwa hafanyi kwa lengo la kibiashara ni kipaji haswa alikuwa anakitendea kazi
 
Wasanii siku hizi hakuna si unaona hata bendi ya TOT toka mwamba wa lituhi ufariki ni kama vile bendi imekufa tu maana hawasikiki tena
 
Captain John Komba alikuwa na kipaji chake Cha ajabu kabisa.

Alikuwa na uwezo wa kutunga wimbo mzuri sana, wenye ujumbe mzuri na wenye hekima za Hali ya juu Ndani ya dakika chache.

Kwa Mara ya kwanza nilimsikia mwaka 1984 alipofariki Hayati Edward Moringe Sokoine.

Ndani ya muda mfupi alitunga wimbo wa maombolezo, ukaruka Radio Tanzania 🇹🇿 Dar es Salaam.

Alifanya hivyo pia mwaka 1986 alipofariki Hayati Samora Machel.

Ndani ya muda mfupi aliliamsha bonge la dude, achana na dude linaloamshwa na mshindi wa tatu pale Kawe.

Alipofariki Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ndio akatoa na album nzima kabisaaaaaàa.

Muda huu tunapomuombolezea mpendwa wetu Hayati BENJAMIN MKAPA Rais wa awamu ya tatu, tayari wimbo ungekuwa hewani.

Tanzania 🇹🇿 tumempoteza mwanamuziki mahiri.
Buriani Captain John Komba.
Buriani Benjamin Mkapa
Kipindi kile alivyo kufa Makamu wa Rais Dr Omary Ali Juma,kesho yake akaachia nyimbo

"Omary Ali Juma,umemuuacha mkapa na nani..........."

Komba alikuwa mzuri kwenye kutunga nyimbo za kuomboleza.

RIP Mkapa & Dr Omary.
 
Tulikua naye siku zote za mapambano,

Mwenzetu,

Ndugu yetu,

Akaja kumkunjia Mpoki kwa kumuiga. Ikasemwa alikua anammega Lulu
 
Wakitunga hapa hamna malipo .. Za kampeni zinatunzo
 
Mtunzi bora wa nchi za kusini mwa jangwa la Africa ni Enoch Mankayi Sontonga.
Mtunzi bora wa nyimbo za chama na taifa Tanzania kpt Komba.

Lakin wote baada ya vifo vyao sioni kama mchango wao unaenziwa sawa na juhudi zako enzi za uhai wao.

Nais ndivyo ninavyo fikiri
 
Sasa kama aliekuwa anatunga alishatangulia mbele za haki kwanini tusijiongeze sisi wana JF Tukatoa bonge mmoja la nyimbo mwimbaji akiwa Don Nalimison, mpiga kinanda Bujibuji , mtengeneza biti mimi mwenyewe Okwanyo58 hapo nadhani sasa itapendeza 😁🤪🏃
 
Siku hizi wanatumia miguvu badala ya akili.
 
Inaweza asitokee Tena Tanzania Kama Marehemu Captain Komba
 
Mkuu, usitarajie Wabanapua kuimba jambo la maana. Capt. John Damian Komba was exceptional
 
Jaman mwny nyimbo ya komba kumuimbia samora machel, sokoine na za nyerere ziweke hapa
 
Back
Top Bottom