Pengo la Capt. John Komba halijazibika, tayari wimbo ungekuwa hewani muda huu

Pengo la Capt. John Komba halijazibika, tayari wimbo ungekuwa hewani muda huu

Captain John Komba alikuwa na kipaji chake Cha ajabu kabisa.

Alikuwa na uwezo wa kutunga wimbo mzuri sana, wenye ujumbe mzuri na wenye hekima za Hali ya juu Ndani ya dakika chache.

Kwa Mara ya kwanza nilimsikia mwaka 1984 alipofariki Hayati Edward Moringe Sokoine.

Ndani ya muda mfupi alitunga wimbo wa maombolezo, ukaruka Radio Tanzania 🇹🇿 Dar es Salaam.

Alifanya hivyo pia mwaka 1986 alipofariki Hayati Samora Machel.

Ndani ya muda mfupi aliliamsha bonge la dude, achana na dude linaloamshwa na mshindi wa tatu pale Kawe.

Alipofariki Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ndio akatoa na album nzima kabisaaaaaàa.

Muda huu tunapomuombolezea mpendwa wetu Hayati BENJAMIN MKAPA Rais wa awamu ya tatu, tayari wimbo ungekuwa hewani.

Tanzania 🇹🇿 tumempoteza mwanamuziki mahiri.
Buriani Captain John Komba.
Buriani Benjamin Mkapa
Na nyimbo za marehemu komba zingeliimbwa na watu wa dini na imani zote. Wasanii wasasa ngoja wakitoa nyimbo hautaamini macho na msikio yako, video zitakuwa na mbwembwe kibao kama vile wako lunc
 
Kweli pengo lake halizibiki kamwe.
 
huyu mwamba alikua kiboko
nahisi alikua anapewa habari kabla maana nyerere kafariki yeye akaja na albam nzima duh
nakumbuka nilikua primary mda wa mchana tunaingia sehemu ya kula tv juu inaonyesha nyimbo za maombolezo kifo cha mwl dah
tumerudi darasani watu wote tunalia machozi 😢😢😢😢
 
Jamaa alikuwa ni NGULI zaidi ya Victor Tesha
 
Wasanii tunaomba nyimbo hata mki copy za komba zibadirisheni zihusu msiba uliombele yetu kwa sasa, mkisema mtunge zenu zitakuja kutoka mzee kaisha zikwa kitambo na jamii umesahau.
 
Captain John Komba alikuwa na kipaji chake Cha ajabu kabisa.

Alikuwa na uwezo wa kutunga wimbo mzuri sana, wenye ujumbe mzuri na wenye hekima za Hali ya juu Ndani ya dakika chache. Kwa Mara ya kwanza nilimsikia mwaka 1984 alipofariki Hayati Edward Moringe Sokoine.

Ndani ya muda mfupi alitunga wimbo wa maombolezo, ukaruka Radio Tanzania [emoji1241] Dar es Salaam. Alifanya hivyo pia mwaka 1986 alipofariki Hayati Samora Machel.

Ndani ya muda mfupi aliliamsha bonge la dude, achana na dude linaloamshwa na mshindi wa tatu pale Kawe. Alipofariki Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ndio akatoa na album nzima kabisaaaaaàa.

Muda huu tunapomuombolezea mpendwa wetu Hayati BENJAMIN MKAPA Rais wa awamu ya tatu, tayari wimbo ungekuwa hewani.

Tanzania [emoji1241] tumempoteza mwanamuziki mahiri.
Buriani Captain John Komba.
Buriani Benjamin Mkapa
Mbona wasanii hawaungani kutoa wimbo wa kumuenz Uncle Ben kma zile za kusifu
 
Back
Top Bottom