Pesa inaweza kuja kwenye maisha yako bila kutarajia

Pesa inaweza kuja kwenye maisha yako bila kutarajia

😹😹😹 Hizi deal za pesa tunaziogopa bure wakati hii dunia tumeletwa kuenjoy na kusepa..!! Tutapiga kelele kila siku watu wanatuibia wanasukuma mipila ya mwaka wa mbele wakati na sisi tunao uwezo wa kuiba..!!
😂😂😂Unapenda sana mambo ya kihabesh..Siku ukifuata mzigo China tutafute wateja wa kuletewa mzigo ,akichagua pochi za elfu 15 tunamletea mzigo wa pochi za buku jero
 
Watu washenzi sana nilikuwa naangalia story ya Hans Pope sasa hivi kwa Milard Ayo yaani kafa 2021 kuna nyau zikakopa benki bn.7 kwa jina lake na kuweka mali zake kama bond mwaka 2024 na sasa hivi benki ndio imeibuka kukamata magari yake hata wasimamizi wa mirathi hawana habari.
 
Kwenye dili jifanye mpole, ww kuwa na timing...wapiga dili wote wa pesa kubwa duniani ukikutana nao kabla hamjaongea sura zao ni za kipole na zina Kama ushamba Fulani hivi, anakusikiliza Kwanza weee ukiongea, hajibu moja Kwa moja, mnaachana Kwanza ww utajua ume win then baadae from nowhere analeta akili za ajabu ambazo hukutarajia na Kwa kuwa wewe hukutarajia basi lazima ujichanganye mwishon...Na ndio maana utakuta matajiri wakubwa sio waongeaji Sana au wanaongea taratibu Sana, very calculative.
 
IMG_3614.jpeg
 
MWISHO.
Basi bwana, tukaaondoka na kaka yangu, yule rafiki yake anaendesha mimi nimekaa siti ya nyuma tunadiscuss issue,ghafla ikaingia meseji sista usitoe hela kizembe hapa huyu tia mafuta tu kwanza mengine tutaongea baadae,Basi nikajiongeza nikawaambia bro mimi natakiwa sehemu mnaweza ni drop hapa?nikamwambia nakutumia ya mafuta,basi nikamrushia laki,sijui alimtoaje mshkaji ila baadae kidogo akanipigia akamsagia mwenzie kunguni akatangaza shida zake akaomba nimkopeshe 300,000...Nikasema 300,kitu gani mtu kaniokoa kwenye mdomo wa mamba nikatuma na ya kutolea.

Hapo simu zinaita balaa, Ikikata ya Bena inaita ya Muddy,Bena ananitumia meseji tamutamu za kunilaghai na kujifanya it's okay sisi tukutane wenyewe tuongee mambo yetu,nikamtumia meseji moja tu"KOSA ULIILOFANYA NI KUNIONA MIMI MBWIGA"..Sikupokea simu yake teeeeena, Huyo Muddy sasa ananipiga mikwala sio ya nchi hii!Muddy anaapa na mizimu yake yote lazima anifanye kitu cheusi,hata kuvuka bahari atavuka ataenda Tumbatu atanirushia jini anasema mimi ni mshamba na mtoto mdogo sana siwezi msumbua akili,Rohoni nasema liwalo na liwe waniue tu! ila moyo unadunda kiaina,Kweli sikuwa sawa!nilikuwa NAOGOPA.
Nikasema leo silali nyumbani hawa jamaa wataniletea majambazi,nina dada yangu huko pembezoni nwa jiji nikampigia simu nikamwambia nakuja,nikaenda zangu huko!Asubuhi tulivyoamka nikampa issue yote yeye ni mjasiriamali na mlokole mzuri,dada akaniambia ndugu yangu hiyo pesa imetoka kwa Mungu mwenyewe,hilo ni DENI nikapewa mistari pale nakumbuka akatoa mfano wa wale waliopewa talanta,akasisitiza hiyo hela lazima izae na nirudishe rejesho kiuaminifu na bwana atanibariki,Yaani ni kama alinifanyia tiba kisaikolojia,maana kiukweli nilikuwa bado nina butwaa na zile hela na mchecheto yaani nisingeenda kwa sista zile hela zingenikoma,maana shetani alikuwa anainong'oneza cha kwanza nenda kwa Yussufer Jewellery nikachukue cheni gram 5 pure gold na here ni na pia niende kwa Aristote nikanunue Peruvian hair moja kali sana...ila kiukweli dada alisaidia sana,yaani ni kama alinisaidi kuisimamia ile pesa,kwa vile tayari nilikuwa na vibiashara vyangu basi tukaboresha nyingine akasema hii iache kwanza basi nikaanza kuzungusha Mungu si Athmani nikaweza kulipa marejesho japo kiukweli marejesho yanapasua kichwa sana!

Kitu ninachoweza kusema kipindi hicho kwa kweli niliishi maisha flani bila uhuru,nilikuwa na wasiwasi yaani sikuwa na amani maana siku kama ya tatu nilitoa ile line nikabadilisha number,kwa kuwa sio watu tunaojuana sana hawakuweza kupata number yangu kiurahisi na yule Bena alishindwa kupeleka mashtaka kwa Andy .

Ikapita kama baada ya miezi saba ndio nikampa story Andy akasema wewe una balaa wewe hivi unamjua yule Bena wewe?jamani nilivyopewa mikanda yake ile niliyosikia mwanzo ni robo tu!
Basi nilipambana japo kuna miezi nilikuwa nasumbua marejesho ila nikamaliza ,Kifupi nilipotea sana mjini nilikuwa sizururi hovyo sikutaka kuingia kwenye matatizo na wale jamaa

Jamani mimi niishie hapo.
Tuwe Makini,Bongo Dar es Salam.
Shukrani zangu ziende kwa Mola wetu Mlezi.
Wakatabahu!
story kali. Asante kwa darasa Sis Joh umeshakuwa mutoto wa mujini. Umecheza kimafya sana.

Matapeli wako very smart. Wanaijua psychology yenyewe ukiacha ile ya makaratasi 😁.
 
Mkuu niliwahi kukuona kinondoni ni mwembamba hivi na dreads bisha.
 
Back
Top Bottom