Pesa inaweza kuja kwenye maisha yako bila kutarajia

Pesa inaweza kuja kwenye maisha yako bila kutarajia

Sis nimesoma huku nacheka sana huwezi amini aiseee..!! 😹😹

Waabeshi wamekufundisha undava.
Niwe mkweli hizo dili mi nishawahi kuzipiga na bro mmoja hivi siwezi kumtaja. Kuna mwingine huyo alikua ndio hatari anaitwa Pablo mtoto wa Manzese (RIP). Huyo safu yake anampanga mkewe front.. kaimbwa sana na Twanga pepeta miaka hiyo..!!

Kuna kitu nikikisema tayari file langu litashuka chap..!! Platform km hii waabeshi wapo wengi wanaishi kwa code..!!
🤣🤣🤣🤣Unajua kilichoniuma ni kuwa kwenye game kumbe we mwenyewe ndio target!dah tuangushie file ikikupendeza mdogo wangu tu enjoy mambo ya waabeshi
 
Sasa hivi wanaondoka na kichwa chako kweupe halafu jumba bovu wanaangushiwa veggies..!! 😹😹

Sasa huku kkoo kuna michezo michafu. Watu wanapigwa pesa wanarudi mikoani kimya kimya..
🤣🤣🤣🤣🤣 dah kwa hiyo unaambiwa lipia kilemba na frame hupewi?dah lazima urudi Tunduma
 
MWISHO.
Basi bwana, tukaaondoka na kaka yangu, yule rafiki yake anaendesha mimi nimekaa siti ya nyuma tunadiscuss issue,ghafla ikaingia meseji sista usitoe hela kizembe hapa huyu tia mafuta tu kwanza mengine tutaongea baadae,Basi nikajiongeza nikawaambia bro mimi natakiwa sehemu mnaweza ni drop hapa?nikamwambia nakutumia ya mafuta,basi nikamrushia laki,sijui alimtoaje mshkaji ila baadae kidogo akanipigia akamsagia mwenzie kunguni akatangaza shida zake akaomba nimkopeshe 300,000...Nikasema 300,kitu gani mtu kaniokoa kwenye mdomo wa mamba nikatuma na ya kutolea.

Hapo simu zinaita balaa, Ikikata ya Bena inaita ya Muddy,Bena ananitumia meseji tamutamu za kunilaghai na kujifanya it's okay sisi tukutane wenyewe tuongee mambo yetu,nikamtumia meseji moja tu"KOSA ULIILOFANYA NI KUNIONA MIMI MBWIGA"..Sikupokea simu yake teeeeena, Huyo Muddy sasa ananipiga mikwala sio ya nchi hii!Muddy anaapa na mizimu yake yote lazima anifanye kitu cheusi,hata kuvuka bahari atavuka ataenda Tumbatu atanirushia jini anasema mimi ni mshamba na mtoto mdogo sana siwezi msumbua akili,Rohoni nasema liwalo na liwe waniue tu! ila moyo unadunda kiaina,Kweli sikuwa sawa!nilikuwa NAOGOPA.
Nikasema leo silali nyumbani hawa jamaa wataniletea majambazi,nina dada yangu huko pembezoni nwa jiji nikampigia simu nikamwambia nakuja,nikaenda zangu huko!Asubuhi tulivyoamka nikampa issue yote yeye ni mjasiriamali na mlokole mzuri,dada akaniambia ndugu yangu hiyo pesa imetoka kwa Mungu mwenyewe,hilo ni DENI nikapewa mistari pale nakumbuka akatoa mfano wa wale waliopewa talanta,akasisitiza hiyo hela lazima izae na nirudishe rejesho kiuaminifu na bwana atanibariki,Yaani ni kama alinifanyia tiba kisaikolojia,maana kiukweli nilikuwa bado nina butwaa na zile hela na mchecheto yaani nisingeenda kwa sista zile hela zingenikoma,maana shetani alikuwa anainong'oneza cha kwanza nenda kwa Yussufer Jewellery nikachukue cheni gram 5 pure gold na here ni na pia niende kwa Aristote nikanunue Peruvian hair moja kali sana...ila kiukweli dada alisaidia sana,yaani ni kama alinisaidi kuisimamia ile pesa,kwa vile tayari nilikuwa na vibiashara vyangu basi tukaboresha nyingine akasema hii iache kwanza basi nikaanza kuzungusha Mungu si Athmani nikaweza kulipa marejesho japo kiukweli marejesho yanapasua kichwa sana!

Kitu ninachoweza kusema kipindi hicho kwa kweli niliishi maisha flani bila uhuru,nilikuwa na wasiwasi yaani sikuwa na amani maana siku kama ya tatu nilitoa ile line nikabadilisha number,kwa kuwa sio watu tunaojuana sana hawakuweza kupata number yangu kiurahisi na yule Bena alishindwa kupeleka mashtaka kwa Andy .

Ikapita kama baada ya miezi saba ndio nikampa story Andy akasema wewe una balaa wewe hivi unamjua yule Bena wewe?jamani nilivyopewa mikanda yake ile niliyosikia mwanzo ni robo tu!
Basi nilipambana japo kuna miezi nilikuwa nasumbua marejesho ila nikamaliza ,Kifupi nilipotea sana mjini nilikuwa sizururi hovyo sikutaka kuingia kwenye matatizo na wale jamaa

Jamani mimi niishie hapo.
Tuwe Makini,Bongo Dar es Salam.
Shukrani zangu ziende kwa Mola wetu Mlezi.
Wakatabahu!
Imepita miaka mingapi tangu hilo tukio? Are you safe now?

Hongera kwa kumaliza deni.
 
Dar nyumba moja ina hati 10 za mchongo.
Watu washalia sana, waliwahi kupelekana wamiliki wawili mahakamani na wote sio wamiliki halali. Mwenye hati OG katulia pembeni anawachora kashakatiwa mpunga..!!

Hao wenyeviti wa mitaa ni matapeli wakubwa na kampeni zao sponsor ni waabeshi..!! Dar vitu vinapangwa kimkakati.
Kabisa kabisa yaani!hamna watu washenzi kama wenyeviti siku ile tunaondoka wanasisitiza wapelekwe wateja wengine kuna majumba mazuri mazuri yanatoa hadi 200M🤣🤣🤣🤣nikasema makibuyu!
 
Kuongea na watu kunasaidia
Yah yani iliniumiza kichwa sana hiyo mission nikamuambia wife ila naye akawa haelewi maana mtu anakupa dili ganji 20m in a week...
Ikabidi nimfuate mshikaji wake jamaa nikamsanua aah ndio akaniambia jamaa unapangwa....

Hapo nishasainishwa mikataba na kuonyeshwa PO na invoice za kutosha....

Mwisho wa siku nikawaambia mikataba atasimamia wakili. Nikampa wakili 20k aongee nao kwenye simu.

Baada ya hapo mikataba ikayeyuka...
 
Mjini pagumu sana nilitakaga kupangwa nitoe kahela kangu nilikotafuta miaka mitatu kwa jasho na damu. Mtu akataka kunipiga kirahisi.

Ila nini!! Mtu sio nyau. Mtu atakunyima vyote ila sio maneno. Niliposhirikisha mtu tu. Aaah nilitoka nduki mwendo wa ngiri mkia juu kinyeo nje....
Wambea waishi sana!wanasaidia sana
 
😹😹😹 Kwahiyo jana tunabonga lingala ukajiuliza huyu mkongolee wa wapi tena?
Pale nilikuwa sijakutambua bado.
Ingekuwa tuna ongea PM, kuongopeana 'I luv yuu' ungenikamata vizuri tu hili parody...😜😜😆😆
Ile unaiomba kwa mtu wako bila kujua, yeye anakuchora tu.
 
Back
Top Bottom