Mbona rahisi sana,kama mnataka substances si mkasome Daily news,
Nitakupa mfano wa uhakika kuhus failure ya waandishi kushindwa kufokasi kwenye point, na baadaye kuwa na maneno mingi.
Zamani sana nikiwa mwanafunzi UDSM tulikuwa na somo linaitwa DS200, sijui kama bado lipo. Mwaka 1985, mojawapo ya mtihani wa somo hili liliuliza watahiniwa
kutathmini mafanikio ya CCM baada ya miaka miaka minane. Mwamba mmoja akatoa jibu lilioanza kwa kusema ilikujua mafanikio ya CCM, ni lazima kwanza uelewa asili ya CCM ni nini, na ili ujue asili ya CCM , lazima ujue mazingira yaliyosababisha vuguvugu la siasa nchini. Hivyo akaanza kuandika historia ya ukoloni kuingia nchini, kuanza kwa vyma vya TAA, Afro Party na Shiraz Party, baadaye akagusia jinsi TAA ilivyobadilika kuwa TANU na jinsi Afro Party ilivyonungana na Shiraz Party kuwa Afro-Shiraz Party (ASP). Akaendelea kueleza jinsi TANU ilivyopigania na kupata uhuru wa Tanganyika, na vile vile ASP ilivyopigaia uhuru wa Zanzibar na hadi kufanya mapinduzi. Baada ya Mapinduzi Zanzibar ikaungana na Tanganyika na kuwa Tanzania; ASP ikabaki na wanachame wake Zanzibar tu, wakati TANU ina wanachama wake kutoka Tangayika tu; jambo hilo halikuwa na tija kujenga umaoja wa kitaifa hivyo mwaka
1977 ASP iliungana na TANU na ndipo CCM ikazaliwa.
Alivyomaliza kuandika kuwa
ndipo CCM ikazaliwa, akaambiwa muda wa mtihani umekwisha; hivyo akasubmit makaratasi yake yakiwa na facts nyingi sana lakini ambazo zilikuwa hazijibu swali la mtihani. Hiyo ndiyo maneno mingi-zero substance.