Pesa ya kujikimu kwa wanafunzi ipunguzwe wapewe elfu 5 ikizidi sana elfu 6, pia pesa ya books and stationary iondolewe au nayo ipunguzwe.

Pesa ya kujikimu kwa wanafunzi ipunguzwe wapewe elfu 5 ikizidi sana elfu 6, pia pesa ya books and stationary iondolewe au nayo ipunguzwe.

Kama wabunge wanalipwa zaidi ya lak 3 kwa kusema ndio, mwisho wa mwezi zaidi ya milion 13, mafuta lita 1000 kwa wmezi, na kiinua mgongo cha miaka 5 zaidi ya mls 250 ambazo zote hizo ni pesa za walipa kodi, basi waache wanafunzi wapewe hiyo pesa maana ni mkopo wakimaliza wataulipa.
Punguzeni makasiriko sio kila kijana hiyo pesa anaitumia kwenye ulevi.
Mbunge anafanya kazi aliyotumwa na wananchi kwa manufaa ya wananchi anaowaongoza kwa hiyo faida ni kwa wote.
Vipi kuhusu huyo mwanachuo?
 
Elim ya chuo iwe Bure,yaani fedha za Ada zitumike kununua mahitaji ya chuo!!

Hostel na chakula viwepo chuoni,wanachuo wapewe fedha za staitonery TU na kujikimu mahitaji madogo tu!!

Hakuna haja ya kuwakopesha wanachuo fedha ambazo hawana uhakika was kuzirudisha kwasababu ya kukosa ajira!!
Hebu wacha hizo mkuu. Nafikri utaratibu wa canteen ni mzuri ila mdau ana hoja. Hela ya boom ipunguzwe ili wanachuo wote waliodahiliwa wapate hiyo kidogo kidogo. Sasa hivi hivyo vigezo walivyoweka vinasumbua sana kwa baadhi ya wanachuo waliokosa mkopo
 
Sioni mantiki ya kuwapa wanachuo elfu 10 ya kujikimu.

Tuongee tu uhalisia ,hiyo elfu 10 ni pesa ya mume ,mke na watoto ,sasa huyo mwanafunzi mnayempa elfu 10 kwa siku ya matumizi anakula au anatumia nini haswa ambacho ni tofauti na mtanzania mwengine wa maisha ya wastani?

Wanafunzi wakumbuke chuo wameenda kusoma na sio kuoneshana ufahari wa matumizi,

Hivyo bodi ya mikopo iwapunguzie hawa wanafunzi pesa kutoka elfu 10 wapewe elfu 5 ikizidi sana elfu 6 na si zaidi ya hapo.

Pia kuna hii pesa ya books and stationaries, kiukweli hakuna mwanachuo anayepoteza pesa yake kununua vitabu ,wengi wanasoma tu slides za walimu wao ikizidi sana wana google tu.

La kama kuna ulazima wa hivyo vitabu basi waende library na uzuri library nyingi vitabu wana azimisha kwa mwanafunzi anayehitaji.

Kwa hiyo hii pesa bora iondolewe tu.

Zingatieni hili kuna mahitaji mengi ya msingi kwa wananchi kuliko kuendelea kuwaendekeza hao.

Bora kiasi kipunguzwe na kielekezwe kwenye huduma zingine za msingi za kijamii.
Huna point ya msingi upuuzwe
 
Najaribu kulitazama hili kwa wabunge wote kwa kutumia mahesabu yafuatayo:

Let's say miezi 15.
Mh. Mbunge awe ameweka kibindoni...
207 000 000 ÷ 15 = 13 800 000
Nimechukulia mbunge awe let say analipwa kwa mwezi 13 800 000
Hii ni kwa yule ambaye hakuhudhuria vikao na kama halipwi posho ya kuhudhuria. The same formula applies to all.

Je, kama anayehudhuria vikao analipwa zaidi ya shilingi 350 000 kwa siku, kwa mwezi itakuwa kiasi gani ukijumlisha mshahara na marupurupu mengine?

Pole kwetu tunao lipwa mshahara wa mwezi ambao ni sawa na posho ya mbunge ya siku moja.
 
Mtu kapewa mkopo unamuonea wivu? Haitoshi pia unataka kumpangia na matumizi hata wapewe 20,000 kwa siku haina shida kama serikali Ina uwezo maana siku atazilipa mwenyewe.
 
Mbunge anafanya kazi aliyotumwa na wananchi kwa manufaa ya wananchi anaowaongoza kwa hiyo faida ni kwa wote.
Vipi kuhusu huyo mwanachuo?
Mwanachuo anasoma kwa manufaa ya nchi. Elimu anayopata anakuja kuajiriwa kuendesha na kusimamia an kutekeleza miradi kama ya maji, barabara, kutibu raia akiwemo viongozi na kadhalika huku akilipa mkopo. Yote hii ni wka manufaa ya nchi. Hakuna nchi iliyoendelea pasipo kuwa na wasomi. Viongozi wengi wana akili kama zako hawaoni direct relationship iliyopo baina ya elimu na maendeleo ya nchi.
 
Mtu kapewa mkopo unamuonea wivu? Haitoshi pia unataka kumpangia na matumizi hata wapewe 20,000 kwa siku haina shida kama serikali Ina uwezo maana siku atazilipa mwenyewe.
Asipo ajiriwa watampata wapi?
 
Mimi mwenyewe sikusoma Kwa mkopo baba yangu alikuwa ananipa hiyo Hela Sasa Kwa nini Serikali isiwajibike Kwa watu wake, haiingii akilini kuanzisha Uzi wa namna hii unless you're not a parent.
 
Mleta mada angesema ipunguzwe ili wanachuo wote wapate. Na siyo lazima iwe 5000 inaweza kuwa hata 7500 kwa siku ili inayobaki ikajazie kwa waliokosa!
 
Pesa wanakopeshwa hakuna mtu anapatiwa pesa ya bure hapo.

Hebu tujiulize kidogo wewe wakipewa hiyo elfu kumi shida kwako ni nini?mazingira ya chuoni ni sawa na nyumbani kwako mpaka ufanye comparison?

Wewe unajiko, gesi, kuni,kibanda chako cha kuishi,unga,mchele n.k.Je, wanachuo wote wanavyo hivyo kiasi kwamba kama bajeti ya elfu kumi ni practical kwako basi itakuwa kwa wengine pia

Anyway,roho mbaya haijengi.Kumbuka hiyo pesa wanalipa badae.
 
Kwanza kabisa kukiwa na usimamizi mzuri wa rasilimali nchini, hao wanachuo wanatakiwa kupewa hata elfu ishirini kwa siku Ili kuweza kutatua changamoto zao zote. Kwanini usiseme Wabunge na Mawaziri wasipunguziwe Posho na Mishahara mikubwa wanayokula pasipo na sababu ya msingi .
 
Kama hoja ni mkopo basi mkopo upunguzwe maana mkopo sio deni kwa mtoaji.

Pesa ipunguzwe ,maana hata wakimaliza wanaobahatika kupata ajira ni wachache hivyo kiwango kubwa cha pesa kimaisha kupoteza tu juu kwa juu
Kwahiyo hautaki Mtanzania mwenzako ale keki ya nchi hii, suala la ajira ilitakiwa serikali yenyewe iwe na uwezo mkubwa wa Kutengeneza Projects kubwa ambazo zitaajili watanzania wengi bila kusahau kuweza kusimamia hizo Projects kwa ubora unaokubalika. So acha vijana wafurahie uwepo wa rasilimali zetu.
 
Sioni mantiki ya kuwapa wanachuo elfu 10 ya kujikimu.

Tuongee tu uhalisia ,hiyo elfu 10 ni pesa ya mume ,mke na watoto ,sasa huyo mwanafunzi mnayempa elfu 10 kwa siku ya matumizi anakula au anatumia nini haswa ambacho ni tofauti na mtanzania mwengine wa maisha ya wastani?

Wanafunzi wakumbuke chuo wameenda kusoma na sio kuoneshana ufahari wa matumizi,

Hivyo bodi ya mikopo iwapunguzie hawa wanafunzi pesa kutoka elfu 10 wapewe elfu 5 ikizidi sana elfu 6 na si zaidi ya hapo.

Pia kuna hii pesa ya books and stationaries, kiukweli hakuna mwanachuo anayepoteza pesa yake kununua vitabu ,wengi wanasoma tu slides za walimu wao ikizidi sana wana google tu.

La kama kuna ulazima wa hivyo vitabu basi waende library na uzuri library nyingi vitabu wana azimisha kwa mwanafunzi anayehitaji.

Kwa hiyo hii pesa bora iondolewe tu.

Zingatieni hili kuna mahitaji mengi ya msingi kwa wananchi kuliko kuendelea kuwaendekeza hao.

Bora kiasi kipunguzwe na kielekezwe kwenye huduma zingine za msingi za kijamii.
Wanachuo wakikufahamu watakuburuzia kichakani ule vitasa.
 
Roho mbaya na ya kwann huwa haijengi inabomoa. Kwani mwisho wa siku si wanakopeshwa na huwa wanalipa? [emoji848]
 
Back
Top Bottom