Pesa ya kujikimu kwa wanafunzi ipunguzwe wapewe elfu 5 ikizidi sana elfu 6, pia pesa ya books and stationary iondolewe au nayo ipunguzwe.

Hatuna uchumi wa ku provide hiyo service kwa sasa
 
Tuongee uhalisia.
Elfu 10 kwa siku kwa mtu ambaye huna majukumu zaidi ya kusoma unaitumia vipi?
Kifungua kinywa 1500, mchana msosi 2000, usiku 2000, bando 2100, stationary 2000. Umekwisha pita uko ndio mana
 
Wewe .Aisha ya Watu maskini wanaotumia 10k Kwa Siku na familia ndio inakuwa reference na hoja yako kuu kuwa wanafunzi wasipewe hiyo hela kwa sababu kuna maskini wanatumia elfu 10 kwa siku na familia zao?


Embu fikiria vyema.
Huyo elfu 10 kwa siku haitoshi kwa mtu mmoja wewe unataka ipunguzwe.
 
Ameomba radhi kwa sababu za kisiasa .

Ila uhalisia mwanafunzi elfu 5 au 6 kwa siku inamtosha kabisa na inabaki.

Unajua kwa hapa DSM mwanafunzi wa shule ya sekondari kwa siku anapewa 2000-5000 na familia kama pesa ya kujikimu.

Mwanafunzi wa chuo mahitaji yake ya msingi ndio hiyo elfu 10. Hapo hujahusisha mambo ya taaluma yake wala anasa
 
Kula
Usafiri
Alipe pango,
mavazi
Bando
N.k
Pesa haitoshi mkuu, mtu mwenye familia ndio kabsa
 
Hako ka elfu kumi umeona ni hela sana?

Elfu kumi huwezi kula ata chips ukashiba!

Nashauri waongezewe iwe elfu 30 kwa siku.

Mbona akina Mwigulu wanatafuna mabilioni na hamlalamiki? Wewe ka elfu kumi tu jicho linakutoka!
 
...
 
Mwaka 2008 tulipewa 5000 na ilikuwa ngumu kuibalance,lazima upige pasi ndefu! Tena kipindi hicho soda 350,rb 600 wali nyama 800, sasa miaka 16 mbele mtu anataka irudi tena 5000 dah
 
Hatuwezi kufuata ushauri wa mtu ambae anajiita sina mood muda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…