Pesa ya Mwanamke ilivyotamu lazima niilambe! Huo ndio msimamo wangu

Pesa ya Mwanamke ilivyotamu lazima niilambe! Huo ndio msimamo wangu

1. Maisha YANANJIA yake.
2. Usisahau Mambo haya.
3. Nyota ya Tibeli.

RIWAYA
1. MLIO WA RISASI HARUSINI
2. WAKALA WA SIRI
3. SABOKA
4. Siku yangu ya kufa ILIPITA
5. Kaburi la Mwanamuziki
6. Mtoto wa MSUKULE
7. Kilio Pasipo machozi.

Vilivyosokoni
1. Mlio WA RISASI HARUSINI
2. Wakala wa Siri.
Navipataje!!?
 
PESA YA MWANAMKE ILIVYOTAMU LAZIMA NIILAMBE; HUO NDIO MSIMAMO WANGU!

Anaandika, Robert Heriel

Ujumbe huu ni Kwa Hustlers wote. Vijana wote mliotokea kwenye Familia Masikini! Usiogope Kula au kutumia pesa ya Mkeo.

Ati nisiitegemee pesa ya mwanamke, Nani kasema?
Pesa ya mwanamke lazima Taikon ailambe! Kama ni Mama yangu lazima niile, Kama ni pesa ya Mke wangu lazima niile. Hao watu wawili lazima pesa Yao niilambe kivyovyote. Nao wanauhalali wa Kula pesa yangu kivyovyote.
Hakuna Raha Kama pesa ya Mwanaume ikiliwa na Mkewe au Mamaye. Raha tuu.

Tabia za ubinafsi ndio zinafanya watu washindwe Kula Bata Duniani. Kama unaogopa Kula pesa ya mwanamke na umetoka familia Masikini. Nakupa pole Sana.

Sijali ninyi Walimwengu mtasemaje, mtajijua wenyewe na unafiki wenu. Hata hivyo kila mtu anakanuni zake.

Kwanza pesa ya mwanamke ni tamu licha ya. Kuwa inamasimango😀.

Hakuna pesa tamu Kama pesa upewayo na Mama yako, na Ile upewayo na Mke wako.

Kwanza ukipewa pesa na Mkeo au mchumba wako unakuwa unachekacheka Kwa aibu😂😂 nafsini ukijisemea hii pesa nitairudisha,lakini ukikiri kuwa huyu Mwanamke ni kweli ananipenda.

Kumbuka kuwa mwanamke kama hakupendi lazima awe mgumu na ajisikie vibaya kukupa pesa yake.

Lakini kama mwanamke anakupenda pesa zake utazila Sana. Zingatia, wanawake kiasili ni wachoyo na wachumi wa pesa. Yaani ili akupe pesa yake basi lazima akupende Sana, alafu mbili uwe mtoto wake wa kuzaa.

Mwanamke akikupa pesa yake wivu wake unaongezeka maradufu, na anataka uwe wake pekeake, yaani ni kusema achilia mbali kutaka kumiliki moyo wako lakini pia anataka na roho yako. Doooh! Lakini tavumilia Mimi!

Mario! Sijui umarioo! Sijui kulelewa! Mtatunga tungo na nyimbo kuniimba Taikon lakini Mimi ndio nimeshaamua.
Muhammad alikula pesa za Bi. Khadija. Haya wewe ni Muhammad Nani anaheshimika hapa duniani, Nani anajulikana?

Yesu Kristo keshakula Sana pesa za kina Maria Magdalena. Haya wewe na Yesu Nani anaheshima kwenye huu ulimwengu. Nani mashuhuri. Nani kaibadilisha Dunia.

Daudi Kala pesa ya Abigail. Haya wewe na Mfalme Daudi Nani anaheshimika, Nani mashuhuri!

Kama unatoka Familia Masikini basi kaa ukijua kuwa Bila kuwa na hekima katika kuchagua Mwanamke mzuri wa kuoa basi Future yako na future ya watoto wako iko mashakani.
Future ya watoto wako ipo mikononi mwa Mkeo.

Kuna watu hawawezi kunielewa, na sipo Kwa ajili Yao.

Usione watu ni wajinga kuoa wanawake kutoka makabila yenye kuchakarika, wanasababu zao. Moja ya sababu ni suala la malezi ya watoto.

Unaoa makabila au watu ambao wavivu wavivu kazi kuwaza vitu vya kipuuzi puuzi, unafikiri utafika wapi.
Jamii zote zenye wanawake wachapakazi Duniani ndizo zilizoendelea.

Ukitoka katika familia Masikini kaa ukijua maisha yako hayatakuwa rahisi, kuna kupanda na kushuka, na kupata na kukosa. Kuna kushinda na kushindwa.

Lazima uwe na Mwanamke atakayekupa backup. Usiogope changamoto za hawa wanawake ati ooh! Sijui wajeuri, ooh! Sijui akitoa pesa anakuwa na sauti.

Hakuna mwanamke mwenye sauti Kwa mwanaume anayempenda, hakuna na hajawahi kutokea.

Kwanza akupende, pili fanya wajibu wako kama Mwanaume, wanawake sio kwamba hawajui au hawaoni, wanamacho ya kuona kuwa Mumewe anahangaika sema ni vile labda ni Fungu la kukosa.

Weka akilini, Wanawake wanamacho Kwa wanaume wanaowapenda na kuwafikisha kileleni.

Kama Mwanamke hakupendi hawezi ona unachokifanya. Hata uvuje jasho vipi, hata uipiganie familia yako kiaje au umpiganie yeye lakini kamwe Mwanamke hawezi kuona ufanyacho Kama hakupendi. Mwanamke huona vile hisia zake zinavyoona. Hilo weka akilini.

Mwanamke Mchapakazi mwenye pesa madafu lazima watoto wako waende shule, yaani piga ya garagaza. Hiyo ni must. Atauza mitumba, genge, au kufanya biashara hata ya kutembeza ilimradi kuitunza familia yake.

Usikubali kuoa mwanamke MASIKINI, Hilo kila mara Taikon analisemaga,

Yaani mwanamke kama mdoli asiyejishughulisha. Usikubali.

Pesa ya mwanamke asiyejishughulisha hailiwi! Sijui umenielewa.

Na Kama pia haujishughulishi kamwe usile pesa ya mwanamke labda uwe mgonjwa.

Wanaume wa jamii ya Taikon, tunaoa wanawake wenye maarifa, na wenye kiu ya maendeleo. Kama hawana biashara au kazi tunawasaidia kupata kazi au tunawapa mitaji ya kufungua biashara ili baadaye tuonje Raha ya kuwa na Mke.

Raha ya Mke siku moja akununulie Suti au kiatu kikali, raha ya mke akitoa shopping anakuja anakuletea zawadi za hapa na pale. Raha ya Mke awe na uchumi bhana😀.

Wanaume wasiojiamini ndio wanaogopa wanawake wenye pesa au uwezo wa kiuchumi. Wanaume wasiojiamini ndio wanaogopa Kula pesa za Wake zao. Ni kutojiamini tu!

Sasa wewe utajiamini zaidi ya Muhammad au Yesu? Au Daudi 😂😂. Hizo njemba tunazungumzia Icon za Dunia.

Zingatia, mwanaume lazima uwe mjanja, uwe na Akili Sana ili uweze kumfurahia na kumfurahisha Mkeo.
Ni kweli kuwa na Mwanamke mmoja kwetu wanaume ni kipengele. Na wake wote Duniani wanalijua Hilo, ingawaje hawataki kuwa Mke mwenza lakini hawajakuzuia kuwa na wanawake wengine bila ya yeye kujua😀.

Sijasema umtegemee Mwanamke wala sijasema Mwanamke amtegemee Mwanaume. Yeyote anatemtegemea mwenzake hafai kuwa kwenye mahusiano ya ndoa.

Ninachosema kusiwe na Ubinafsi. Usione shida Kula pesa ya Mkeo kwani pia niyako. Pia mke asione shida Kula pesa ya Mumewe kwani pia ni yake.

Mfundishe mkeo kujitegemea hata bila ya uwepo wako. Kutokana na kuwa jamii zetu zilimuandaa mwanamke kumtegemea Mumewe Jambo ambalo sio zuri Kwenye ndoa.

Kumtegemea Mtu ni kumfanya kuwa Mungu mtu.

Ndio maana Taikon yeye kitu chakwanza kwenye mahusiano ni Upendo, kisha uaminifu, alafu mwisho Uhuru.
Uhuru ndio kujitegemea kwenyewe.

Usiogope kuachwa 😂😂 ooh! Nikimpa mtaji ataniacha Kama mnawatoto usiogope kuachwa. Kuachana ni lazima iwe mkiwa hai au siku mmoja wenu akifa😀.

Taikon ni mtu wa mfumo Dume ambao siku zote ndio unaotawala Dunia. Muandae Mkeo kujitegemea na kuitunza familia bila uwepo wako. Au ukiwa unaumwa au katika Hali mbaya.

Kama hujanielewa utanielewa ukishakuwa mtu mzima. Baadhi watachelewa kunielewa ikiwa ni Too late.

Unapoambiwa nyuma ya mafanikio ya wanaume wengi kuna Mwanamke elewa kuwa Pesa ya Mwanamke inaliwa, jasho la mwanamke linaliwa. Na wala sio kosa.

Waliofanikiwa wengi katika Nyanja nyingi tunalielewa Jambo Hilo.

Pia zingatia kuwa kila Mwanaume aliyeanguka nyuma yake yupo Mwanamke.

Usikubali kuwa na Mwanamke nyongaji, mdoli, asiye na msaada.

Yaani umsaidie yeye tuu! Kumbuka falsafa ya wanawake wote Duniani ni kuwa kwako atapata nini.

Kama hujanielewa shauri yako!

Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
nilimkopa wife laki sita, na Sina dalili za kulipa, na juzi kakuta sms ya mchepuko kwenye simu yangu, aisee kanipiga mkwara nisipompa hela yake lazima avute pumbu zangu,

huyu mshenzi alivyo kauzu Sina jinsi lazima nimlipe mama'e
 
nilimkopa wife laki sita, na Sina dalili za kulipa, na juzi kakuta sms ya mchepuko kwenye simu yangu, aisee kanipiga mkwara nisipompa hela yake lazima avute pumbu zangu,

huyu mshenzi alivyo kauzu Sina jinsi lazima nimlipe mama'e

😀😀

Usimtese Mkeo.
Usizini
 
Tatizo lako wewe unaejiita taikon wa fasihi huwa unaandika uzi mreeefu.

Na bahati mbaya zaidi nadhani huwa hauhakiki uzi wako kimaudhui kabla ya kuupost.
Ama lah huwa una mambo mengi kichwani ukiwa unaandika uzi wako.

Kwasababu kwenye huu uzi wako upo kuwili kuwili mara ukatae hiki lakini ukiendelea mbele umejitetea kwa kukikubali kwa maneno mengine.

Uzi una maneno meengi yanayojirudia kimaana.

Kama wewe ni mwandishi kweli basi punguza maneno meengi yenye maana moja.
 
Tatizo lako wewe unaejiita taikon wa fasihi huwa unaandika uzi mreeefu.

Na bahati mbaya zaidi nadhani huwa hauhakiki uzi wako kimaudhui kabla ya kuupost.
Ama lah huwa una mambo mengi kichwani ukiwa unaandika uzi wako.

Kwasababu kwenye huu uzi wako upo kuwili kuwili mara ukatae hiki lakini ukiendelea mbele umejitetea kwa kukikubali kwa maneno mengine.

Uzi una maneno meengi yanayojirudia kimaana.

Kama wewe ni mwandishi kweli basi punguza maneno meengi yenye maana moja.

😂😂😂

Mimi ni Wale wahubiri tunahubiri mpaka waumini wanalala.
 
Weka akilini, Wanawake wanamacho Kwa wanaume wanaowapenda na kuwafikisha kileleni.
Hapa ndo mnapokosea mpaka kusimamia visigino kumbe mwanamke hana hisia na wewe.

Kama ulivyosema wanawake kwenye mahusiano hufikiri kwa hisia na sio akili kama wanaume kama Vishu Mtata hufikiri. Hivyo basi haijalishi perfomance yako, kumkamata mwanamke kwanza kabisa ni maneno na si vitendo.

Pili vitendo vikishabihiana na maneno yako ya awali kwa angharabu 60%.

Tatu ndio kitandani sasa.
Hapo hata kama ni kimoko chali unarudi palee juu kwenye maneno anatengenezeka .....
Usikubali kuoa mwanamke MASIKINI, Hilo kila mara Taikon analisemaga,
Usikubali kuoa mwanamke mvivu.
Anaweza kua masikini lakini ukamtumia kupata pesa.
Kusema usioe mwanamke maskini huko ni kutaka kamseleleko na hiyo sio sifa ya mwanaume.

Kuna jamaa kaoa mwanamke kwao ni kweli wana pesa mno lakini ni mvivu wa kutupwa, hafanyi kazi yoyote. Anazidi kutipwilika na kunenepeana tu. Sasa hata ule muonekano uliompendea unapotea kwa kupenda mwanamke asie maskini.

Akili kumkichwa ROBERT HERIEL
 
Back
Top Bottom