Peter Madeleka: Kutishia watu kuwapeleka Magereza ili wateseke ni Ushamba na ulimbukeni. Kuuza bandari za Watanganyika ni ufisadi

Hii ni tafsiri yako ila si ya mkataba IGa
 
Hii ni tafsiri yako ila si ya mkataba IGa
IGA imepotoshwa mpaka tumeshindwa kuitazama kwa akili za kawaida tu. Ingekuwa na nguvu sawa na inavyotamkwa hizi barua za TPA zinazoongelea tender za uendeshaji wa bandari zisingeweza kutolewa.

Unapoona zabuni inatangazwa maana yake yule mwingine aliyepatikana hana mamlaka juu ya huyo anayetafutwa.
 
Lete hio IGA ya ukweli maana ilivuja si ya kweli....
Pili asojua serikali yetu janja jinga ni nani??
 
IGA iliyovuja ni ya kweli na aliyevujisha sasa hivi yupo lupango.

Kwamba serikali yetu ni janja janja ni hisia tu za kitanzania.
Ni hisia zilizokua proven acha kutetea ujinga watanzania tushavuka huko...

Kuhusu iyo IGA nikuletee hukumu yake kutoka mahakama kuu mbeya usome kwakutulia ili uelewe au unajua unajizima data mzee??
 
Nashauri waongeze magereza na wayaboreshe maana kesho wataingia wao
 
Naona mama ameamua kuwa kama Magufuli.
Ni mwendo wa kuwashughulikia wote wanaokosoa utendaji wa Serikali yake.

Ameamua kuvaa rasmi viatu vya mwendazake
Mbona mnamdhalilisha Magufuli namna hii? Yaani kweli Magufuli angwachekea hawa akina Mwabukusi, Mdude, Lissu na Slaa?

Au ulitaka kumaanisha nini ndugu Mzee Kigogo
 
Ni hisia zilizokua proven acha kutetea ujinga watanzania tushavuka huko...

Kuhusu iyo IGA nikuletee hukumu yake kutoka mahakama kuu mbeya usome kwakutulia ili uelewe au unajua unajizima data mzee??
Hukumu ya kurasa tisini na saba imeonyesha kuwa Mwabukusi na wenzake hawajui sheria za kimataifa, ni aibu ya kitaifa ile.

Nakuhakikishia suala zima la DP World lina faida sana haswa kwa wafanyabiashara wakubwa wanaotumia bandari yetu sisi tunaopinga wengi wetu ni wanaharakati tu, wadandiaji wa mada mbalimbali bila ya kuwa na uelewa wa kina wa nini kinachofanyika.
 
Ndicho ulichoelewa katika kurasa hizo zote ennhh?? Basi mi sibishani na tahira smart ngoja ninyamaze
 
Mbona mnamdhalilisha Magufuli namna hii? Yaani kweli Magufuli angwachekea hawa akina Mwabukusi, Mdude, Lissu na Slaa?

Au ulitaka kumaanisha nini ndugu Mzee Kigogo
JPM angeshawapoteza kitambo hao wanaharakati wasio na uelewa wa masuala mengi ya sheria za kimataifa na masuala ya bandari.

JPM alimnyamazisha Father Kitima asingeshindwa kuhakikisha DP World wanaingia mkataba mapema.

Father Kitima jumapili anasalisha misa makanisani na siku zinazobakia anakuwa meneja wa kampeni za urais za Tundu Lissu!, analiingiza kanisa zima kwenye siasa zake za kibinafsi za kumpinga mwekezaji kwa kuandika waraka kabisa.

Leo hii tender nyingi tu zinatangazwa na TPA, ni aibu kubwa sana kwa wote walioandika ule waraka bila ya kujua kwa kina mipango ya serikali ni ipi!. Katengeneza ufa kati ya TEC na serikali kwa ubinafsi tu wa kibinadamu.

Yule mchungaji mwenye sifa ya kulewa sana konyagi alipoongea alionekana ni mlevi tu anayepayuka, kumbe alikuwa na hoja za kina na za halali kuhusu upotoshaji wa ule waraka.
 
You too?
 
Umeusoma mkataba wa IGA kweli wewe?

Au unaandika tu kwa kutumia fikra na hisia zako badala facts zilizo mezani?

Kama hawa mafisadi wenzako wanafukuza ndugu zao wamasai toka Ngorongoro au Loliondo ili ardhi ya hifadhi ya maeneo hayo wapewe wageni toka mataifa mengine iwe ni kwa kupangisha, kuwekeza au kukodisha au kuwapa bure tu, unadhani wanashindwa nini kugawa bure bandari zetu za Tanganyika?

Na the fact na kwa mujibu wa mkataba ule wa IGA, ni kuwa bandari zote za baharini na maziwa yetu ya Tanganyika, mwaarabu amepewa bure huku watawala hawa wajinga wa CCM wakidhani kuwa kuna mikataba mingine iitwayo HGA ndiyo itakayokuwa na manufaa kwa Tanganyika!!

Hizi ni fikra za kijinga na kipumbavu sana..!

By the way, ni kwanini nyie watawala hamjifunzi kwenye mikataba mingine ya madini, gesi, mafuta na mingine mingi mliyoingia huko nyuma na ambayo kama nchi tulipigwa na sasa tunalipia gharama kubwa kuliko maelezo?

Kama nyie hamjifunzi basi, sisi wananchi na wenye nchi tumeshaliona hilo na tumejifunza ktk namna ngumu sana na kwa hiyo, tutawapinga mpaka mwisho mtoweke na mpotee kabisa..!!
 
JPM angeshawapoteza kitambo hao wanaharakati wasio na uelewa wa masuala mengi ya sheria za kimataifa na masuala ya bandari.
Cha ajabu akapotea yeye tena chini ya ardhi na kugeuka mavumbi ya udongo kama tu ambavyo hawa nao wanaindea njia hiyo hiyo..!!
JPM alimnyamazisha Father Kitima asingeshindwa kuhakikisha DP World wanaingia mkataba mapema.
Mjinga wewe. Kumbe unajiandikia tu ukiwa huna kumbukumbu juu ya mambo haya...

Ngoja tukukumbushe...

Ingawa Hayati Rais John P. Magufuli alikuwa katili na muuaji, Lakini kwenye kutetea mali na rasrimali za nchi yake kupitia mikataba mibovu na ya kijuha iliyoingiwa na kina Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete alikuwa vyema japo hakuwa anatumia njia sahihi wala kusikiliza ushauri wa "asiowapenda"..

Mbele ya hayati Rais Magufuli, hawa waarabu wa Dubai na kampuni yao ya DP World wasingejaribu hata kuleta ujinga na upumbavu wao huu.

Mathalani, Magufuli alipokalia kiti cha u - Rais mwaka 2015, alikuta Jakaya Mrisho Kikwete anataka kuingia mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na wa - China wenye thamani ya mabilioni ya dola na wenye maudhui kuwa wachina waijenge, waiendeshe na kuisimamia wao hiyo bandari kwa miaka 99...!

Hayati Rais Magufuli alisema, "...ni kichaa pekee anayeweza kukubaliana na mkataba wa namna hii...!". Hiyo ilikuwa bandari moja tu ya Bagamoyo.

Vipi huyu mama na nyie wenzake mlioingia mkataba usio na ukomo kabisa na usioonesha faida na malipo atakayotoa kwa nchi na waarabu wa Dubai kupitia kampuni yao ya DP World kuwapa bandari zote tena za upande mmoja tu wa muungano yaani Tanganyika?

Nyie na mama yenu Samia Suluhu Hassan mnadhani ni vichaa wa kiwango gani kwa mujibu wa mwanaCCM mwenzenu Hayati Rais John P. Magufuli..?

Bila shaka Rais Samia Suluhu Hassan na nyie mnaomshabikia na kumuunga mkono ni vichaa +++ wa kiwango cha barabara ya vumbi.
.!
 
Aliyeshiriki kuuandika mkataba kifungu kwa kifungu ndiye aliyenifafanulia kila kitu kilichomo mle.

Hiyo IGA haina nguvu yoyote ya maana kisheria, vinginevyo hizi barua za TPA za kutangaza tender za uendeshaji zisingesambazwa kila mahali. Mwarabu kapewa magati namba tatu mpaka namba saba ambayo ni asilimia nane tu ya eneo zima la bandari la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Fikra za kipumbavu ni zetu sisi tunaoshindwa kuuelewa vyema mkataba unamaanisha nini, hili ni tatizo letu la kulea ujinga hapa Tanzania, kila mtu anajiona anao uhuru wa kujadili kila kitu hata kile ambacho hana kabisa uelewa wake.

Elimu yetu ni tatizo kubwa, kila mtu anachanganyikiwa na maisha na haoni suluhisho mbeleni.

IGA mipaka yake ni eneo dogo sana, usitishwe wala kudanganywa na maandishi ya vifungu vya mkataba.
 
Mkataba wa IGA ungekuwa unatubana zisingesambazwa hizi barua za TPA zenye kualika makampuni yenye uwezo wa kuwekeza yaje yawekeze.

Umeandika maneno mengi lakini ni pumba tupu. Bandari zote zinahitaji waendeshaji mahiri na watapatikana kulingana na uwezo wao, Siasa za JPM eti alipinga uwekezaji, ni kwa sababu aliingizwa chaka na Kipilimba aliyekuwa boss wa TISS wa wakati ule na alipokuja kugundua kosa lake akamtimua mara moja.

Ukiwa na akili za kijamaa zisizokuwa na uwezo wa kubadilika ndio utakuja na hoja nyingi za kusema sisi wenyewe tuendeshe bandari zetu!, hatuna uwezo huo mkuu.

Teknolojia pekee ni mtihani kwa uendeshaji wetu. Achilia mbali tabia za wizi na ufisadi ambao kila mwaka CAG anauweka wazi.
 
Magufuli asingewafanya chochote zaidi wangekuwa rafiki zake, Magufuli asingekubali mkataba unaomlazimisha kukitokea mgogoro na mwekezaji mahakama zetu hazihusiki, na huku yeye ndiye aliyekuwa nyuma ya sheria ya raslimali 2017 kutungwa.
 
Magufuli asingewafanya chochote zaidi wangekuwa rafiki zake, Magufuli asingekubali mkataba unaomlazimisha kukitokea mgogoro na mwekezaji mahakama zetu hazihusiki, na huku yeye ndiye aliyekuwa nyuma ya sheria ya raslimali 2017 kutungwa.
Magufuli aliingizwa choo cha kike na washauri wake, na kwa kuwa alijenga SGR kwa pesa nyingi asingekuwa na jeuri ya kukataa mkataba unaoleta mteja mpya anayekwenda kuitumia reli hiyo mwaka mzima.

Bandari sio rasilimali ya taifa, ukiondoa yale maji pale bandarini hakuna chochote chenye sifa ya kuitwa rasilimali.

Meli ya MSC inayoleta makontena ya magari au nguo huwezi kuiweka kwenye kundi la rasilimali za nchi.

Ile mitambo ya kupakua na kupakia mizigo huwezi kuiweka kwenye kundi la rasilimali za nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…