Peter Madeleka: Kutishia watu kuwapeleka Magereza ili wateseke ni Ushamba na ulimbukeni. Kuuza bandari za Watanganyika ni ufisadi

Proof ya Nini, mbona watu walisema patrobas ni double agent mapema kabisa ila baadae ikawa dhahihiri. Ni muhimu sana chama kujiweka mbali na Hawa moles kutoka TISS hata huyo Mwabukusi wafanye naye kazi ila akiwa huko huko NCCR sio tena aingizwe CHADEMA.

Nimeona hata kina Mwamakula sijui Askofu Maxmillian yaani watu sketchy sketchy wanakaribishwa Hadi jikoni. Lazima chama ki separate mambo ya jamii na harakati za chama. Ni ajabu sana Lissu anaenda ngorongoro alafu anasindikizwa na watu ambao sio wanachama!!

This should stop otherwise tutakuja malizwa kizembe.
Kwa hiyo vibaraka wenzako woote wa CCM unawajua akina Katambi na wenzake
 
Wewe nawe ulienda shule kweli ? Hakuna anayekataa ubinafishaji wa Bandari, kinacholeta ukakasi ni maudhui ya mkataba wenywe.
Tatizo sio mkataba ni uelewa wa kilichoandikwa. Ule mkataba wa IGA ambao una mawanda mapana ya kibiashara.

Hayo mawanda ndio yanayotayarishiwa mikataba ya kibiashara na humo ndimo watanzania tujimwage kwa kina katika kutetea maslahi yetu kibiashara.

Anayelalamikia mkataba kuwa ni wa kinyonyaji hana uelewa wa nini haswa kinakwenda kufanyika.
 
Wakili huyu kwanini anaandamwa sana na serikali hii? Ana siri gani anazozijua wakihofu kuendelea kuzilipua hadharani hadi wakeshe wakifikiria namna ya kumrejesha gerezani? Kwanini wananchi wasiamini serikali hii imejaa uonevu kwa kutumia kichaka cha demokrasia ambayo ni garasha tupu?

Serikali acheni kumtesa wakili huyu kutokana na madhaifu yenu na watu wenu
Huyu wakili ni kati ya mawakili wenye akili sana na bora Tanzania inejaliwa kuwa Naye ndio maana anaandamwa
 
Kwa mujibu wa RIPOTI ya CAG ya mwaka 2020/2021, ni kwamba, MAGEREZA yote Tanzania, YAKIJAA, yanauwezo wa KUBEBA watu 35,000 tu. Uwanja wa MKAPA-DSM, UKIJAA, unaweza KUBEBA watu 60,000. Tanzania ina watu 60 MILIONI. Kwa hiyo, KUTISHIA watu MAGEREZA, ni USHAMBA na ULIMBUKENI.

View attachment 2748697
Tuna rais wa ajaby
Rais anapaswa kusimamia maslahi ya umma na si maslahi ya kikundi kidogo cha watu.

Hakuna mahala ambapo nimeona rais huyu yupo kwa ajili yetu
 
Kwa mujibu wa RIPOTI ya CAG ya mwaka 2020/2021, ni kwamba, MAGEREZA yote Tanzania, YAKIJAA, yanauwezo wa KUBEBA watu 35,000 tu. Uwanja wa MKAPA-DSM, UKIJAA, unaweza KUBEBA watu 60,000. Tanzania ina watu 60 MILIONI. Kwa hiyo, KUTISHIA watu MAGEREZA, ni USHAMBA na ULIMBUKENI.

View attachment 2748697
Basi ungeendelea kubaki huko Ili kudhinirisha ushamba wao! Pumbavu!
 
Hakuna anayeweza kuuza bandari ni uelewa wetu kuwa mdogo na kuwasikiliza sana wanaharakati wenye kupotosha jamii wakiwa na malengo maalum.

Bandari inakodishwa, hii ya Dar inakwenda kuwa na wapangaji wawili DPW na mwingine wa magati namba nane mpaka namba kumi na moja.

Ile ya Tanga inakwenda kuwa na mwendeshaji mmoja, ile ya Bagamoyo inakwenda kuwa na mwendeshaji mwingine.

Haya ni masuala ya kiuchumi yenye kuhitaji mtu kuyatazama kiuchumi, mtu tu layman mwenye uelewa mdogo wa masuala nyeti hawezi kuelewa nini haswa kinachotafutwa.

Tunatoka katika mfumo wa mmiliki wa bandari kuendelea kumiliki yeye kama yeye tunaingia katika mfumo wa Land lord Port ambao mwendeshaji mkuu TPA anakuwa na wapangaji wengine ili kuongeza ufanisi na kurahisisha mzigo mwingi sana uliopo ndani ya Tanzania na nchi zinazotuzunguka kuweza kuyafikia mataifa ya nje haraka.

Kuna tani zaidi ya milioni 30 za mizigo mbalimbali inayotakiwa itoke huko bara na kwenda nje ya nchi, huo ni mzigo mwingi sana na kwa aina ya uendeshaji wa kizamani wa bandari tulionao hakuna nafasi ya kitaifa kuweza kuinuka kiuchumi.

Haya ni masuala ya kiuchumi yenye kutaka ufafanuzi wa kina wa kiuchumi, huu sio wakati wa kufikiria kizamani halafu matokeo ya ufikiriaji huo yawe na mashiko kwenye maisha ya kisasa.
Kuendesha wenyewe sio suala la kiuchumi
 
Tatizo sio mkataba ni uelewa wa kilichoandikwa. Ule mkataba wa IGA ambao una mawanda mapana ya kibiashara.

Hayo mawanda ndio yanayotayarishiwa mikataba ya kibiashara na humo ndimo watanzania tujimwage kwa kina katika kutetea maslahi yetu kibiashara.

Anayelalamikia mkataba kuwa ni wa kinyonyaji hana uelewa wa nini haswa kinakwenda kufanyika.
Wewe ndio hijui. Kama unajua basi wewe ni chawa
 
Kuendesha wenyewe sio suala la kiuchumi
Sisi wenyewe ndio tunapata hati chafu kila CAG anapofanya ukaguzi pale TPA. Mawazo ya kijamaa hayana msaada katika uendeshaji wa bandari kisasa.

Kuna masuala mengi ambayo sisi hatuna uwezo wa kuyakabili katika uendeshaji wa bandari. DP World anamiliki meli 400 maana yake baadhi yake anaweza kuzitenga kwa ajili ya kuhudumia bandari yetu peke yake.

Kuna masuala ya kuharibika vifaa vya kazi pale bandarini na uwezo wa mwendeshaji wa kuhakikisha vinafanya kazi haraka ili uendeshaji usikwamishwe.
 
Basi tutawaliwe , maana inaonyesha hatuna uwezo wa kujiongoza
 
India tunapokwenda kutibiwa matatizo ya moyo kila mara wameingia mkataba na DP World.

Na wao wanayo haki ya kusema watawaliwe kisa hawana uwezo wa kujiongoza?. Haya ni mawazo ya kijamaa na yanatupotezea sana ule uwezo wa kuitazama dunia halisi tunayoishi.
 
Hakuna anayeweza kuuza bandari ni uelewa wetu kuwa mdogo na kuwasikiliza sana wanaharakati wenye kupotosha jamii wakiwa na malengo maalum.

Bandari inakodishwa, hii ya Dar inakwenda kuwa na wapangaji wawili DPW na mwingine wa magati namba nane mpaka namba kumi na moja.

Ile ya Tanga inakwenda kuwa na mwendeshaji mmoja, ile ya Bagamoyo inakwenda kuwa na mwendeshaji mwingine.

Haya ni masuala ya kiuchumi yenye kuhitaji mtu kuyatazama kiuchumi, mtu tu layman mwenye uelewa mdogo wa masuala nyeti hawezi kuelewa nini haswa kinachotafutwa.

Tunatoka katika mfumo wa mmiliki wa bandari kuendelea kumiliki yeye kama yeye tunaingia katika mfumo wa Land lord Port ambao mwendeshaji mkuu TPA anakuwa na wapangaji wengine ili kuongeza ufanisi na kurahisisha mzigo mwingi sana uliopo ndani ya Tanzania na nchi zinazotuzunguka kuweza kuyafikia mataifa ya nje haraka.

Kuna tani zaidi ya milioni 30 za mizigo mbalimbali inayotakiwa itoke huko bara na kwenda nje ya nchi, huo ni mzigo mwingi sana na kwa aina ya uendeshaji wa kizamani wa bandari tulionao hakuna nafasi ya kitaifa kuweza kuinuka kiuchumi.

Haya ni masuala ya kiuchumi yenye kutaka ufafanuzi wa kina wa kiuchumi, huu sio wakati wa kufikiria kizamani halafu matokeo ya ufikiriaji huo yawe na mashiko kwenye maisha ya kisasa.

Vichwa ngumu hawaelewi wao kila wakiambiwa kitu na wapinzani wanakubali..
 
India tunapokwenda kutibiwa matatizo ya moyo kila mara wameingia mkataba na DP World.

Na wao wanayo haki ya kusema watawaliwe kisa hawana uwezo wa kujiongoza?. Haya ni mawazo ya kijamaa na yanatupotezea sana ule uwezo wa kuitazama dunia halisi tunayoishi.
Uthibitisho WA mkataba WA India na DP weldi unaweza kutuonyesha au upo kwenye ndoto zako
 
Acheni uongo? Kama kasingiziwa kwanini sikusikia hao waliotekeleza uhalifu wamekamatwa?? Yaani mtu amuue mwanao alafu asingizie baba yake ndio umemuua then na wewe ukae kimya tu kisa "umesingiziwa"? Si lazima utatafuta aliyefanya hicho kitendo Ili ujisafishe!!

Ukikaa kimya means umekubaliana na shutuma so huwezi kwepa lawama.
Usitake kuhalalisha uhalifu wako hapa kama ilivyo desturi yenu
 
Uthibitisho WA mkataba WA India na DP weldi unaweza kutuonyesha au upo kwenye ndoto zako
Cha muhimu ni kampuni hiyo hiyo tunayoikataa ndio wameikubali huko India. Ni kampuni hiyo hiyo tunayoiletea mizengwe ndio imekubaliwa huko UK na Belgium.

Uandishi wa mikataba ni shule kamili, sio kila mtu anayedhani anayafahamu masuala ya mikataba anao uelewa wa kipi kinachoandikwa kwenye mikataba.

Tanzania tunacheza mno na masuala ya elimu, na huu mkwamo wa kimaendeleo sababu mojawapo ni hiyo.
 
Kwa hiyo mkataba wetu Una mapungufu na sio hiyo kampuni
 
Usitake kuhalalisha uhalifu wako hapa kama ilivyo desturi yenu
Nani kahalalisha huo ndio ukweli? Unadhani mtu binafsi anaweza ondoa CCTV camera au anaweza order walinzi wa compound wasiwepo siku hiyo? Lissu pia aliwahi ripoti Nissan Patrol inamfuatilia ila hakuna hatua ilichukuliwa alafu mkiambiwa mmeshiriki mnakua wakali.
 
Back
Top Bottom