Peter Msigwa: Baada ya mauaji ya Oktoba 29 na ukiukwaji wa haki unaoendelea, siwezi tena kubaki CCM, nimeamua kurejea CHADEMA

Huyu ni mnafiki. Nawashauri wasimpokee
Ujio wa peter msigwa umekuathiri vipi wewe kama mwanachama? Ameondoa wanachama? Amevunja chama? Au tatizo ni hisia binafsi?

Kama mtu ana uwezo wa kuongeza ushawishi, kuongeza nguvu kwenye kampeni zinazoendelea, connection, mali na kuisaidia CHADEMA kufika kwa wananchi wengi zaidi, shida iko wapi?

Peter Msigwa siyo mwanachama wa kawaida kisiasa. Anaweza akatusaidia mambo mengi ya kimkati yaliyofanyika kabla na baada ya uchaguzi, ameshaijua system ya CCM, ameshajua propaganda zao, mbinu zao za kisiasa na namna wanavyocheza game ya ushawishi. Hayo mambo hayaonekani kwenye Facebook au Twitter lakini ndani ya siasa ni silaha kubwa sana

Kama kweli lengo ni kukijenga chama na kushindana kisiasa basi tunatakiwa kuangalia mtu ana value gani kwenye mapambano ya sasa tusiwe na visasi na emotions kwa wakati kama huu na tukianza kubeza kila aliyewahi kukosea hatutapata tunachotaka kukisikia kutoka kwake
 
Msigwa anapaswa kudeki ofisi za CDM kanda zote kabla ya kufikiriwa kupokelewa kwenye chama hiki kitukufu.
 
Chadema hamjawahi kujitambua kwa makosa yenu, miaka ijayo samia atahamia chadema na mtaanza kumsifia vile vile
Nikiondoa maneno sita ya mwanzo kwenye mstari huo; sitashangaa sana kwa baadhi ya watetezi wa hawa malaya wa kisiasa wakipiga kelele Samia ajiunge ndani ya CHADEMA.
Na utashangaa sana watakavyokuja na sababu za ajabu sana za kushawishi Samia akubaliwe CHADEMA.
 
N
Kama walivyofanya kwa lowassa πŸ˜‚
 
N

Kama walivyofanya kwa lowassa πŸ˜‚
Mkuu 'Mbaga', sijui kama umebadilika kiasi hiki kwa kadri ninavyokumbuka historia ya humu JF.

Lakini ngoja nijiseme mwenyewe hapa, kama hukumbuki.

Ujio wa Lowasa CHADEMA wakati ule, binafsi niliuona tofauti kidogo na huu umalaya tunaouona umezagaa sana ndani ya siasa za nchi hii.

Binafsi niliunga mkono ujio huo; pamoja na kwamba sikujuwa ulianzia wapi.

Lengo lilikuwa matumaini ya kuiondoa CCM madarakani; na Lowassa alikuwa na mategemeo makubwa ya kufanya hivyo wakati ule.

Ni hivi kama bado huelewi: Yeyote ambaye angeweza kuwa na uwezo wa kuiondoa CCM madarakani ningemuunga mkono; hata hii leo, wewe ukisimama na kusema utaiondoa CCM madarakani, nitakuunga mkono, hata kama sijui unakwenda kufanya nini ukiwa huko kwenye madaraka.

Kwa hiyo, swala la ujio wa Lowassa ni tofauti sanba na hawa wafanya biashara mbovu; akina Msigwa.
 
Ukiona Mtu anaweza kumsaliti mzazi wake na kuja kwako rafiki yake, usidhani atashindwa kukusaliti ww rafiki.

Sasa chadema wakadanganyika na maneno matamu ya lowassa kuwa wataiondoa ccm

Ndo alichofanya lowassa.
 
Kwa mara ya kwanza, nimekusoma ukiwa umeandika kwa utulivu, na unastahili kujibiwa kwa utulivu vilevile.
Naheshimu sana mijadala ya aina hii.

Msigwa kaonyesha wazi kuwa hana msimamo. Hili ndilo jambo muhimu kabisa kwa mwanasiasa yeyote anayetaka kuheshimika.

Ni kitu gani kilichomwondoa CHADEMA?

Alipoondoka CHADEMA alikwenda wapi; na alifanya nini?

Ujio wa Msigwa unawahusu wanachama wooote wa CHADEMA waliobaki na kupata mateso chini ya marafiki zake wapya alioungana nao huko CCM, au hili hulijui?

Je, angefanikiwa juhudi zake za kuwasaidia alioungana nao kuimaliza CHADEMA, wakati huu angerudi kwenye chama kipi?Peter Msigwa kwa historia yake hana ushawishi na nguvu za kuisaidia CHADEMA. Kama kuna watu wenye mwelekeo wa akili za Msigwa ambao anaoushawishi nao. hau hawafai kuwa sehemu ya CHADEMA.

"System ya CCM" siyo jambo jipya kwa Msigwa, kwamba ilihitaji ajiunge huko kuisoma na kuielewa. System hiyo hiyo imekuwepo miaka yote, na ni hiyo kila mara iliyotafuta njia za kuiua CHADEMA; wewe leo unakuja na 'spin' ya Msigwa kwenda kujifunza system ya CCM upya?

Chama kilichozana na sampuli ya kina Msigwa, "kuangalia mtu ana value gani kwenye mapambano..."?
Watu wasiokuwa na msimamo, 'commitment' juu ya wanayoyasimamia? Hao ni wafanya biashara mbovu tu ya kisiasa. Usitegemee lolote toka kwa watu wa aina hiyo.
 
Ukiona Mtu anaweza kumsaliti mzazi wake na kuja kwako rafiki yake, usidhani atashindwa kukusaliti ww rafiki.

Sasa chadema wakadanganyika na maneno matamu ya lowassa kuwa wataiondoa ccm

Ndo alichofanya lowassa.
Ninaelewa sana unachojaribu kueleza hapa.

Ujio wa Lowasssa ndani ya CHADEMA wakati ule ni tofauti kabisa na haya yanayojadiliwa hapa.

Wakati ule kulikuwepo na uwezekano mkubwa wa kuing'oa CCM madarakani. Hilo ndilo lilikuwa jambo muhimu kuliko mengine yote.
Lowassa alikuwa na matumaini ya kuwaondoa CCM kutokana na historia yake tokea nyuma.
Alifanyiwa mizengwe na hao unaowaita wazazi wake.
Kampeni aliyofanya ndiyo iliyomwangusha; vinginevyo hali ingekuwa ngumu huko CCM.
 
That is just human nature. Hakuna mtu ambaye hupoteza muda wake akimsifia ex-wife (ex-husband) wake au ex-girlfriend (ex-boyfriend) wake!
Our political dispensation has been reduced to such derogatory level?

Lord have mercy upon us!
 
Ingekuwa vipi kama mauaji ule umwagikaji damu ungekupatia cheo?
Angekuwa muungwana angejibu hili swali.

Au tuwaulize hawa wanaomshangilia kwa uamizi wake huu wa kijinga kabisa watusaidie kujibu swali lako.
 
Our political dispensation has been reduced to such derogatory level?

Lord have mercy upon us!
A search for angels in a sinners house is a futile exercise.

Kwa politicians, switching political parties ni kitu cha kawaida sana! Hata Lissu alijiunga CHADEMA akitokea NCCR Mageuzi.
 
Licha ya matusi yote yale aliyo kuwa ana warushia chadema + vicheko vya dharau na lawama kede kede Leo anarudi chadema

Maana hapo kwanza ncheke

Hawa wanasiasa wa tz walisha wapima raia wa Tanzania na kuwaona ni wajinga so wame amua kuwapeleka wanavyo taka kama ming'ombe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…