The ghost writer
JF-Expert Member
- Apr 5, 2023
- 967
- 1,971
Kama Kuna kitu hujawahi kukigundua kwa muda mrefu basi ni hii👉 "Namna picha ya profile yako inavyokuelezea wewe ni mtu wa aina gani ndani na nje ya mitandao ya kijamii."
Hata hapa jamiiforums kabla yakusoma hoja ya mtu, kabla hujaangalia mada zake, na hata kabla hujajua yuko upande gani wa mjadala... macho yanaanza kutua kwenye Profile Picture (PFP).
Ndani ya sekunde chache tu, ubongo unakuwa tayari umempa mtu "CV" yake.
"Huyu anaonekana ni tajiri..."
"Huyu lazima ni mbishi..."
"Huyu anaonekana ni mzee wa quotes..."
"Huyu bila shaka ni mchambuzi wa kila jambo..."
Cha kuchekesha zaidi ni kwamba mara nyingi tunajikuta tunamjengea mtu taswira nzima kwa picha moja tu—halafu akianza ku-comment, ndipo tunagundua tulikuwa tumekosea kabisa... au pengine tulikuwa sahihi. 😂
Sasa Leo tunakwenda kufafanya "diagnosis" ya aina maarufu za Profile Pictures zinazotumika sana mtandaoni, Jinsi zinavyoonekana, na zile dhana ambazo wengi wetu hujitengenezea kuzihusu.
Tuanze na hizi
The Sigma Male PFP.
PFP zenye picha za kina Patrick Bateman, Thomas Shelby, Ryan Gosling, valdmir Putin n.k.)
Inavyoonekana:
I simply don't care. Discipline is forever. I move in silence. I
Maisha yao Mtandaoni.
Anataka kuonekana kama mtu mgumu, mtulivu na asiyejali chochote. Lakini ukimjibu kwa emoji moja tu 😅, anaanza kufikiria kama ulimaanisha dharau ama kejeli.
Anapenda quotes (nukuu) za "focus on yourself" lakini muda mwingi yuko online akisoma comments zote za wengine tena bila kuruka hata moja.
Anataka kila mtu amuone kama mtu wa "cold mindset" na asiyejali chochote, lakini akiona mtu amenukuu comment yake bila kumtag, siku yake yote inabadilika. 😂
Anapenda kupost quotes (nukuu) za "Never chase, always attract." Halafu kila baada ya dakika tano anarudi kuangalia kama post yake imepata likes mpya. 😅
Akiingia kwenye mjadala, reply zake zinaanza na "Emotion pembeni..." lakini mwisho wa thread ndiye anayeandika paragraph ndefu zaidi.
Anaamini ukali unaanzia kwenye PFP. Akibadilisha picha, anahisi aura yake itapungua.
Maisha Yao halisi;
Mtandaoni wanaonekana majasiri, lakini live ni watu wapole wanaoweza kuogopa hata kumwambia muhudumu "oda yangu imekosewa." 😅
The historical figures PFP
Hawa Sasa ndio wanajionaga "Wazee wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa"! 😅
Watu wanaoweka picha za viongozi au watu maarufu wa kihistoria (kama vile Martin Luther king Jr, Thomas Sankara, Napoleon, Marcus Aurelius, au Julius Nyerere) wanajiona kama washauri wakuu wa sayari hii.
Maisha yao mitandaoni:
Wachambuzi wa Siasa za Dunia. Huwa hawatoi maoni kuhusu mambo ya kawaida kama udaku au muziki. Utawakuta chini ya posts za siasa, uchumi, au migogoro ya kimataifa wakichambua kana kwamba walikuwepo wakati mikataba inasainiwa.
Wanapenda kutumia maneno magumu ya kifalsafa au misemo ili kukuonesha kiwango chako cha shule ni kidogo.Wanamapinduzi wa Keyboard: Profile zao zinasema "Haki na Usawa," na huwa wanapinga kila mfumo uliopo sasa hivi duniani wakiwa wamerefusha miguu kitandani.
Taswira yao kwenye Maisha Halisi (The Reality Check):
Kwenye maisha ya kawaida, mara nyingi ni watu waliofanya vizuri darasani (wazee wa kukariri), lakini hawana ajira au wameajiriwa ila mshahara kiduchu mfano Mwalimu Mpwayungu village.
Ni watu wanaopenda kusoma vitu vingi sana mtandaoni (Wikipedia ndio maskani yao)😅
3.The Redpill PFP
Watu wanaoweka picha za mrengo wa Redpill (mara nyingi huwa ni picha ya mwanaume mwenye suti kali, saa Kali, miwani mikali. wanajiona kuyafahamu vyema mahusiano na mapenzi utadhani wamegundua siri zote za ulimwengu.
Maisha Yao ya mtandaoni;
Wanajionaga (The High-Value Alpha). Ni Maadui wa kubwa wa Mapenzi (Anti-Simp). Kazi yao kubwa ni kuonya wanaume wenzao mtandaoni wasihonge, wasiliye kwa ajili ya mwanamke, na wasionyeshe hisia zao.
Kila post yao inaanza na "Wanaume, amkeni..."Wachambuzi wa Uhusiano. Utasikia "Mwanamke akifikisha miaka 25 thamani yake inashuka" au "Onyesha dharau ili akupende.
Kwenye Maisha Halisi (The Reality Check);
Mtandaoni wanajifanya wababe wanaotawala wanawake, ila UHALISIA wanaishi kwenye nyumba za mama zao, mashameji au nyumba za dada zao na wanakaripiwa vikali wakichelewa kurudi nyumbani au wakisahau kuosha vyombo. 😂
Ni waoga Mbele ya wanawake wazuri wanapokutana nao live, wanakuwa wapole Ile "Alpha Male" yote inayeyuka, wanabaki na aibu.
Cha kusikitisha na kuchekesha, wengi wao waliingia kwenye mrengo huu baada ya kuachwa kwa kashfa (broken heart) na msichana fulani wa chuo. Hizo kelele zote mtandaoni ni donda ndugu linalouma!
4.The Motivational PFP
Hao sasa ndio "Manabii wa Mtandaoni"! 😅
Watu wanaoweka picha za maneno ya motisha (Motivational Quotes) "the hard work pay"
Maisha yao ya mtandaoni;
Ni matajiri wa Maneno mengi ya motisha ila kutake action sifuri. Watakutag kwenye picha ya Jeff Bezos au Elon Musk ikiwa na maneno kama: "Kama huna mpango wa kutengeneza pesa ukiwa umelala, utafanya kazi hadi ufe."
Kwenye Maisha Halisi (The Reality Check):
Hawa ndio wazee wa Mizinga ya Kimya Kimya. Licha ya quotes zote za utajiri, hawa ndio watu wanaoweza kukupigia simu ya ghafla: "Oya mwanangu, niazime buku tano hapa nimekwama, nitakurudishia jioni.
Kiuhalisia, mara nyingi wanakuwa wanapitia stress za maisha, kwahiyo zile quotes wanaziweka ili kujifariji wenyewe kwanza kabla ya wengine.
5. The Bakini PFP
Watu wanaoweka picha wakiwa kwenye mavazi ya kuogelea (Bakini/Bikini PFP) au nguo fupi za ufukweni huwa wanatega mitego yenye nguvu ya sumaku mtandaoni.
Huu hapa uchambuzi wao usio wa Siri Mtandaoni;
DM zao zimejaa mesezi kama "Mambo mrembo," "Uko vizuri," au "Nitumie namba yako." Wao kazi yao ni kuangalia nani mwenye "profile yenye pesa" ili wamjibu, masikini wengine wote wanaachwa kwenye Request.😅
Wapenda starehe na kila post yao inakuaminisha kwamba wanaishi maisha ya kifahari ya hoteli za nyota tano huko Zanzibar au Maldives, hata kama picha hiyo ilipigwa mwaka mmoja uliopita na bado wanaivuta hadi leo.
Kwenye Maisha Halisi:
Watafutaji wa attention (The attention seekers). Mtandaoni picha inaonekana ya kitajiri sana, lakini live ndio wale wanaoweza kukaa masaa matatu ufukweni wakinywa soda moja na maji ya chupa, huku wakigombana na mpiga picha kwa nini hajamtoa vizuri kiuno. 😂
Wakati mtandaoni wapo nusu uchi na wanajiamini, live huko mtaani kwao wanaweza kuwa wanavaa yale madira makubwa
6. The Car PFP
Hawa ndio wanajionaga "Madereva wa Mtandaoni"! 😅
Watu wanaoweka picha ya gari kali—iwe ni Ford, Range Rover, BMW ya kisasa, au gari la mashindano ya F1 wanajiona tayari wapo kwenye barabara kuu ya mafanikio.
Hali ya maisha yao mtandaoni;
Wanajifanya Wachambuzi wa Magari (Car Enthusiasts). Huwa wanajua kila kitu kuhusu injini, horsepower, na gharama za vifaa vya gari ambalo hawajawahi hata kushika usukani wake. 😅
Wanapenda ku-comment kwenye posts za picha za matajiri au wasanii wakisema, "Hivi karibuni nitamiliki hii chuma." Wanaishi maisha ya kwenye ndoto😅
Kwenye Maisha Halisi:
Mtandaoni picha ni Bugatti Chiron, lakini live ndio wale wanaoongoza kugombana na kondakta wa daladala kisa amewadhulumu chenji ya shilingi mia mbili. 😂
Ujuzi wao mkubwa wa kuendesha gari unaishia kwenye magemu ya simu (Asphalt) au PlayStation. Live hata leseni hawana.
Ni watu wenye ndoto kubwa sana maishani na wanaopenda maisha ya kifahari. Hiyo picha ya gari wanaiweka kama vision board ya kuwapa hamasa ya kupambana, hata kama kwa sasa mfuko wao unasoma "sifuri."
7.The celebrity Worshipper PFP
Hao sasa ndio "Marais wa Vyama vya Mashabiki" au "Wamiliki wa Mahaba ya Mtandaoni"!
Watu wanaoweka picha ya msanii au mtu maarufu (kama Diamond Platnumz, Alikiba, Cristiano Ronaldo, Messi, Beyoncé, au mastaa wa K-Pop) wanajiona kama mawakili rasmi waliolipwa kulinda majina ya masanamu yao.
Maisha Yao mtandaoni;
Huwa hawana maisha yao binafsi mtandaoni. Kazi yao ni moja tu: kulinda heshima ya staa wao. Ukimkosoa msanii wao hata kidogo, watakutusi tusi ambalo litakufanya ujutie kwanini ulinunua smartphone.
Wanajua takwimu zote za staa wao—views za YouTube, tuzo walizoshinda, idadi ya mabao, hadi jina la mbwa wa msanii huyo.
Wakiongea, wanapenda sana kutumia neno "Sisi." Utasikia: "Sisi jana tumetoa ngoma kali sana" au "Sisi tuna magoli mengi msimu huu." Utadhani walikuwa studio au uwanjani wakisaidia kutoa pasi.
Kwenye Maisha Halisi;
Mtandaoni wanapoteza bando la usiku kucha kubishana na kutukana watu kwa ajili ya mtu maarufu, lakini live huko mtaani staa huyo hata hajui Chochote kuhusu wao.
Hawapati hata senti tano ya mgao wa faida. Wakati mtandaoni wanatamba kuhusu utajiri wa msanii wao (magari, majumba, cheni za dhahabu), live wanaweza kuwa wanaishi chumba kimoja chenye feni inayopiga kelele kama cherehani chakavu.
8.The No PFP
Hawa Wanajulikana kama "Mizimu ya Mtandaoni"! 😅 Watu ambao hawana picha kabisa (ile picha ya kijivu ya default ya mfumo). Pengine ni watu wa kuogopwa sana mtandaoni.
Maisha yao mitandaoni;
Ni Watazamaji Tu (Silent Observers): Hawapost kitu, hawacomment mara kwa mara, wanajifanya wanajua siri za kila mtu. Siku wakiamua kucomment, hawana cha kupoteza! Wanaweza kuandika tusi au dharau ya karne kwa sababu wanajua huwezi kuwajua sura zao wala maisha yao.
Kwa upande mwingine ndizo akaunti maalumu zinazotumika kuchungulia maisha ya ma-ex wao, maadui zao, au watu maarufu. Ni akaunti ya kijasusi!

Ni watu Imara / Watu Makini, Live wanaweza kuwa ni watu wazito sana labda bosi fulani wa kampuni, mtu wa kitengo cha usalama, au mtu mwenye hela zake ambaye hataki kabisa usumbufu wa kidijitali.Wazee wa "Teknolojia Imeniacha"
Kwa upande mwingine wanaweza kuwa ni wale ambao hawajui kabisa jinsi ya kuweka picha! Unaweza kuta ni mjomba wako au shangazi ambaye alitengenezewa akaunti na mtoto wake, kwa kifupi ni wanaoanza kumiliki smartphone 😂
Muda mwingine wanaweza kuwa ni watu wenye Maisha ya Siri: Ni watu wanaopenda usiri wa hali ya juu. Hata ukikutana nao live, hawapendi kupigwa picha, au kurekodiwa.
Subiri Part 2😅