Unachokiita psychology ni bias zako tu, ukitaka kuona mtu ni mshamba utamuona tu hata kama aweke picha gani.
The faceless noodles
Hawa watu sijui ndio wanajionaga "Wajumbe wa FBI" au ?😅
Ni wale wanaoweka picha ya mwanaume aliyevaa koti la 'hoodie' lililofunika kichwa, sura haionekani (faceless) au kuna kivuli kikubwa mbele utadhani wadukuzi (hackers) wa mitandaoni au watu wenye maisha ya hatari sana.
Uhalisia wa maisha Yao mtandaoni.
Wanajifanya (The Mystery Man). Wenye Maneno ya mafumbo. Hawana stori za kawaida. Kila wakipost, wanaandika maneno mafupi ya siri au mafumbo kama: "Trust no one," au "Usinifuate."
Hawataki kabisa mtu ajue sura zao, umri wao, au wanakoishi. Ukijaribu kuwauliza maswali ya kawaida DM, wanakujibu kwa ukavu utadhani wanahojiwa na polisi.
Wanapenda kushea memes za watu wapweke (lonely text) au zile za "Sigma Male" wakijifanya wao hawahitaji marafiki duniani.
Kwenye Maisha Halisi (The Reality Check):
Mtandaoni picha inaonekana ya kijasusi na hatari, lakini live ndio wale watu wapole kupitiliza ambao wakikaa kwenye kikundi cha watu hawaongei neno, na mtu akiwatazama machoni wanainamisha kichwa haraka kwa aibu.
Sababu kubwa ya kuficha sura kwenye hoodie sio kwamba wao ni majasusi, bali labda wanaona sura zao hazina "vibe" la kitajiri, kwahiyo hoodie inakuwa kama kichujio (filter) cha bei rahisi.
Licha ya muonekano wao wa mtandaoni, live ni watoto wazuri kabisa wa mama zao, wanaotumwa kununua vitunguu gengeni na wanafua nguo zao wenyewe kila Jumamosi asubuhi huku wakisikiliza nyimbo za taarab au Bongo Flava.