Philip Mangula ang'atuka nafasi ya Umakamu Mwenyekiti CCM Taifa. Abdulrahman Kinana apendekezwa na Halmashauri Kuu kuchukua nafasi yake

CCM ya 2014 inarudi kwa kasi; muda mfupisana ujao zomea zomea dhidi ya rangi ya kijani mitaani itarudi pia kwa kasi.
 
Wapinzani sasa tujipange vzr,kama huyu mzee abdrahaman karudi tena
Kama unamaanisha tujipange kudai katiba mpya hapo sawa, lakin kama unamaanisha kujipanga kwa uchaguz hapo hamna kitu kama hicho mana bila katiba mpya itakuwa ni uchafuzi tu kama kawaida
 
Mambo ya kushughulikiana yapo tu kila awamu.
Kuna Raisi, Kuna chama halafu kuna JAMHURI. Ukitaka uwe mbali na kushughulikiwa, Vimbiana na woote ila katika kuvimba kwako uwe una uelewa wa kutofautisha matokeo ya kumvimbia Raisi, matokeo ya kukivimbia Chama na matokeo ya kuivimbia JAMHURI na maslahi yake. Kama unataka kuvimba nenda kwa wavimbaji Nunda kama kina Mbowe wakufundishe tofauti ya hayo majina matatu.
 
CCM ya 2014 inarudi kwa kasi; muda mfupisana ujao zomea zomea dhidi ya rangi ya kijani mitaani itarudi pia kwa kasi.
La ajabu itakuwa nini sasa hapo wakati, tofauti na miaka mitano iliyopita, wananchi sasa wapo huru kuonesha hisia zao alimrad hawavunji sheria!!!
 
Sasa hapa ndio watu wataona kuwa Jiwe aliharibu Nchi,Msoga gang watatumia njia alizotumia Magufuli kuwanyamazisha Wananchi-style hiyo hiyo watatumia kwa wale watakaosumbua utawala wa Samia.
 
Natuma salaam kwa ndugu Bashiru na team yake popote walipo.
Naomba wa burudike na wimbo wa TOT usemao, CCM ni ile ile, CCM ni ile ileeeeh.
 
Sasa Chadema huu ndo muda wenu wa kushine kama mtakuwa na akili. Nendeni kwa wananchi mjijenge. Maana ukweli sasa hii iliyopo ni serikali ya kufavor matajiri ambao ni minority hapa Tanzania.
Yani Mbowe afungwe tena ndani kutetea Wananchi wasiojielewa??
 
Sasa hapa ndio watu wataona kuwa Jiwe aliharibu Nchi,Msoga gang watatumia njia alizotumia Magufuli kuwanyamazisha Wananchi-style hiyo hiyo watatumia kwa wale watakaosumbua utawala wa Samia.
Kwamba wajanja wa mjini watumie njia za mshamba?
 
Dah! Shamba la BIBI

Hakuna wa kuwakemea, hakuna (consequence) uwajibikaji au kuwajibishwa kwa matendo yao sanasana ukiwa mpigaji, mwizi mkubwa utazawadiwa cheo serikalini na kulindwa na wenzao.

Ni zaidi ya shamba la bibi, huu mfumo unafanana zaidi na Mafia state, Few Dons, Godfathers, vigogo, Wahalifu wanaongoza nchi, wanafanya watakavyo wakilindwa na vyombo vya umma kwa maslahi yao na washirika wao, familia zao, mtandao wao. Mafioso wenzao.
 
Bibi wa Taifa😁😁😁
Your browser is not able to display this video.
Your browser is not able to display this video.
 
Magufuli amisha onyesha njia,ikifika kipindi cha Uchaguzi ni ubabe tu utatumika baada ya muda watu watatumia maisha yataendelea.hakuna tena cha kuhofia kuwa chama kitakufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…