Hukunipuuza, hilo huwezi ukaniongopea
Sawa,bali nilifanyaje ? Nilikimbia si ndiyo ? Sasa jambo ambalo ukiangalia tu hiyo translation uliyoiweka hayo maelezo unayakuta katika mlango wa aya zilizo futwa na zoezi hilo limefanyika kabla ya mtume kufariki.
Lakini kingine suala la kufutwa kwa aya nilikwambia kabla na nikakuwekea jina la kitabu urejee, lakini huenda ninayo yaongelea ni mapya kwako. Sasa unapopewa muongozo fuata ili usiendelee kuonekana mbambaishaji.
Kwasababu mwanzo nilipokupa pages ya sehemu ambayo ina hiyo Quote hukumakinika na kuangalia page nyingine tofauti ambayo haikuwa lengo langu, na ulipoona hiyo Quote haipo ukaleta screenshot hapa kama ushahidi kuni prove wrong kua nimepotosha (mpaka muda huo kwako hicho kitabu kilikuwa authentic)
Nakuuliza swali unakubali kama nilikueleza juu ya aya zilizo futwa katika Qur'aan unakubali ?
Kingine ishu ilikuwa ni wewe uyarejeshe yale maneno kwenye kile kipande ulicho screenshot kwenye kitabu asili lakini hukufanya hivyo.
Kuna maswali nimekuuliza naomba unijibu, maana naona unatafuta huruma.
Since nimeku correct kuwa hiyo page uliyoweka sio ambayo nimekuambia, na nikakuonesha na screenshot yake, hukurudi tena kuijibu hiyo hoja.
Sasa nirudi tena kujibu ujinga ambao nilishakujibu huko mwanzo, na ukisoma hicho hicho kitabu hayo maneno yabajielezea wazi kuwa yapo katika mlango wa "Nasikh wa al Mansukh" hivi unajua maana ya hayo maneno ?
Kingine huu ndiyo utaratibu wangu napoona mtu namjibu hoja zake anarudia rudia huwa nashika njia naangalia hoja mpya. Siwezi kupoteza muda na mjinga, sababu mtu makini na anaye taka kujua ukweli ushahidi mmoja utamfaa na kumtosheleza lakini mtu mbishi na asiyetaka ukweli hata umpe hoja au shahidi elfu hakubali, na huyu ndiyo wewe.
Au wewe unataka nikwambie nilikimbia, nikaenda kusoma si ndiyo au unataka nikupe jibu gani ? Au nikwambie swali lako lilikuwa gumu nikaenda kusoma ? Jalia vyote hivyo, haya kimebadilika nini ? Kijana unapoteza muda kwenya hakuna.
Matokeo yake umeanza ku flip maneno kua hicho sio kitabu kilichozungumza ukweli na kwamba inatakiwa nisome kitabu kilichaondikwa kwa lugha ya asili (kiarabu) ili niweze kugundua hilo. (kuanzia hapo kitabu ukakitoa authenticity)
Nani kati yangu mimi na wewe alikuwa anamshauri mwenzake asome kitabu cha asili ? Bila shaka ni mimi. Hizi translation nyingi huwa hazikidhi haja, kingine watu wengi wanafanya mambo kwa udanganyifu,labda kama wewe si msomaji wa vitabu, sisi wengine vitabu ndiyo maisha yetu, vitabu ndiyo mapambo yetu yaani hatuwezi kuishi nila mavitabu.
Huu ushauri huwa tunaambiwa na walimu na sisi tunawaambia nyinyi vijana, maana yake unapaswa usljifunze lugha kama unataka kuwa mtafiti na upate kile hasa kilichokusudiwa, wapo watu kibao wanaamua kujifunza lugha fulani kwa lengo kufanya utafiti fulani.
Sijasema hicho kimeandika uongo, nimesema hicho kipande ulichokikusudia wewe kwenuye kitabu asili hakipo, sasa nakuuliza wewe kimetoka wapi ? Lakini hujaona kama nimekubali ya kuwa hayo ya humo yapo katika mlango wa "Nasikh wa al Mansukh" kama ilivyo kwenye kitabu cha asili, na ndiyo maana nasisitiza kwamba kwanini hukusoma hiyo translation na ukaona fika kwamba hayo yamo kwenye chapter hiyo ya aya zilizo futwa ? Sasa ujinga wako usiutafutie upenyo, wewe kubali tu kwamba hili limekushinda na hoja huna.
Sasa nakuambia hivi, kwa mtindo huu unao enda nao wa "shortcut" hautakufikisha kokote. Bora upoteze miaka na mikaka kujifunza jambo na ukapatia kuliko kupita mapito unayo pita.