Pi Network, imebaki siku Moja watanzania tujifunze kuhusu crypto scam, litakuwa ni funzo muhimu sana ili kuepusha wakurupukaji kwenye crypto

Pi Network, imebaki siku Moja watanzania tujifunze kuhusu crypto scam, litakuwa ni funzo muhimu sana ili kuepusha wakurupukaji kwenye crypto

Kuna Uzi nilifungua kuhusu scam aliyotufanyia Mo Dewji, Kwa kujifanya account yake ilikuwa hacked, na wengi tulifahamu baada ya Kanye west kutufumbua macho.

McAfee aliwahi kusema alikuwa na uwezo wa kutengeneza pesa nyingi kuliko Mungu, akiwa na Lockheed Martin kwasabu ya kutengeneza black software, Kwa wale msiofahamu kuhusu black software, black software ni zile software unazopewa task utengeneze lakini haziko public available, na Wala hauwezi kuwa na ruhusa ya kusema in public ulitengeneza software Gani, mana ukianza tu kuzigusia hata Kwa uchache ktk public unakuwa ni national threat, mwisho wa siku inabidi wakuue.

McAfee alipiga pesa nyingi kwenye crypto sio kwasabu ya kutrade bali kumention coin ambazo watu wanunue na kuuza kwenye Twitter Kwa sasa X, alikuwa anapewa commission yake lakini wamiliki wa coin walipiga pesa ndefu kutoka Kwa raia au followers wa McAfee, mana walikuwa wanacheza na Liquidity.

Kwa wale ambao tunafuatilia Habari ndiomana tunaona black project ambazo wamezifanya USA kwenye Area 51, Kuna wanajeshi zimewasababishia kansa lakini wanachohitaji ni matibabu tu sio fidia, na hata uwaulize walikuwa wanafanya nini Area 51 hawawezi sema kwasabu ni classified project, na hata taarifa za kuthibitisha kwamba walishiriki haziwezi patikana kwasabu ni National interest,

Leo nataka niwaambie wale wote wanaomiliki Pi, kuwa Pi ni scam project haitompa mtu umilionea zaidi ya wamiliki kwasabu wamepiga pesa nyingi kwenye Ads na data mining, wamekusanya KYC na kuuza Kwa makampuni yanayohusika, hususani MeTa na Google.
Pi yaweza kuwa ni black project ya kukusanya taarifa zenu na kuweka malware kwenye simu zenu.

Crypto unahitaji elimu na sio ukurupukaji, ndiomana ma CEO wa Pi ni social engineers sio crypto enthusiast, kaangalie hata chuo alichosoma CEO wa Pi wame mremove kwenye bio ili wajiepushe na scam ambayo kesho mtaishuhudia.

Kama unaelewa crypto mining huwezi sema unamine Pi, ndiomana apps zote za mining play store walishagazitoa.

Watu wanafikiri pi itampiku BTC lakini haiwezi japokuwa BTC Kuna siku itakuwa na anguko kubwa pale watu watakapojifunza maana halisi ya privacy, kwasabu huwezi amini katika privacy na unatumia CeX (centralized exchanges) kama Binance, Coinbase n.k kwasabu ni trackable.

Bitcoin sio anonymous bado ni trackable kwahiyo naamini kizazi kijacho hakitoitumia Bitcoin kwasabu ni zero privacy.

Sasa vipi kuhusu Pi ambayo ni KYC based, haziko open source tujue wanafanya nini Wala Chochote, lakini wajinga wanaikumbatia na hususani wazee wa affiliate,
Niwaambie tu Pi haitofika hata 1$ ila itavanish

Sasa kesho tusubiri kuona crypto millionaire wa Pi Network waje hapa mana ni siku ya Mainnet.
Daaaah nimeliwa. Mpaka sasa nina 5,000pi, 1980pi tayari iko migrated kwenye wallet na bado nachimba. Hii taarifa imeninyong'onyesha sana.
 
ivi tafauti yenu na LBL ni nn maana na nyie kazi yenu kuangalia matangazo 🤣
matangazo hayakua lazima kuyaangalia na wengi waliya switch Off.
Sasa sijui unazungumzja matangazo yapi wakati kuna sehemu ya ku disable!

Mimi ubishi na watu ndugu yangu huwa siwezagi! hasa kwa kitu ambacho tunatofautiana ufahamu na uelewa
 
Daaaah nimeliwa. Mpaka sasa nina 5,000pi, 1980pi tayari iko migrated kwenye wallet na bado nachimba. Hii taatifa imeninyong'onyesha sana.
umeliwa kivipi? kama inawezekana nitumie hizo migrated alafu delete account yako maana kuna options pale kwenye profile.

wewe unawasikiliza hawa vichwa maji hawajui chochote
 
matangazo hayakua lazima kuyaangalia na wengi waliya switch Off.
Sasa sijui unazungumzja matangazo yapi wakati kuna sehemu ya ku disable!

Mimi ubishi na watu ndugu yangu huwa siwezagi! hasa kwa kitu ambacho tunatofautiana ufahamu na uelewa
huezi yazima forever yale ukiswitch off after some time unaanza kuyaona tena
 
Daaaah nimeliwa. Mpaka sasa nina 5,000pi, 1980pi tayari iko migrated kwenye wallet na bado nachimba. Hii taarifa imeninyong'onyesha sana.
Endelea kuchimba ndio ubilionea wenyewe
 
mimi na mine Pi tangu 2019 ndio nayejua.
1740669746934.png

Oyaa unawajua hawa mabilionea wenzako? apa walikua wanapanga mkakati wa kuwekeza kila mkoa 🤣 🤣 🤣
 
🤣 🤣 🤣 mabilionea wavivu au sio
Hao ni wehu wanaotembea siku moja nilijaribu kuangalia kama Azania , Azam , Mo kama wako kwenye masoko mtandao sikuwakuta , nikamcheki vunjabei kama Yuko kwenye masoko mtandao sikumkuta nikajiridhisha hawa wajinga wanaopagawa na platform mbalimbali ni wendawazimu , maana kajitu hakana production , hakana kiwanda , nako kapo mbele kama kisimi nikajua hii mijinga kweli , nikakuta kuna watu wa West Africa wengi nikajua tayari matahira lazima yapigwe tu
 
wewe na wale vijana wa zumarudi mna tafauti?
Hao watu wa pi ni wendawazimu dunia nzima haina mfumo wa kumtajirisha mtu kizembe check akina Amani, musk wote hutowakuta huko Sana utawakuta masoko ya hisa hao sio wajinga Wana real investments na daily Wana hustle kupata tenda mbalimbali sasa hii mijinga inayoshoboka kizembe Acha ipigwe kwani wale ndugu wa bitcoin ushawaona wamepata ubilionea ? Maana kila siku wanalia tu
 
wew
kwahio mpaka sasa utakua bilionea si ndio? si ulikua unajua price ni laki 3 ukatuona mazoba, si ndio ndugu bilionea
wewe jamaa tukiendelea kubishana na mimi nitaonekana mjinga! Ishu ni kukupuuzia tu
 
Pesa ni matokeo ya kufanya kazi kwa bidii, kua mbunifu , kutatua matatizo katika jamii, tofauti na hapo ukiona unaitwa kwenye fursa jua wewe ndio fursa ya waliokuita, fursa sio rahisi kiasi hicho
 
Back
Top Bottom