Yawezekana kabisa mkuu, alafu wengine wamekuwa wezi kuliko hata hawa wanawake tunaokutana nao mitaani. Yaani mpaka unawaza kama kweli mlioana kwa nia ya kujenga familia au la. Yaani asione pesa mbele yake, unaweka mitego na unamnasa anakwambia nimechukua kidogo tu nilikuwa na shida nayo, na hapo umetoka kumpa hela na biashara umemfungulia.
Nimewahi kushangaa diku moja askari wananifuata kitaa, naambiwa natakiwa kituoni, kufika nawekwa selo hadi kesho yake mchana. Nawauliza kosa ni nini na kwa nini niko hapa, naambiwa utajua kesho. Inafika keho yake mchana wife kafika, napelekwa dawati la jinsia, na shauri linasikilizwa. Naambiwa siuudumii familia, napigwa na butwaa, na mshangao kabisa, anadai anataka ATM kadi yangu,nakumbuka niliwahi kumwachia kadi hiyo nikiwa masomoni nje kwa takribani miaka miwili na nikakuta hakuna hata balance. Usafiri nimemnunulia, mafuta naweka mimi, watoto shule wanasoma nzuri kabisa. yeye mwenyewe nimempeleka shule na ajira nimemtafutia, ameacha ajira anataka bishara. Biashara imemshinda kutwa ni kubadilisha nguo na style za nywele. Natoka selo mchana wa saa nane, napokea simu toka kwa HR, ananambia brother nini tena kimetokea! Mkeo kaja hapa anataka mgawane mshahara 50/50, Naona huyu sasa ana mental kesi au karogwa.
Nikaamua kuondoka nianze maisha mapya, mzee wangu mmoja akanishauri nisiondoke. Akasema kata mirija yote ya pesa na adabu itarudi, kukimbia familia ni laana kwa mila zetu. Nikakata mirija, biashara imecolapse, gari mafuta na hata aservice hakuna. Familia natoa mahitaji yote ya muhimu, ngumu kumeza nikapunguza kabisa. Kwa sasa adabu inarudi na sitorudi nyuma.
Kuna baadhi ya wanawake ni pasua kichwa kwelikweli. unamwambia ondoka ukapumzike kwenu anagoma. Mama mkwe anatetea binti yake balaa. Nayakumbuka maneno ya mama, miaka takribani 17 nyuma, akinikanya kuwa huyu unayemuoa atakusumbua. Nabaki kukumbuka na kusikitika sana.