Mkuu Mohamed Said naomn unisaidie vitu viwili.
la kwanza ni naomba ya kupata vitabu vyako especcia lly kama kuna softcopy za kudownload.
La pili,naomba unisaidie kujua akina nani kutoka kaskazini(kwa majina) walikuwa vinara wakati wa kutafuta uhuru wa Tanganyika.
Nashukuru.
Gazaniga,
Ikiwa uko nchini unaweza kununua kitabu cha Abdul Sykes nakala ya Kizungu
au Kiswahili Ibn Hazim Media Centre Msikiti wa Mtoro na Manyema kwa nakala
shs: 10,000.00 au Tanzania Publishing House (TPH) Samora Avenue.
Wanaharakati wa Kaskazini Arusha ni kundi la Japhet Kirilo na Moshi ni kundi
la Yusuf Olotu maarafu kama Yusuf Ngozi.
Hii ni kwa kuwataja wachache.
Hakuna ukweli ambao Wazanzibari HAWAPENDI kuusikia kama huu na sijui kwa nini inakuwa hivyo!
John Okello atabaki kuwa mtumuhimu sana wa kukumbuka katika historia ya Mapinduzi ya Zanzibar milele na milele.
Kuna Tofauti kati askari wa kukodi , Mercenary na wapigania uhuru. Okelo hakuwa mpigania uhuru bali ni askari wa kukodi kwa ajii ya kuipindua serikali halali ilochaguliwa na wananchi na pia kusimamia mauaji ya waislam .
yeye anakumbukwa pamoja na walomtuma kwa unyama alowafanyia waislam wa znz.
Waislam wa nchii hii sio walijitolea wao binafsi na mali zao kwa ajili ya kuona nchi hii inakua huru.
walitoa mali zao na ardhi zao kwa watanzania wenzao kama mchango wao kwa taifa hili , mfano
huku waislam wakijitolea hali na mali zao upande mwengine wao wakatumia nafasi hio ya uhuru kujikusannyia ardhi nyingi kwa matumizi yao wenyewe
- Sheikh Mohammed Abdalla Tambaza, kila mtu anajua eneo lote la Upanga Shule Ya Tambaza, Msikiti wa Maamur , Maeneo ya Makaburi ya Kisutu , nk
- Mzee Mwinyi mkuu mwin'juma wa Magomeni ametoa ardhi yake kwa matumizi ya waislam na watanzania
- Sewa Haji , aliejenga Hospital ya Muhumbili
- Majengo ya Bunge ya mwanza yalotolewa na Familia ya Karimjee
- maeneo ya makaburi ya kinondoni
Zanzibar ilipataje uhuru na ilikua mwaka gani?
Na hiyo serikali halali iliingia vipi na chini ya rais nani madarakani kabla ya mapinduzi ya Field Marshal John Okello.?
Mbona unaandika kama hujui historia yako? Hao waislamu unaodai walijitolea Mali zao kwa "watanzania" wenzao ilikua ni mwaka gani?
Punguza kukusha Madrasa, mwenzio bi faizafox kajigomboa na elimu dunia walau anajua dunia inavyokwenda.
Nnahisi kwa kuwa hilo ni baraza la wazee, Ali Sykes siku hizo ni kijana.
Nakujibu hivi: You re totally wrong!
Usiwe mvivu wa kufikiri.
Jisomee nani aliijenga Muhimbili na mwaka gani.
Kabla ya hapo ilikua ikiitwa jina gani. Jee hujaona hata ile wodi pale ikiitwa Sewa Haji ?
Jee huujuu ukumbi wa bunge wa mwanzo ? Ule mpaka kedho unsitwa karimjee
Jee huijui shule ys Tambaza ? Kile kiwanja na shule ys muhimbili vyote ni ardhi za familia ya Mzee Tambaza.
Jee huyajui makaburi ya kisutu?
Na pale makaburi mnayozikana kinondoni zote zile ni ardhi za waislam.
Tanganyika ukenya uganda zanzibar zote zilipatiwa uhuru mmoja baada ya mwengine kuanzia 1961 . 1962 na 1963.
Zote uhuru ulipatiwa December.
Znz harakati za kugombea uhuru ziliwashirikisha wote ASP ZNP ZPPP na Umma party .
uchaguzi ulifanyika ma ZPPP na ZNP wakaunda serikali ya uhuru.
Zanzibar ikajiunga na UN mwaka huo huo ma pia ikawa mwanachama wa CWealth.
Then okelo akatumwa kufanya mapinduzi.
Uhuru wa Zanzibar ulipatikana 23 Dec. 1963
Safi sana mkuu ndo ajabu hyo pia watu walikua hawajui kuwa ilikua ikifika ramadhani huyo nyerere alikua anafunga pia.
Mohammed said vp naweza kupata vitabu vyako?
Wewe Shori acha mambo ya kuhisi; mbona Dossa Azziz aliyekuwa umri mmoja na Ally sykes yumo kwenye hiyo picha?
Bulesi,
Baraza la Wazee wa TANU hakika lilikuwa kama jina lake linavyosema ni
baraza la wazee.
Dossa unamuona hapo na Nyerere sababu ni kuwa Dossa alikuwa na gari
na mara zote alikuwa na Nyerere katika safari na mizunguko hapo mjini.
Dossa aliweza kufanya haya yote kwa kuwa Dossa hakuajiriwa alikuwa na
biashara yake mwenyewe kwa hiyo alikuwa huru kushughulikia mambo ya
TANU mchana kutwa.
Ally Sykes alikuwa akifanya kazi Government Stores kwa hiyo nyakati za
mchana hakuweza kupatikana pale New Street Makao Makuu ya TANU
ilipokuwa ofisi ya Nyerere.
Katika utafiti wangu picha ambayo niliyoiona ya Ally Sykes na Nyerere ni
moja tu.
Picha hii ilipigwa nyumbani kwa Ally Sykes Mtaa wa Kipata kabla ya uhuru.
Picha ya chini ni nyumba hiyo ndogo ni ofisi ya TANU baada ya kujengwa
upya kupisha ile ya asili iliyojengwa kati ya 1929 - 1933.