Picha: Dar es Salaam waonesha uhalisia suala la bandari nchini. Viongozi wajitafakari sana

Jamami mbona mkataba wa uendeshaji bandari bado?

Hivi ni kipi hamuelewi?
 
Bandarini pale ni wizi mtupu. Usione watu wanapinga ujio wa DP world ukafikiri ni wazalendo. Ukweli ni kwamba wanaopinga mkataba wengi ni wale wezi wa bandarini, wapitisha madawa ya kulevya na vishoka.
Nakwambia, hii rasharasha tu, hata kazi za DP-WORLD hazijaanza rasmi, vitu vya "polomosheni" siku hizi havionekani mitaani kwetu.
 
Wakazi wa Dar na viunga vyake tunazijuwa dursa zitazozalishwa na bandari ya kisasa.

Hao DP WORLD wengine hapa tunawangoja kwa hamu. Tuna vijukuu vyetu tunataka violewe Dubai.

Fursa hizo.
Fursa nyingi zinakuja, but watakaoziona ni wachache ambao akili zao bado hazija athiriwa na wanasiasa uchwara.
 
Saa 8 hii bado upo kitandani unaota. Tatizo la ndoto unaweza kuota kuwa wewe ni tajiri namba 1 duniani, lkn ukija kushtuka unakuta mfukoni huna hata 200 ya kununua muhogo wa kula.
Hahaha, mjukuu wangu siku moja kanizushia ugomvi alipoamka. Anasema kapewa minoti na mama'ke imejaa mifuko yote, nimrudishie.

Nimelipa deni wiki nzima, kila siku buku.
 
Wewe umeolewa?

Kama bado hujaolewa nakushauri itumie fursa, tafuta jihandsome la Kiarabu lenye Dirham zake uolewe Dubai.

Usiziwachie fursa za DP World.

Ngino nje ya ndoa usiisogelee kabisa. Haramu.

Unamshauri akachanganye damu na wauzao wa Mtume SAW? Yuko mmoja alimshauri mkewe. Bahati mbaya mama akashindwa kutofautisha Banyiani na wale wa uzao wa Mtume. Jamaa akaishia kumuuliza mkewe mbona mtoto ananywele za singa. Akajibiwa kitanda hakizai haramu.
 
Acha unaa na fitina chawa wa🍀. watanzania ni waelewa na waungwana.Ila usisahau ahadi yenu feki,Kuwa fitina kwenu mwiko,na pia mnasema rushwa ni adui wa haki,isije Kuwa mengi ya mitazamo yako inaongozwa kwa nguvu ya mlungulatu,ili kuwaandama wazalendo wa kweli,na kuwaomba mafisadi🤔
 
Mpaka mtumie makalio kuongea ndio mtaeleweka kwa sasa tunasema bandari haiuzwi
 
Kitanda toka lini k8kazaa? Anaezaa anaelalia kitanda.

Huyo afanye toba, uzinzi ni haramu.
 
Ni kama unachanganyikiwa!! Pole
Nichanganyikiwe kwa lipi?

Kwa hili la wana Dar es Salaam kushtuka na kukataa kutumiwa na wanasiasa uchwara kwenye ajenda zao na kupelekea mkutano wa bandari kudoda?

Au kwa hili la watu kutumia ID kumi kumi mitandaoni ili kuwahadaa wasiojua kinachoendelea afu mikutanoni wanahudhuria watu wawili watatu?
 
Aheri hata papai lina faida, unaweza kulila.

Uwe na majitu yenye upungufu wa akili kama mleta mda halafu utegemee maendeleo! Laana kubwa ya nchi yetu ni aina ya watu ilio nao.
Siku zote chizi (mtu asiekuwa na akili) humuona mzima kuwa ndio chizi. So sishangai wewe kuniona mimi sina akili, ilihali kiuhalisia wazima tunajua kuwa wewe ndio huna akili.
 
Wewe waonyesha ni msomi wa hali ya juu.Unatuelezea,na kukuelewa ki urahisi sana.Mengi ilikuwa siyajui,lakini nimeyajua kupitia uzi huu wako.
 
Huu ndio ukweli.Endeleeni kutuelimisha wananchi wa kawaida.
 
Ni kweli kabisa.
 
Sasa wewe shuleni unawezaje kujibu swali ambalo haulioni?

Wanaokudanganya kuhusu mapungufu ya mkataba huwa hawakuwekei mkataba wenyewe uuone na kuona mapungufu. Badala yake huishia kukwambia tu porojo kwamba sijui bandari imeuzwa, sijui mkataba mbovu nk bila kuonesha kifungu kinachoonesha mauziano ya bandari wala ubovu wa mkataba.

Na wanafanya hivyo makusudi kwa sababu wana amini bado kuna baadhi ya watanzania ni wajinga, namaanisha wale wanaoamini chochote wanachoambiwa hata kama hakina ushahidi.

Weka mkataba hapa uoneshe mapungufu kifungu kwa kifungu na wajuzi wakujibu kifungu kwa kifungu.
 
Fursa nyingi zinakuja, but watakaoziona ni wachache ambao akili zao bado hazija athiriwa na wanasiasa uchwara.
Kuna mtu amenambia DP World wakishaanza kazi wataleta vichwa vya trucks (tractor) 300 na trailers 1,000 na kuwako pesha transporters wadogo wadogo bila riba ili mizigo yao ifike kwa wateja wao kwa wakati.

Hii ni fursa kubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…