PostGE2025 PICHA: Hii ndio Ambulance mpya ya Mbunge Sara Msafiri aliyoikabidhi kituo cha Afya Mziha, Yeye amshukuru sana Rais Samia

PostGE2025 PICHA: Hii ndio Ambulance mpya ya Mbunge Sara Msafiri aliyoikabidhi kituo cha Afya Mziha, Yeye amshukuru sana Rais Samia

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Shekaina Glory

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2025
Posts
207
Reaction score
116
IMG-20251217-WA0112(2).jpg

MBUNGE SARA MSAFIRI AKABIDHI AMBULANCE KITUO CHA AFYA MZIHA

Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Mheshimiwa Sara Msafiri, amekabidhi rasmi gari la wagonjwa (ambulance) kwa Kituo cha Afya Mziha, huku akitoa maagizo mazito kwa uongozi wa kituo hicho kuhakikisha gari hilo linatumika kikamilifu kwa lengo la kuokoa maisha ya wananchi.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Mziha, Mheshimiwa Msafiri amesisitiza kuwa ambulance hiyo ni mali ya wananchi, hivyo inapaswa kutunzwa, kulindwa na kutumiwa kwa uwajibikaji mkubwa, bila kutoza gharama zisizo rasmi wala kutoa visingizio vya ukosefu wa mafuta au kutokuwepo kwa gari pindi huduma ya dharura inapohitajika.

Aidha, Mbunge huyo amewataka wananchi kushirikiana kwa karibu na uongozi wa Kituo cha Afya Mziha ili kuhakikisha huduma ya usafiri wa dharura inapatikana wakati wote kwa wananchi wote wanaohitaji.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Sara Msafiri amepongeza uongozi wa Kituo cha Afya Mziha kwa ushirikiano mzuri waliouonesha na Kituo cha Afya Chazi katika kipindi ambacho Mziha haikuwa na ambulance, akiwataka kuendeleza mshikamano huo kwa maslahi mapana ya wananchi wa Mvomero.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero amesema uwepo wa gari la wagonjwa haupaswi kuwa chanzo cha usumbufu kwa wananchi, akisisitiza kuwa huduma ya dharura inapaswa kupatikana bila vikwazo, huku akitoa onyo kali kwa watumishi watakaokiuka maelekezo hayo.

Awali, Diwani wa Kata ya Mziha, Denis Ezekiel, amesema kabla ya kupatikana kwa ambulance hiyo, wananchi walilazimika kufuata huduma ya gari la wagonjwa kutoka kata jirani, safari iliyokuwa zaidi ya kilomita 108 kwenda na kurudi, hali iliyosababisha ucheleweshaji wa kuwafikisha wagonjwa Hospitali ya Turiani na kuhatarisha maisha yao.

Naye Mlezi wa Kituo cha Afya Mziha, Alex Mzava, amesema licha ya kituo hicho kukamilishiwa vifaa vyote muhimu vya upasuaji, bado kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji, hali inayokwamisha kuanza kwa huduma za upasuaji na huduma nyingine muhimu kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mziha amesema wananchi wa kijiji hicho kwa muda mrefu wamekuwa wakikumbwa na changamoto kubwa za huduma za afya, ikiwemo usafirishaji duni wa wagonjwa pamoja na vifo vya mama na mtoto, hali iliyosababisha mateso makubwa kabla ya kupatikana kwa msaada huo wa gari la wagonjwa.
 
Sara unajitahidi kujipigia debe na kuhalallisha kujisimika kwa CCM madarakani bila ridhaa ya wananchi ukweli ni kuwa hakuna aliyekuchagua , maana tarehe 29 hakukua na uchaguzi bali mauaji ya halaiki.
 
Sara unajitahidi kujipigia debe na kuhalallisha kujisimika kwa CCM madarakani bila ridhaa ya wananchi ukweli ni kuwa hakuna aliyekuchagua , maana tarehe 29 hakukha na uchaguzi bali mauaji ya halaiki.
Sasa kama CHADEMA mligoma angefanyaje?
Gari ya wahisani hiyo aache porojo. Hakuna pesa ya serikali iliyonunua gari hiyo. Kibao cha namba ya gari kinaonesha hivyo.
Wahisani gani?
 
Tuliza nyege waambie ukweli gari limetolewa na mabeberu
 
Back
Top Bottom