Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Hujuma hizi si kwa SGR tu, watu wanakata vyuma kwenye madaraja, wanafungua vyuma vya nguzo kubwa za Tanesco, wanaiba taa za sola, wanaiba waya za umeme mitaani, mita za maji, vyuma kwenye reli za Tazara na TRC na nguzo za alama za barabarani. Tukisema wanaihujumu SGR ni kukuza mambo na kutuaminisha huo wizi mwingine ni wa kawaida usiohitaji kudhibitiwa, wizi unaofanyika kwenye SGR ulianza mwanzo tu mradi ulipoanza ikiwemo vifaa vya ujenzi na mafuta. Serikali inaweza kudhibiti haya kwa kusimamia biashara ya vyuma chakavu zinazofanyika kiholela nchini.Bado tuna safari ndefu mno. Pichani ni hujuma zinazofanyika kwenye miundombinu ya Reli ya Kisasa (SGR)View attachment 3148683View attachment 3148684View attachment 3148685View attachment 3148687View attachment 3148688