PICHA: Je Unaikumbuka Jambo Forums? Ulikuwa Wapi enzi hizo?

PICHA: Je Unaikumbuka Jambo Forums? Ulikuwa Wapi enzi hizo?

Lkn jamani rara rere ,napendekeza apewe tuzo ya ku like,jamaa anashine sana karibia kila jukwaa kwa ku like tu,
Au apewe cheo cha u platinum member!!!,teh teh tehee,najua ni ngumu kupata cheo hicho,ma expert member tuko wengi humu.
 
Tuyaache hayo mkuu naona unataka kupanic
Siyo nataka ku panic nyie wabongo wengine hamna adabu wala ustaarabu.

Mtu humjui kihivyo ushataka utani naye mpaka kumuuliza mambo personal ya watoto wake.

No home training. No couth.

Yani wewe ndiye hujafundishwa ustaarabu kwenu, ukiongea unanuka mdomo, nikikuambia hapo umeharibu, this is offensive, siyo poa, unanilaumu mimi na panic.

Unamkanyaga mtu kwenye daladala halafu akikuambia hapa umenikanyaga unamwambia asi panic asikupigie kelele.

Kujamba unajamba wewe kwenye halaiki, halafu ukiambiwa hapo umeharibu, lawama unampa aliyekuambia umejamba.

You are so self- unaware.
 
duh maisha yanakwenda mbio sana, ilikua ni mwendo wa kushinda kwenye internet cafe tu
 
Mtandaoni niliingia first mwaka 2001 kwenye computer ya msomali mmoja wa East Africa Fuel Co ltd,,japo nilijua kuna internet tangu 1993 kupitia magazeti ua Newsweek na Time nilikua nayasoma kwenye library ya kanisa catolic,,magazeti yalikua yanaletwa kwa padre,akimaliza kuyasoma anayaweka library,,nadhani kwa wilaya ile mi ndo nilikua msomaji pekee wa hayo magazeti😂
 
Yale magazeti ilikuwa ukitoka kusoma habari zake halafu kuwahadithia wabongo wanakuona mtu wa ajabu.

Kuna magazeti hayo ya Newsweek na Times ya mshua nilikuwa nasoma miaka ya 1993 - 1996, habari za ozone layer depletion due to Chlorofluorocarbons (hii kuiandika na kuitamka tu wabongo walikuwa wanaona uchawi). Habari za antibacterial resistance, habari za Big Bang Theory.

Nilikuwa nasoma humo halafu nakwenda kuwahadithia watu kijiweni na shuleni watu wanaona kama habari za dunia nyingine.

Kwenye mtandao nilitengeneza website yangu ya Geocities mwaka 1996. Sadly zile websites za geocities waliziondoa zote.

Miaka hiyo ukijua kutengeneza website unaonekana wewe mtu fulani wa ajabu sana. Mtaani walikuwa wananiita "kijana wa dotcom".

Tulikuwa tunaenda internet cafe ya Raha Tower pale na producer Roy Bukuku (RIP). Roy mchizi yule anakaa kwenye computer kaiunganisha na website imeibadilisha ile keyboard ya computer imekuwa keyboard ya muziki, halafu anakupigia muziki kwa kutumia keyboard ya computer, inakuwa kama keyboard ya muziki.

Nikamwambia Roy wenzako ndiyo kwanza tunajifunza internet wewe ushaiunganisha keyboard ya computer iwe keyboard ya muziki na unatengeneza nyimbo tayari?

Those were the days maan!
 
Yale magazeti ilikuwa ukitoka kusoma habari zake halafu kuwahadithia wabongo wanakuona mtu wa ajabu.

Kuna magazeti hayo ya Newsweek na Times ya mshua nilikuwa nasoma miaka ya 1993 - 1996, habari za ozone layer depletion due to Chlorofluorocarbons (hii kuiandika na kuitamka tu wabongo walikuwa wanaona uchawi). Habari za antibacterial resistance, habari za Big Bang Theory.

Nilikuwa nasoma humo halafu nakwenda kuwahadithia watu kijiweni na shuleni watu wanaona kama habari za dunia nyingine.

Kwenye mtandao nilitengeneza website yangu ya Geocities mwaka 1996. Sadly zile websites za geocities waliziondoa zote.

Miaka hiyo ukijua kutengeneza website unaonekana wewe mtu fulani wa ajabu sana. Mtaani walikuwa wananiita "kijana wa dotcom".

Tulikuwa tunaenda internet cafe ya Raha Tower pale na producer Roy Bukuku (RIP). Roy mchizi yule anakaa kwenye computer kaiunganisha na website imeibadilisha ile keybiard ya computer imekuwa keyboard ya muziki, halafu anakupigia muziki kwa kutumia keybiard ya computer, inakuwa kama keyboard ya muziki.

Nikamwambia Roy wenzako ndiyo kwanza tunajifunza internet wewe ushaiunganisha keyboard ya computer iwe keyboard ya muziki na unatengeneza nyimbo tayari?

Those were the days maan!
alikuwa mbele ya muda, rip.
 
Nlikua chuoni India
Maswali kuhusu India. Niwie radhi kwa ujinga wangu.

Nimesoma na Wahindi. Nimefanya kazi kwa ukaribu na Wahindi. Bado nafanya kazi na Wahindi.

Yote hayo ni nje ya India.

Wahindi wanajulikana kwa mapenzi yao ya kutumia viungo vyenye harufu kali sana.

Ukienda kwenye nyumba zao wanakoishi, ni harufu ya viungo tu….binzari, mdalasini, n.k.

Kutokana na utumiaji wao huo wa viungo kwenye vyakula vyao, hata harufu za miili yao ni kali na mbaya sana, hususan kwa wale ambao si wasafi.

Huko India, sehemu zote huwa zina harufu ya curry? Hata ukiwa barabarani harufu ya curry ipo?

Kwenye vyombo vya usafiri je? Na kwenyewe kumejaa harufu ya curry?
 
Je Unaikumbuka Jamboforum?
Leo Kwenye Kufukunyua Makabuli kwenye Picha Zangu Nimekumbana na Picha Ya Mojawapo Ya Kurasa za JamboForum enzi Hizo Ambayo Kwa sasa ni Jamiiforum..

Ama Kweli Tumetoka Mbali, asante sana Maxence Melo kwa kutufikisha kwenye Maudhui Bora na Hakika Tumetoka Mbali sana..
View attachment 3204571
Dan Kilingeni Msata nalisongesha.. Nilikuwa faya mno kwa tiba za ukagugi wa kienyeji😀 hata siamini kabisa ndio mimi wa sasa wa never miss church😉
 
Nilikuwa member wa jambo forums kabla haijawa jambo forums. Tulikuwa tunabishana yahoo groups. Dikumbuki majina ya groups huko, lakini nahisi jambo forums ilianzia yahoo.
JamboForums ilianzia na Bcstimes.com mwaka 2005.

Bcstimes.com ikadukuliwa na kuathiriwa na virusi vya Condor dragon.

Mdogo mdogo ndo ikazaliwa JamboForums.

Mimi, Mwanakijiji, Mkandara, Njabu Ngabu, Jasusi, Fikiraduni, Reverend Kishoka, Deshbhakt, FMES [Le Mutuz]na wengineo, ndo tukahamisha makazi huku.

At the same time, Youngafricans.com nayo ndo ilikuwa ipo kwenye siku zake za mwisho.

Members wa huko nao wakaanza ku migrate huku.
 
Hakika
 
Back
Top Bottom