Acha ujinga wewe usiwe mtu wa kukimbilia kuandika bila kufikiri. Yani mwenzio kaandika bila kufikiri na wewe pia umekimbilia kum quote bila kufikiri ukidhani uliem quote atakuona mjanja.
Unataka kuniambia wewe umekariri code za nchi zote duniani hata zile ambazo hazina umuhimu wowote kwako?
Nigeria mimi sina baba, mama wala ndugu yoyote anaeishi kule, na isitoshe sina mpango wala fikra za kwenda kuishi kule, sasa unataka nikariri namba za nchi yao kwa sababu ipi? Yani mtu na akili zako uishi maisha yako kwa njia za kukariri na kuhifadhi code namba za nchi zote duniani hata zile ambazo hauna mpango wa kwenda katika maisha yako?
Wewe ulitakiwa uniulize mimi sababu ya ku google hizo namba mbili ili nikuambie afu ndo uandike kutokana na kile nitakachokujibu.
Hivi wewe ukiona nyoka afu jamaa anakwambia kwamba huyo sio nyoka ni mjusi utakubali tu kichwa kichwa kisa umekaririshwa? Jamaa amesema yeye ni mmarekani tena boss kabisa wa kampuni husika. Ila namba yake inaonekana kuwa sio ya Marekani bali ni ya Nigeria. Sasa ulitaka mimi nimuache bila kumuonesha kwamba ni ngumu kunitapeli mimi kwa style ile. Lakini pia nimeona kama ningemwambia tu kuwa yeye ni Mnigeria bila kumuonesha sababu iliyonifanya nimuone yeye ni mnigeria ingekuwa ngumu kunielewa. Ndo maana mimi kwa kifupi nika google code namba za US na Nigeria na kumtumia aone kwamb siku hizi kabla ya mtu kutapeliwa huwa ana search ili kujiridhisha. Of course najua mtu anaweza kuwa na namb ya Nigeria na akaitumia nchi yoyote, lakini sio kwa mtu wa aina ya huyu tapeli. Na hasa ukizingatia kwamb Nigeria ndo kunapotoka matapeli wengi hapa Afrika. Bora namba ile kidogo ingekuwa ya UK afu aseme ni raia wa US kidogo ingeleta mantiki kwa boss mzungu wa Marekani kuwa na namba za UK ila sio Nigeria.