Picha: Lift ya kwanza yazinduliwa Jijini Mbeya

Actually naipongeza sana serikali ya ccm kwa hili, hakika wametimiza moja ya sera zao muhimu sana, eboo!? Mkuu wa wilaya hana kazi ati anaenda kufanya uzinduzi wa lift.... Du!? Kweli hii noma......
 
Inashangaza Kidogo ingwa liftinawkenda na urefu wa majengo yanayoruhusiwa,ninachokijua Mbeya kwa sababu ya uwepo wa tetemeko la ardhihurukusiwi kujenga ghrofa zaidi ya tatu na mahitaji ya nlift huja kuanzia ghorma ya nne.

wewe umenikumbusha mbali sana. mwaka nadhani ulikuwa 1965 ule nilikuwa nimetumwa mahali. nadhani ilikuwa kupeleka taarifa fulani kwa jirani mmoja aliyeishi kuvuka vijito viwili. ilikuwa kama saa 4 hivi asubuhi nikawa nimefika kwenye kijito cha kwanza niko peke yangu. kumbuka sasa wakati huo mimi ni kabinadamu kadogo hivi labda futi 3 na pointi kadhaa hivi. basi lilikuja tetemeko kubwa sijaona tetemeko jingine kama hilo tangu siku ile. mto ulikuwa unatetemeka, majani marefu kule kwetu tunaita belebele (hiyo b siyo b unayoijua wewe; ni tamshi kati ya b na v) yakiyumba kushoto na kulia kwa kasi. nilidhani dunia itapasuka siku ile. na wala sikujua kama ningerudi salama nyumbani. bahati nzuri ilikuwa ni kijijini nyumba ndefu za matofali hakuna wakati ule. nyumba ndefu zenye uzito zingekuwepo zingeanguka.

Mkuu acha waoengee sanaa wabongo wengi ni vilaza huwa hatupendi kujuwa tatizo nini
Lift valley(bonde la UFA) nahisi wengi hawajui condition

mkuu point of correction!! ni Rift Valley siyo Lift Valley

ha ha ha ha....
 
reference..
mwaikimba.. mapunda na mwaipopo wacha ambao hawajulikani..
kwa hiyo mbeya ni wana sport hatuhitaji lift.. hata ghorofa 20 tunapanda kwa kukimbia.. lift ni kwa WAZEMBE!
 
Inamaana hata kiberenge walikuwa hawana jamani? ??
 
aisee...
afu nasikia Mbeya bila wachagga haiwezekani...

Wew mat*** kweli wew, unaleta ukabila wako huku. Nenda huko huko banyamulenge wewe. Kwa taarifa yako mby haijatawaliwa na wachaga na hawaiwezi huu mziki mwingine
 

acha kudanganya watu kama hujui stastics kaa kimya, au uliza utasaidiwa, mwanza lift zimekuwepo kwa zaidi ya miaka 40, majengo aliyokuwa na lift kipindi hicho, ni jengo la ccm ambalo lift yake nafikiri ilishaharibika, lingine ni bugando, vipi wewe unasema jengo la NSSF ndio la kwanza?
 
Inashangaza Kidogo ingwa liftinawkenda na urefu wa majengo yanayoruhusiwa,ninachokijua Mbeya kwa sababu ya uwepo wa tetemeko la ardhihurukusiwi kujenga ghrofa zaidi ya tatu na mahitaji ya nlift huja kuanzia ghorma ya nne.

msisingizie matetemeko, ghorofa lolote ambalo lipo kwa matumizi ya kijamii kama ofisi n,k lazima liwe na lift kwa ajili ya walemavu, ndivyo sheria za majengo zilivyo, hili jambo la kuzindua lift ni aibu, bukoba walipata jengo lenye lift miaka kadhaa iliyopita lakini hawakufanya upuuzi huu.
 
Bado kweli tupo nyuma kimaendeleo itachukuwa miaka 50 ijayo na sisi tuwe na Maendeleo kazi kweli ipo jamani.
 
Lift ya kwanza ilipatikana lini?

unauliza lift ya kwanza Moshi acheni hizo unaijua hospital ya KCMC iilijengwa miaka ya sitini na kunalift ndani nakumbuka kuna hotel ina KNCU oppsite na round about yulikuwa tukitoka church na mzee Tunaendakula pale ilikuwa na lift back in the fifties
 
Moshi nilipanda lift 1999 pale Kahawa House!!!.......

mkuu hiyo lift ni zamani hiyo hoteli imejengwa thirties miaka ya themanini nakumbuka mzee alikuwa anatupeleka pale na kulikuwa na lift
 
Mbeya iondolewe hadhi ya kuwa Jiji mara moja..

Huu ni udhalilishaji wa majiji..

Hata Pwagu anakuzidi kete. Joti ndo kakuzidi kabisaaaaa. Labda Jangala unakaribiana naye. Wewe akili yako inajua kwamba kigezo cha mji kuwa jiji ni idadi ya kuwapo kwa lift? Ama kweli mburura zipo nyingi njomba. Hapo unamdhalilisha aliyechagua miji ya kuiita majiji. Lol!:A S angel:
:A S angel:
 

Jengo la kwanza kuwa na lift Arusha lilijuwepo kabla hujazaliwa, AICC ina umri mkubwa kuliko wewe,na si kweli kuwa naura spring ndito ya kwanza bali ya mwisho mwisho kwani hoteli kama Impala zilikuwepi long before hiyo naura, wacha uongo
 

nakusahisha kidogo kuhusu arusha mkuu. jengo la AICC ni la zamani sana. sina uhakika lini lakini tayari yalikua na lifti and im sure AICC imejengwa kabla ya naura spring. pia jengo la ushirika sikumbuki jina lake, lenye ofisi za banka of africa na riverside shuttle, lipo just after metropo ukiwa unaelekea clock tower on your left side. ni la zamani na lina lifti pia.
 

Safi,nilitaka kumjibu hiki hiki kuhusu mwanza,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…