Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 12,826
- 17,371
Muislam gani unautwika?Nimesemwa sana na familia, nimesemwa sana na mke wangu, Msikitini wananisema sana na kunitenga kisa tu mimi mtafunaji mzuri sana wa nyama ya nguruwe [Kitimoto].
Kitimoto ni nyama tamu na pendwa sana duniani kote. Ikiwa kavu ni tamu sana, ikiwa choma ndo kabisa, na ikiwa rosti kwa ugali ni mubashara kabisa ukiwa na beer mbili tatu pembeni.
Si mimi tu, wapo pia wenzangu kibao wanatafuna vyema sana hii kitu. Fresh kabisa.
Tuache nongwa jamani.
Kitimoto sawa waweza kula sehemu ya shida.
Je ulisoma popote katika Korani ikiruhusu kuwa ukiwa jangwani pasipokuwa na maji, ukapata pombe utulize kwa kiu yako?