Picha: Nimepata msongo wa mawazo baada kuona katuni ya leo ya Masoud Kipanya akizungumzia sakata la Wachina

Katuni inaonesha kabla ya ujio wa mchina tuliishi kwa bei zetu na biashara tulikuwa tuna ungishana lakin alipo kuja mchina ameshusha bei ile bidhaa ya mchele na wateja wanakimbilia kwake lakin mchina anunui vitumbua vya uyo mteja anaye nunua kwake mchele yeye uwenda hotel kwa wachina wezake kununua chakula mwishoe mama wa kibongo na muuza duka wa kibongo wanashindwa kuwa na pesa maana akuna anaye muuzia mwezie
 
Kwanini wabongo tusitembee na mbinu hii?
 
Nilivyoelewa hii katuni. Mtanzania anauza mchele kwa elfu tatu na anamuuzia mama ntilie. Baadaye mama ntilie anapika chakula na kumuuzia mwenye duka. Biashara inafanyika. Anaingia mchina na kuuza mchele bei pungufu elfu moja. Mama ntilie anavutika ananunua kwa mchina. Mchina badala ya kumuungisha mama ntilie anakula kwa hotel ya mchina mwenzie.

Athari zake, mzawa hana wateja na mama ntilie hana wateja. Wote wanafilisika wakati wachina wananeemeka kutoka kwa wazawa
 
Na ndo maana hata matajiri wakubwa nchi hii wana asili ya kuwa wahindi na waarabu.
Kabisa kuna jamii mfano wahindi, waarabu au wayahudi na kwa Afrika kiasi Nigerians.. Huwa wanaishi kama network flani ya watu popote wawapo ugenini kwa hiyo si ajabu wakafanya kazi ama biashara ya kuuzia wengine, Ila pesa wanayoipata wanahakikisha inabaki kwenye circle yao.

Ndio maana popote utapozikuta hizi communities lazma wafanikiwe kwa sababu wanatumia selflessness ya jamii zingine kujiinua na kisha kutengeneza generational wealth
 
Kwako mlalamikaji wetu Mindyou

Mkuu huko juu nimeongelea suala la predatory pricing.

Wachina wana hiyo practise. Huko Marekani wana ile Ali Express, Temu na Shein ambazo zimekuwa zikilalamikiwa sana na Marekani kwamba zina lengo la kuua kampuni za kimarekani kama Amazon.

Hata India pia wanalalamika same thing.

Wachina wako tayari kula hasara au kutotengeneza faida hata kwa miaka 5 ili wateke soko, after that mtaisoma namba.
 
Kwanini tusiige mbinu zao?
 
Maek
Marketing strategy, kwanini na sisi tusiwe wabunifu, unadhani mtu kukubali kula hasara kwa muda mfupi Ili apate wateja wengi for future ni mchezo?
 
Nikuulize swali kwahiyo wewe unachotaka raia wa chini auziwe vitu gharama Kubwa na mbongo Ili wabongo wachache wafaidi wengi waumie

No what im saying is, suluhisho la Wafanyabiashara wazawa kuuza vitu bei ghali sio kuleta Wachina, kwa sababu hata Wachina wakishashika soko WATAONGEZA BEI.

Wamefanya hivyo India kwenye malighafi za madawa ya binadamu pamoja na Southeast Asia kwenye steel industry.

Wenyewe wana mipango ya muda mrefu.
 
Acheni upumbavu wa kuuza kwa bei ya juu kitu chenye bei dwelele mnapenda faida za juu nakwambia mimi nikikuta mchina anauza kwa bei dwelele na nunua hapo kama mmeshindwa kutuhurumia watanzania wenzenu mchina katuhurumia basi acheni nongwa kusave buku2 si haba asee
 
Hii nchi watu wenye mamalaka wanawaza madaraka tu na kujirimbikizia mali, Hakuna kiongozi yoyote wa nchi hii kwenye chama tawala mwenye uchungu na hii nchi wote wachumia tumbo na wabinafsi


Ukiona kwa namna wanavyoiba mali za nchi hii ni kama vile wanajiandaa na kitu fulani kwamba hii nchi kuna kipindi kitafika hali ya maisha itakua ngumu sana.
 
Jibu swali unataka raia wachache wawanyonye raia wengi na wao kufaidika Kwa kigezo Cha uraia wao Ili wananchi waumie sio wafanyabiashara waendelee kupata faida kubwakubwa Kwa kupandisha bidhaa ovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…