Picha: Nimepata msongo wa mawazo baada kuona katuni ya leo ya Masoud Kipanya akizungumzia sakata la Wachina

Raia wa TZ tupo katika wakati mgumu sana kwa kweli, kwanza kabisa mchina huwa na bei ya chini kwa sababu zifuatzo: -

1) Ana-control the whole chain of supply (good for them lakini anavunja rizki za watu hapo katikati)
2) Halipi kodi ipasavyo
3) Anakandamiza wafanyakazi wazawa katika maslahi na kuwatumikisha to the maximum (ikiwa unafanya kazi kwa mchina jiandae hata kwenda kazini siku ya Eid wiki ijayo 🙂 )
4) Technological advantage aliyonayo inayokuwa supported na funding from their Government/it's agencies wanapotaka kuwekeza Africa

Lazima tutambue wachina hawakuja kwetu kutusaidia, bali wamekuja kujisaidia wenyewe! Ikiwa sisi tutashindwa kulinda maslahi ya watu wetu basi ni sisi wenyewe ndo wakulaumiwa.
 
Mama muuza vitumbua hamtegemei muuza mcheke peke yake, na muuza mchele anunue kwa mchina kwa Tsh 1000 akauze mtaa mwingine kwa Tsh 1200
 
Hakuna cha shallow thinking, watanzania hatupendi ushindani kwenye nyanja yoyote ile.
Wewe unashindana vipi na mtu aliyekuzidi technojia na mtaji!!!!

Angalau pia basi angekuwa analipa kodi kwa usahihi utasema itaenda kununulia vifaa vya hospitali ukiumwa utibiwe, lakini hata hilo pia hafanyi! Athari ya kuwakumbatia wachina ni kubwa sana sio pale tu unapomuona ameshika yeye bali athari inaenda mpaka kwenye nyanja nyengine anazoziathiri indirectly.
 
Principal of Economic
 
Acha madalali wafundishwe jinsi ya kufanya biashara... Mbongo anataka kwenye mauzo ya siku 1 apate faida ya kwenda kufanya starehe na kuwatukana maskini 🤣🤣
nimesoma maoni ya wadau nilichogundua ni kwamba wanaolalamika wengi ni hao madalali wanaovuna faida mara mbili kabla ya ujio wa wachina so far watz wanapenda wabaki wao ili kuwakandamiza maskini wa hali ya chini ,imagine nguo inauzwa 15k lets say china ila kibongo bongo mtu anakuuzia 30k 😡😡😡 siamini kwamba hiyo faida ya 15k inaishia kwenye VAT yaan anaona jau kupata faida ya 5k so sad ......vua inyeshe tuone panapovuja
 
Kwanini mchina anauza Mchele bei Rahisi ameupata wapi huo Mchele?

Huo ni Mchele wa plastic umetengenezwa maabara
Mchele wa plastic ukapitaje bandarini? Kwahiyo wewe unakubali plastic inabandikwa jikoni inageuka wali kisha wewe unakula alafu tumbo lako linasaga plastic fresh tu bila shida sio? Hivi nani anawalisha haya mawazo huko vijiweni?
 
Bahati mbaya bidhaa wanazituuzia kwa bei ghali wanauziwa na wachina haohao ila ubaya umeanza baada ya wachina kuuza kwa kila mtu bei ileile anayowauzia madalali kitu kinachowapa stress madalali 😁
 
Umewah kwenda china mkuu au unaakisi mambo tu!
 
vichwa ngumu hawaoni kama hili ni tatizo halafu shilingi ikiyumba lawama kwa gavana na masisiemu
 
Bahati mbaya bidhaa wanazituuzia kwa bei ghali wanauziwa na wachina haohao ila ubaya umeanza baada ya wachina kuuza kwa kila mtu bei ileile anayowauzia madalali kitu kinachowapa stress madalali 😁
Thus why wamekuja na malalamiko kibao bila kujali maumivu wanayopata wananchi wenye hali duni ,ila wanajijali wao. Viva chinese ila hapo kwenye kukuza uchumi kuna madhara yanakuja kuletwa na wachina
 
Kampeni za kipuuzi, wafanyabiashara wakubwa km wale wa Kariakoo huwezi kuwaona kwenye hivyo vitumbua vyenu. Huo mfano hauendani na uhalisia, wachina hawauzi hivyo vitu, wao wanauza bidhaa zinazotoka kwenye viwanda vyao. Mchina anakuachia hela ya kutosha mfukoni utakayoitumia kufanya manunuzi mengine ikiwemo hivyo vitumbua. Masoud limeshakuwa bepari hawezi kuwa upande wa wananchi wanyonge.
 
uchambuzi wa hii katuni umenifanya nigundue watu humu n weupe sana kichwani
 
Unapata msongo wa mawazo kirahisi sana.
 
Serikali ipunguze kodi na tozo kibao kwa mkulima na mfanyabiashara ila mchele wa Kilosa au shinyanga umfikie mlaji kwa bei rahisi kama ya mchina.
Pia baadhi ya wafanyabiashara wapunguze tamaa ya kupata super profit.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…