Picha: Rais Samia Suluhu aongoza kikao cha Baraza la Mawaziri

Naona waziri Hussein Mwinyi yupo na PM na senior Lukuvi hapo.

Mama aliwahi kuendesha kikao hicho enzi za JPM na Hussein akiwa kakaa pembeni ya PM hivyo yani.

Asipokuwepo Raisi, Makamu, WM, basi kikao kitaendeshwa na Lukuvi, Hussein akiendelea kukaa hapo hapo sio?

Zanzibar inaongozwa na raisi au waziri wa serikali ya JMT? Kikao hicho kinazungumzia mambo ya Muungano tu au hata na yale yasio ya muungano?

Kwanini kwenye bunge la JMT, ZNZ ingekuwa inawakilishwa na spika wa baraza lao pengine na makamu wa huko kwao?

Kwanin kwenye bunge la JMT kusingekuwa na session ya kujadili mambo ya muungano ambapo wawakilishi wa Znz wanakuwepo, session ikiisha wajikatae?

Hata sielewi, ndo mnasema tunatakiwa kupata Katiba nyingine ili niweze kuelewa?
 
Daah! Mkuu una uchungu hatari. Tatizo katiba mbovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…