Picha: Said Othman Mangwelele a.k.a mchawi wa drafti wa muda wote

Picha: Said Othman Mangwelele a.k.a mchawi wa drafti wa muda wote

Siku hizi amekuwa msafi na amenepa! Kipindi Cha nyuma jamaa alikuwa halii Chakula wala kuoga, kutwa yupo kwenye vijiwe vya goda mji mzima akicheza kamari.
Anyway alinipa michezo mitatu nitoe draw moja...sikutoboa akala elfu tano yangu
 
Aisee
 
Kuna jamaa anajiita Mwita au Nyamongo huyu ni hatari
Kwa Tanzania anasema yeye ndiye bingwa wa French lakini ata hili draft la kawaida anacheza
Akicheza na Sisco sidhani kama Sisco anaweza kumfunga
Huyo wa french ntacheza nae
Si yupo online !
 
Kama ulishawahi kutazama game zake either physically au online bila shaka utakiri huyu jamaa ni mchawi kama sio jini kabisa.

Jamaa anakufunga anavyotaka yeye, yani kuna ile game unaona kabisa imeisha ila jamaa hataki kumaliza ,atataka akufunge ki ladha kiasi kwamba hata wewe unayefungwa utafurahi goli utakalo fungwa.

Mwanafunzi wake anayekuja kwa kasi kwa sasa ni dogo Shukuru.View attachment 3396277
Lakini kwa sasa kuna ujio wa dogo Sisco, huyu kijana anasumbua sana, sidhani kama kuna bingwa yeyote hapa TZ atatoboa kwa huyu dogo .

Labda kama mkongwe Mangwelele angeamua kurudi kwenye michezo kumnyamazisha huyu kijana. Nina uhakika donge nono lingewekwa kati yao na si ajabu Sisco angeushangaza ulimwengu.

Thread yako inachanganya, umezungumzia watu wawili ambao infact mmoja bado mchezaji (Dogo Sisco) na mwingine mstaafu (Mangwelele) Nia ilikuwa kumpa credit Mangwelele....good.
sasa kusema Dogo Sisco ni mchezaji anaekuja vzur kwa sasa ni kulikosea heshima drafts, tuweke sawa hapa,,Sisco ndio sura ya drafts Tanzania. Na kutamani kuona mechi ya ushindani na Mangwelele huku ukitamka labda ndie mwenye nafasi ya kumzuia Sisco, ni ngumu sababu mmoja alistaafu na sasa ni mkufunzi unajua hili bila shaka au la umeamua tu kudanganya halaiki . Period.
 
Kuna jamaa anajiita Mwita au Nyamongo huyu ni hatari
Kwa Tanzania anasema yeye ndiye bingwa wa French lakini ata hili draft la kawaida anacheza
Akicheza na Sisco sidhani kama Sisco anaweza kumfunga
Mwita ni mchezaji mzuri wa french.....lakini sio namba moja Tanzania, kwa hiyo hiyo french yake kule Kanda ya ziwa Kuna miamba kumzidi yeye akina kasikio etc...

Kwa British...asikudanganye mtu Sisco, huyo mwita hana uwezo wa kupata sare tu....kwanza hata mwita mwenyewe hawez kubali kucheza na Sisco....
 
Hongera zake.Ila hujasema ameshindana mara ngapi na wapi mpaka kujiridhisha kwamba yeye siyo Mwamba.Usijekuta kule Utete kuna Mwamba ila bado hatujajua tu.
 
Back
Top Bottom