Picha: Said Othman Mangwelele a.k.a mchawi wa drafti wa muda wote

Kuna jamaa anajiita Mwita au Nyamongo huyu ni hatari
Kwa Tanzania anasema yeye ndiye bingwa wa French lakini ata hili draft la kawaida anacheza
Akicheza na Sisco sidhani kama Sisco anaweza kumfunga
Ushawahi sikia habari za kasikio?
 
Mwita anapatikana wapi?
 
Sio chai mkuu, ni kweli tupu, one day nilishuhudia mmoja wa matulatula toka Manyanya akicheza draft, hawa jamaa noma sana, yani wamekariri madrafti, wamekariri kila kete kwa zile za mbele zote, ukiaanza tu washajua waanze na kete gani wakufunge na wana majina ya game kwa kila kete utakayoanza, shida kidogo kwao ni wao wakianza kucheza draft ukipambana unaweza kupapatua japo droo! Hawa jamaa hawafungiki ni kama wachawi flani. Ukicheza nao ushindi wako ni droo tu, unapigwa tano bila labda na droo moja au mbili!!

Wana madrafti kwenye cm zao jinsi ya kucheza kila kete ya mbele hadi mwisho!! Wanatumiana wao kwa wao au wakiona unajua wanakuingiza kwenye genge lao.

Ukicheza nae ukatoa droo analipanga draft upya mbele yenu na kucheza yeye peke yake pande zote mbili yako na yake kuanzia mlipoanza na hadi ajue alipokosea ukachomoka, akishindwa kujua alipokosea anapeleka huo mchezo kwa matulatula wenzake kina Mangwelele , Issa Mamba, Sisco na yuko mwingine sijui tula Noeli huko Manyanya yaani ukitoa droo inageuka vita kubwa kwao.
 
Tula ni mtu asiye jua drafti.

Hao uliowataja wote mabingwa.

Huyo mwingine anaitwa Noel Alex Namaloe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…