Elections 2015 Picha: Tulichokishuhudia katika mapokezi ya Magufuli Jijini Mwanza, upinzani unafutika

Elections 2015 Picha: Tulichokishuhudia katika mapokezi ya Magufuli Jijini Mwanza, upinzani unafutika

Kweli ccm ina njaa ya watu.

Hawa ndio watu wa kuandika mtandaoni eti upinzani unafutika!.

Hawa ni wanachama wa ccm, tena ni wachache sana maskini kama ningelikuwa mimi ningepotezea.

Jifunzeni kwa CHADEMA. Mbunge wa CHaDEMA akikohoa tu, umati a watu wanakosa hata pa kuweka miguu.

Mbona huyu raisi wenu watu wachche sana tena nyumbani kwake? Kwingine hali niaje?

Hapa kuna tatizo tena kubwa!.


Maskini mama magufli mwalimu wa watu hata kupunga mkono hajui!. Hawajafundisha wanamwacha aabike mbele kwa mbele. Anapunga mkono kama anafukuza kuku kwenye ulezi!.

Poleni ccm.

Watanzania tuliwaamini, mafisadi wakawapenda lakini shetani kawapenda zaidi.
 
Nilifikiri kwa Mwanza na ukichukulia kuwa huyu mteule ni wa kanda ya ziwa tulitarajia zaidi ya hapa; Kirumba (au hata furahisha) ingetapika! Mbona hamkwenda huko mkaidhia pale ofisi ya ccm ambapo ni pafinye sana?
 
Propaganda kazini. Naona alinajisimamisha tu ili aonekane, kunachamaana alichosimamishiwa huko kote?
 
...ccm ata malaika akipewa nafasi, mfumo uliopo utampoteza tu kusiasa...tubadiri chama tupate mwelekeo mpya na mtazamo mwingine zaid. Kenya wameweza na wanapga atua mbele. Juz tu wametoka ktk moja ya nchi maskini dunian na kua nchi ya uchumi wa kati
 
Mimi so mwanasisa ila mleta Mada umechemka Mimi naishi Mwanza huo unaosemq umati uliuona peke yako au hujui maana ya umati kuwa Fair embu weka picha za majuzi WENJE an anaenda kuchukua form ulinganishe nazajana ndio utuambie UPI umati kati yamgombea urais name mgombea ubunge
jipime mwenyewe
 
Lowasa mwenyewe kapasuka atawezaje kupasua chama kwanza tunataka aanze kulipa kodi na zile biashara zake haramu tunaanza kudili naye atakufa mapema sana.
Kuli yako karne hii haikisaidii chama. Kwa hiyo kodi inalipwa kwa visasi, maana yakeni kuwa walioko ndani ya chama hawawajibiki kulipa kodi?
 
MwanaDiwani endelea kuota ukishtuka utakutana na anayeapishwa! Ndo utajua huo umati au umauti wa CCM!
 
Last edited by a moderator:
Ha ha ha ha ha kweli misemo ya wahenga inaaplication nyakati hizi.....mfa maji haachi kutapatapa...naona mamia waliompokea kweli kama sio makumi....ha ha ha huo kwako umeona ni mwanzo mzuri na hata hujalinganisha na mapokezi yoyote ya chadema mkoani hapo...this is unrealistic mjomba.penye wengi pana mengi wengi wanaonesha kupunga kumjua tuu john watoto nao wanaongeza idadi ya mapokezi kweli nimeona je wana impact yoyote..? Hapa ndipo sasa tuanze kuelewa kauli ya mmoja wa hao waliopokelewa ...tutashinda hata kwa goli la mkono..hawakukosea walipo sema kisebusebu na kiroho papo sababu najua inakuuma sana kama ni mwanachama hai wa green kwa mashua hii inayo pigwa na mawimbi mazito ingali hata safar haijaanza utamwaminisha mtu ilizama iliwa ukingoni kwa lipi tafuta kauli itakayoonyesha ilianza safari ikakumbwa na mawimbi mazito ikazama..kadhalika ccm mtawaeleza vip kimepotea mwanzo hata hatua bado wadanganyeni kwanza kua hatua ni nzuri sana ili baadae wawe na lakusema..mtamkumbuka sana bwana lowassa na niwwaambie tuu ndugu mavi ya kale hayanuki ila unamoyo wakuyabeba kwa mkono ilihali wajua ni mavi..hasa kama yamenyeshewa na mvua.nawaombea kila laheri wote wenye moyo katika harakati za kuudangaanya umma na kufunika uhalisia hasa kwa wale wasioweza pambanua na kujua kweli mbalamwezi yaweza waka vp mchana ili hali tunaambiwa mchana ni usiku sasa.
 
Unaposema sasa chama kinarudi kwa wafanyakazi na wakulima una maana gani?Kwani chama kilikuwa kwa akina nani?
 
Mbona hako kaymati hakafikii Hata kale alikojaza silinde juzi kati hapo tunduma,ccm imeshakufa jamani
 
ninachofahamu ni watu walifika kwa mwito wa serekali ni maafisa wa serekali na wanafunzi walioombwa kuvaa kiraia
 
Kweli Mbowe kiboko-Leo ndi nimejua umuhimu wa red-brigade. hawa wenzetu wana ulinzi wa dola wengine inabidi kujitegemea ki dhati kabisa
 
ni kweli rais ni magufuli ila kwa wabunge bado sana
 
Ccm imempa kazi sana huyu jamaa, aendelee tu atakapofia hapohapo maanake huo umati huku MWZ yetu huwaga ni wa diwani viwanja vya furahisha.
 
Chuki ziyawamaliza

Ha ha ha! Mkuu MOTOCHINI mambo vipi? Nadhani angekuwa ni yule "mkuu" wa "wakuu" mambo yangekuwa tofauti hapo. Hivi na yeye alienda Ujeremani? Maana si msikii sikii tena.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom