Hii inatokea kwenye nchi ya kusadikika afrika tu (dubai, south afrika, labda kongo kwa utajiri tukonazo sawa tu kwanini zimendelea kuliko sisi? shida ni viongozi wasiokuwa wazalendo, na wabinafsi yaani pesa wanaiba ndani wanahifadhi uswisi, ni afrika pekee utaona hii, mzungu hawezi kuchota ulaya pesa ahifadhie afrika matumizi ya akili tu waafrika si hatuna), nchi zilizostaarabika huwezi kuta aliyeshikilia mpini akifanya mauaji ya wanaonyonywa kwa kodi wakidai haki zao, maswali ni mengi kuliko majibu, je huyu mfalme juha yuko pale kwa maslahi ya wananchi? kweli yaani analazimasha kubakia ili awaletee maendeleo?:
Sasa tufanyeje:
1. watawala wa aina hii tuwakatae, tusiwaheshimu hata kwa kutumia akaunti feki, tuwazomee wakitoa hutuba, wasipate amani kabisa kwenye utawala wao, watawala wasioheshimu maisha ya wengine.
2. Swali la msingi(mengine yote yanajibika) linabaki kwa hawa waliotuua? Hawa wanaotupa hukumu isiyolingana na kosa, thamani ya sheli au mwendokasi hailingani na uhai wa mtu mmoja abadani na tuheshimiane tusilinganishe uhai na vitu vya hovyo, dharau hizo! Tupunguze unyonge mapolisi tunaishi nao tuwasalimie