Mlima simba
JF-Expert Member
- Dec 28, 2017
- 3,856
- 7,059
Nadhani Sisi sote tupo salama wakuu, bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada.
Mnamo tarehe 18.03.2025 majira ya Saa nne usiku wakati narudi Kutoka mihangaikoni nikashuka kituoni kwangu Kibaha picha ya ndege.
Kutoka picha ya ndege mpaka ninapokaa Pana umbali kidogo kwa hiyo kwa usiku huo lazima nichukue piki piki au bodaboda.
Baada ya kuanza safari na Yule boda boda ndipo akanza kunisimulia kuwa limepita gari la matangazo likitangaza kuwa biashara mwisho Saa sita usiku baada ya muda huo kitakachompata yeyote asilaumu.
Uwe boda boda , uwe muuza Duka uwe mama ntilie uwe muuza chipsi hutakiwi kukutwa baada ya Saa sita usiku.
Swali linakuja je Sisi tunaorudi kuanzia Saa sita tunafika vipi makwetu? Kwa maana tukishuka picha ya ndege tunapanda Bodaboda mpaka kufika huko tunapokaa sasa wanavyozuia watu wasifanye kazi kuanzia Saa sita usiku na kuendelea wanatumia sheria ipi ya nchi?
Kuna BODA BODA wao huwa wanaanza kazi usiku mpaka asubuhi hawaoni wanawanyima fulsa ya kujitafutia kipato kwa njia ya halali?
Lakini pale picha ya ndege ni kama Buguruni Vile hata ushuke Saa Saba usiku unapata mahitaji ila sasa imekuja amri ikifika Saa sita kamili kila kitu kiwe kimefungwa je huu ni utaratibu wa Aina gani?
Nawasilisha .