Picha ya Rais: RC Makonda amtaka Msanii Idris Sultan kujisalimisha kituo cha Polisi

Picha ya Rais: RC Makonda amtaka Msanii Idris Sultan kujisalimisha kituo cha Polisi

Tatizo shule , yule Bwana Mdogo yeye ufikiri yupo juu ya sheria kwa matamko yake ya Kipopoma.

Laana ya Kumpiga Mzee Warioba, inamsumbua vibaya sana.
 
ukiacha maudhui lengwa

naona ajabu sana pale Popomaz anapomshauri Popoma,maana tabia zenu zinafanana..

awali nilidhani Popomaz wa JF ndiye Bashite...lakini kwa huu Uzi siyo

sema mnashea matabia ya kujimwambafy kizamani ZAMANI
 
Wewe Jamaa nimekusema, nimekushauri na hadi nikakuambia ya kwamba kati ya Watu ambao mmechangia tena kwa 75% kufanya Utawala huu wa Awamu ya Tano Kuchukiwa, Rais nae Kuchukiwa na hata Chama chetu cha CCM nacho Kuchukiwa au Kudhihakiwa basi ni Wewe Paul C. Makonda na nasikitika kwamba pamoja ya kwamba unajifanya Mjanja na Mtoto wa Mjini hili bado hujalijua.

Kwa ‘ Upuuzi ‘ wako wa ‘ Kimaamuzi ‘ ambao kila mara huwa unaratibiwa kwa Kupenda Kwako ‘ Kukurupuka ‘ huku ukitaka ‘ Publicity ‘ na pia Boss wako Mheshimiwa Rais azidi Kukuona bora kati ya Watanzania Kitendo ulichokifanya jana natamani sana utembelee Mitandao mbalimbali ya Wakenya na Waganda achilia mbali ile ya Afrika Kusini uone jinsi ‘ Ulivyochambwa, Kutukanwa na Kudhihakiwa ‘ huko huku ukitufanya Watanzania wote tuonekane ni ‘ Mapopoma ‘ wakati kumbe ‘ Popoma ‘ ni Wewe peke yako hata ‘ Malaika ‘ wa Mbinguni nao wanalijua hili.

Sitaki leo niseme mengi hapa ila nadhani kama kuna Mtu ( Msanii ) ambaye kwa ‘ Uwasilishaji ‘ wake ambao amekuwa akiufanya kwa Marais ( ambao wanatajwa kuwa ni Wakali na Madikteta ) katika Ukanda wetu basi angekuwa ni Bwana Godfrey Mwampembwa ( wengi mnaosoma Gazeti la The East African mnajua kwa Jina lake la Kazi la GADO ) achilia mbali Msanii wetu mwingine wa Uchoraji hapa Tanzania Masuod Kipanya.

Sanaa ni jambo pana mno na ndiyo maana kuna Kozi ‘ Maalum ‘ ya hiyo Fani hivyo kwa Sisi wengine ambao huwa ‘ tunawashawashawa ‘ tu kwa ‘ Upopoma ‘ Wetu ni vyema kama hatujui aina ya Ufanyaji Kazi wao basi tukawa tunajiridhisha Kwanza. Hivi alichokifanya huyo Msanii aliyeambiwa akaripoti Polisi kina tofauti gani ya Kimantiki na kile anachokifanya huyo Gado na Kipanya ambao wao wanafanya katika Magazeti na huyu anafanya kupitia Mitandao?

Nilienda mbele kutaka Kujiridhisha zaidi hasa kwa hawa Marais ( Wababe / Madikteta ) ambao mara kwa mara huyu GADO amekuwa akiwachora huku muda mwingi akiwa anatoa Uwasilishaji wake wa Kuwasema ambapo kuna muda Picha zake zingine unaweza kusema anaweza akakamatwa na hata Kuuwawa na kugundua ya kwamba hao Marais wote walishanukuliwa wakisema kuwa hawana shida na GADO kwani hata wao kuna muda wanahitaji Kucheka au hata kusemwa ili waweze kujua mapungufu yao hali ambayo imefanya hata wao wamkubali GADO na tena wanamuheshimu kuliko inavyodhaniwa.

RC Makonda nakusema hivi mara kwa mara kwakuwa Wewe ni mwana CCM mwenzangu hivyo nakuomba badilika Ndugu kwani kama ni Kujipendekeza kwa Rais JPM sasa umevuka mipaka. Yawezekana ukawa umejuana na Rais JPM hivi alivyokuwa Rais wetu wa JMT ila kwa kukusaidia tu ni kwamba kama kuna Rais ambaye anapenda Utani na Kujichanganya ( ukiondoa Jakaya Kikwete ) basi ni Boss wako sasa Rais JPM na nina uhakika hata kilichofanywa na huyo Msanii wala JPM hajakasirishwa nacho isipokuwa ni Wewe sasa ndiyo unataka Kumlazimisha Rais JPM abadilike, akasirike na awe na Roho mbaya ( Kisununu ) na Unafiki kama wako.

Ona sasa huu ‘ Upuuzi ‘ wako kwa huyo Msanii wa Vichekesho ( Comedian ) umesababisha hadi Watu wengine kuja na za ‘ chini chini ‘ kwamba ulikuwa unamchukia huyo Kijana ambaye ni ‘ Sukari ya Warembo / Mtanashati / BaruBaru ‘ kwakuwa kuna ‘ Demu ‘ umepoteza muda unamtaka ila ‘ Kakutosa ‘ lakini ‘ Dogo ‘ anajipigia zake tu na kwamba kumbe ulikuwa unamuwinda ili upate sababu ya ‘ Kumkomoa ‘ ili umalizie hasira zako za Kukosa ‘ Mbunye ‘ uliyokuwa ukiitamani na unaila kwa Macho tu sasa.

Halafu ni kwanini Wewe unapenda Kujifanya ndiyo IGP au DPP wa nchi hii? Na kama unazipenda mno Kazi za Msemaji wa Serikali aliyonayo Dkt. Abbas au ile ya Msemaji wa Ikulu Gerson ili uwe ‘ Mtetezi ‘ mzuri wa Mheshimiwa Rais basi usimwombe tu huyo Boss wako akupe hivyo Vyeo na ikiwezekana basi akupe na hata vile vya Uwaziri Mkuu au kile cha Umakamu wa Rais lakini hata ikiwezekana basi awe anakupa na ‘ Deiwaka ‘ ya kuwa Rais wa Tanzania ili uridhike kwani hivi ndivyo unavyotaka ili uweze ‘ Kuwatisha ‘ vyema Watanzania ili ‘ wakuogope ‘ na uweze ‘ Kujitajirisha ‘ zaidi kupitia ‘ Uwoga ‘ wao Kwako kama ambavyo ilivyo sasa.

Na Wewe Rais wangu mpendwa kabisa Dkt. Magufuli, Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru na wana CCM wote hasa wale ‘ Waandamizi ‘ kabisa endeleeni tu ‘ Kumlea ‘ na ‘ Kumdekeza ‘ huyu Kijana wenu ila Mimi GENTAMYCINE namalizia kwa kuwaambieni tena kuwa kama kuna Mtu ambaye amechangia na anachangia kila Siku Rais JPM Watu wamchukie, wamuone mbaya, waichukie hii Serikali yake na hadi Chama chetu cha CCM basi ni huyu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul C. Makonda. Endeleeni ‘ Kutudharau ‘ akina ‘ sie ‘ na kudhani kuwa kila tunapomsema hapa basi tuna Chuki au Wivu nae ila huenda kuna Siku mtatukumbuka na kutuheshimu. Na yawezekana wengine tukawa na umuhimu mkubwa Kwenu kuliko hata huyu Kijana ambaye Kutwa anakuja tu na Vituko na ‘ Ukurupukaji ‘ wake.

Makonda una tatizo gani kwanini husikii na hutaki kubadilika Ndugu?
Very well said..
Shida kuna watu wengine wajinga-wajinga kama W. J. Malecela jana wanaandika na kuonyesha kwamba hakuna kosa lolote alilofanya Bashite..na kwamba Idris amefanya makosa..hawa ndio wanampa kichwa.
 
Idrisa bana yaani natania hadi baba wa wenyewe? Haya sasa kazi unayo..
 
Chachu Ombara,


Kwa mantiki ya kawaida tu, binafsi sioni huyo msanii kafanya kosa lolote. Ikiwa kweli anapelekwa polisi kwa "kosa lolote la jinai" in respect of that cartoon, basi mpira utabaki kwa polisi husika kuona jinai hiyo. Binafsi SIIONI. Huyu msanii anataka Rais wetu apate muda kama raia wa kawaida ILI AFURAHIE BD YAKE. KOSA LIKO WAPI? Kwa upande mwinigne, labda RC anataka kumzawadia huyo msanii kwa ubunifu na upendo kwa Rais wetu. TUSUBIRI TUONE.
 
2198206_Idris.png
 
Masoudi hamchori Rais wewe
Magufuli hayupo vile,ukimpeleka mahakamani utashindwa tu kesi
Huyo msanii hakumchora Rais,ame distort muonekano wa Rais hata wewe unajua kwamba ile sura ni ya rais halafu huku chini amemvika vi mtikila
Ushamba mzigo
 
Alien pilot, Wacha uongo Trump maagizo kibao anayatolea twitter.

Haya wacha hiyo U.S.

Msanii wenu Menina ameitwa BASATA kupitia instagram na ameenda.
Aliyetoa maagizo ya Idris aende kituo cha Polisi ni mtu anaejulikana kwa jina la Baba Keagan. Sio Mkuu wa mkoa Paul Makonda. Hata ningekuwa mimi nisingejisumbua kwenda. Huo ujumbe toka BASATA ulitoka kwa mtu asiyetumia jina kama hili la Baba fulani.
 
Back
Top Bottom