hiyo nyama aliyokamatwa nayo thamani yake ni 900,000, kwanini tusichangishe mchango ili tulipe faini atoke? manake kwa upande mwengine hizo sheria tumezitunga wenyewe, na yeye sio kwamba hafahamu kwamba wanyamapori ni msala. sisi tuliozaliwa maporini tunajua tangu utoto wetu nyamapori ilitungiwa hadi jina kwasababu serikali ikikukuta nayo ni msala, hivyo ukikutwa nayo hata kama una njaa ni msala kwasababu sheria inafuata mkondo, haiangalii tajiri wala masikini. cha muhimu hapo ni aidha kuifuta hiyo sheria ili tuvamie tule swala wote, au la tumchangie huyo mama alipe faini kwasababu kosa aliloshitakiwa nalo lina option ya faini, hata kama ameenda gerezani tukienda kulipa faini anatoka hata kesho.