Uzuri mnaoponda hapa hamtafika hata 50. Ni walewale wa 5 mnapost na kujijibu uzi unafika kurasa 10.
Mnataka Serikali inunue kimyakimya halafu zipotee kimyakimya baadae. Sasa hivi ni uwazi kila mtu aone ili baadae ahoji.
Ndiyo maana watu wengi hawakujua kuwa Tz ilikuwa na ndege kipindi cha nyuma mpaka Magu alipowaeleza. Na kitu kingine serikali lazima iwaambie wananchi wake kuhusu mafanikio yao ili wawe na kujivunia nchi yao.
Kingine, kwa sasa hatuzungumzii picha za ndege za kipindi cha Baba wa Taifa. Mambo ya kuzungumzia picha bila ndege yalikuwa awamu ya 4 na 3, sasa hivi tunazungumzia ndege halisi 11 za AirTz.