Picha zinatisha: Ni picha za Wamasai waliojeruhiwa na wengine damu zinavuja

Wamasai wasiwe wabishi, wameshatengewa eneo la kuhamia shida nn? Wanyama hawawezi

Wamejeruhiwa tuu? Wanabahati sana. Wazanzibari huwa wanauliwa, wanapewa vilema, wana najisiwa, kila uchaguzi lakini hampigi kelele. Mnaona damu za Wazanzibari kumwagwa ni jambo la kawaida.
Kwa hiyo hapo ni programme ya kulipa kisasi? Kweli wewe ni dooogi.
 
Wote mnatetea huu upuuzi ni "MBWA" ukikasirika njoo unipige nimekaa pale binadamu gani nyie msokua na huruma kwa wenzenu eti ooh wamejeruhiwa tu. kwa hiyo kujeruhiwa ni raha au njoo tukujeruhi wewe ujue uchungu wake. mambo kama haya mnapaswa kuhurumia wenzenu na kuombea yaishe salama sio kuwadhihaki namna hii.
 
Nilisema mapema mno, Masai huwezi kuzugumza nae na kuelewana, nilipendekeza wahamishwe kwa nguvu, sbb ardhi si mali ya Masai, hakuna mwenye hati miliki ya ardhi ikiwa serikali inataka ardhi hiyo. Hivyo hapa nimeona wanaharakati na NGOs kibao ambazo huwaingizia fedha kwa njia ya kuwapiga picha na video masai kibao na kutumia kama njia ya kupata dollars kwa kusema ni maskini sana na serikali imeshindwa kuwahudumia.

Njia iliyo nzuri, serikali ishafanya juhudi kubwa kufanya nao mazungumzo kupitia Waziri Mkuu mara nyingi sana, hata sitaki kuhesabu, nadhani kuwapatia maeneo mengine ndio jibu, na serikali imetoa maeneo mengi tu, ila masai wengi wanatumiwa na hao wanaharakati, hivyo kuwatoa kwa nguvu ni sawa.
 
BAVICHA wako kimya huko wanapewa cha kusema sahizi ili kesho wafufuke tena

Sent from my VTR-L29 using JamiiForums mobile app
 
Si mlisema Magufuli ni katili anaua watu, haya sasa huyu mama yenu hiki kinachofanywa na vijana wake kwa amri yake ni nini?
 
Napenda amani, lakini hawa wametuulia sana ndugu zetu wakulima kinyama na kishenzi kabisa kule morogoro.
Tatizo wamasai nao wanadekezwa mno. Huko Ngorongoro wanafaidika mno na hiyo mamlaka ya hifadhi ndo maana bila aibu kuna wengine wamejenga mahekalu ndani ya hifadhi wakati serikali yenyewe imewajengea wafanyakazi wake nje ya hifadhi wilayani Karatu. Ifike sehemu wamasai nao waelewe serikali ikiamua ubabe watahamishwa kwa nguvu. Wananchi wengine huwa hawasumbui sana kwenye kuhama. Fidia tu zinalipwa watu wanahama.
 
Hii ni vita ya uchumi.hao woooote ni wakenya wasio tutakia mema Tanzania.
Ni lazima tuwashugulikie tu akuna namna
 
Unakubali kuhama kwa hiari kabisa,serikal inatumia kod za wananchi kuwaandalia makazi yaliyo bora kabisa,wakati wa kuhama unafika unagoma unashika na sime,ungekua wewe u ngefanyaje?
Ukijibiwa hapa Chinga naomba nitag
 
Hakuna mwananchi asiyejua haki yake kwa sasa hasa ile haki ya uhuru wa kuishi popote ambayo ni haki ya msingi ya mtanzania. Wamasai ni watu wanaojitambua sana shida yetu ni kuwa ukisimama katika haki yako serikali ya CCM inakutumieni FFU wawapige kama hivyo na kutumia silaha za moto hata kuwaua kabisa bila kujali.

Na huo ndio umekuwa mtaji wa watawala miaka nenda miaka rudi. Hutapewa ruhusa ya kuandamana kupinga udhalimu kama katiba inavyotoa haki hio.

Serikali inatamba ina jeshi na inalitumia kugandamiza haki za raia wanyonge kinyume kabisa na dhamira ya uwepo wa polisi wa kulinda haki na mali za raia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…