Picha zinatisha: Ni picha za Wamasai waliojeruhiwa na wengine damu zinavuja

Picha zinatisha: Ni picha za Wamasai waliojeruhiwa na wengine damu zinavuja

Serikali na Taifa lina haki ya kulinda rasilimali zake. Sasa kama hawataki kutii mamlaka halali lazma hazina ya Taifa Ngorongoro ilindwe kwa gharama yoyote. Ngorongoro na Loliondo Sio mali ya Wamasai wengi ni wahamiaji na wavamizi tuu waondoke mara moja. Vinginevyo watachakaa.
nafikiri sii vema sama kutoa kauli ambayo hujaifanyia utafiti wa Kutosha, usemacho kina walakini. Wamaasai ni wananchi ambao wanapaswa walidwe kwa mujibu wa katiba. Dialoge hutumika kutekeleza hata miradi vijijini kwa kutafuta wananchi kuunga mkono. Je philosophy tumeipeleka wapi? Eti kuna watu ambao sii wamasai hao ndio watolewe ila wenye ardhi yao wakubaliena nao sii kutumia nguvu. Kumekuwa na kauli tata nyingi kuhusu hili na sii lam leo karibu awamu zote tangu Ali Hassan Mwingi,marais waliofuata walipiga danadana hadi Rais wa sasa. Ananguvu nyingi. Naamini kabisa hili linaweza kutatulika kwa kufikia win win situation.
 
Jili la kuhamisha Wamaasai mbona naliona linafanywa kwa haraka nyingi? Shinikizo linatoka wapi? Linaweza kufanikiwa iwapo busara ikitumika na sii kwa zimamoto, slowly slowly, elimu, influency, na kuandaa wanakopelekwa kikamilifu ili watu waone faida zake kuhama sii kwa namna hii hata kidogo. Naona kuna shinikizo mahala, tunaiomba serikali yetu iwe na umakini hasa wanapodeal na watu amboo ndio waliowapa madaraka wanayotumia kwa sasa. Ndivyo katiba yetu inavyosema. Inapokuja kitu chochote against watu ni shida kitu hicho hakiwezi kushinda wananchi (Wamaasai ni wananchi sio wanyama) Tufuate katiba katika kulitatua hili, sitaki kuamini ni Mwana Mfalme wa Uarabuni tena sii mwananchi anuwezo wakuishinikiza nchi hadi serikali isahau wajibu wake. Chonde chonde serikali yetu turudi kwenye Katiba/ Mwananchi ni supreme before anything.
 
Back
Top Bottom