Hatuwezi "kuachana na hilo la 'wanaenda kupewa waarabu'" (in fact hata wawe wahindi, wachina, wazungu); hili ndilo swala la msingi kama kweli lipo.
Hatuwezi leo hii kuwaumiza wananchi wetu kwa sababu tu ya kuwafaidisha wageni, eti kwa sababu za uwekezaji. Ingekuwa hivyo, pasingekuwepo na sababu yetu kudai uhuru wetu ili tujiamlie mambo yetu yanayotufaa sisi wenyewe.
Kwa hiyo nasema tena, kama kuna uhusiano wowote wa kuwahamisha kwa mizengwe ndugu zetu wa kimasaai ili eneo apewe mwekezaji, nami nitaunga juhudi za mapambano kudai uhuru kutokana na huu ukoloni mpya unaokuja kwa mlango wa "uwekezaji."
Tanzania haina upungufu wa sehemu za uwekezaji, na in fact, uwekezaji siyo kipaumbele cha maendeleo yetu; maendeleo yetu ni sisi wenyewe. Viongozi wanakosa sifa za uongozi wanapodhani kuendelea kwetu kunaletwa na hao watu wanaokuja kununua utu wetu hapa na kutufanya kama wageni ndani ya nchi yetu.
Umeweka mifano ya maeneo yaliyochukuliwa na serikali na ukaitaja Bagamoyo kana kwamba watu waliondolewa bila stahiki zao?