Picha zinatisha: Ni picha za Wamasai waliojeruhiwa na wengine damu zinavuja

Picha zinatisha: Ni picha za Wamasai waliojeruhiwa na wengine damu zinavuja

Tushajifunza, huo ujinga wa kuchagua taipu ya yule mjinga hatufanyi tenaa,
Mama bado yupo sanaa na katiba tutaichezea akae madarakani adi kifo mwendazake ametupa funzo sana, nchi iliingia kwenye historia ya kuongozwa na kichaa wakati wenye akili timamu tupo
Kwan Jah si yupo? Chezeen hiyo katiba, yeye atafanya yake.
 
Lazima umfuate Beberu anachotaka ukikaidi ndo km hivi!! yeye atatoa risasi na hela zako na zile za kuwalipa askari wako weye andaa watu tu na utawale milele anae kuletea fyooo tuambie sisi!

hizo mbuga na akili ya kuzihifadhi tulianza sisi kuweka hizo sheria bila sisi hao wanyama wasinge kuwepo!! hakuna aliye juu ya utaratibu wetu!.....sisi ndo tumeweka misingi ya kitaifa chenu iko..

.kwetu kalikuwa na bado ni ka Tanganyika teritorry hatutaki mijadala na maskini! sisi ndo sisi letu ni moja japo mtalia sana lkn fuateni yetu muwe salama! km mmechoka na maisha tuliyowapa bure Bisheni nasi muone!

kamwe mtalaumiana mpaka kiama!!! kiongozi km hutaki lawama ajili yetu ng'oka mwenyewe kabla hautakuja hapo! tunawataka wana JF na wengine wenye kiherere here! wafunge midomo!

tunaweza kuwadaka mmoja baada ya mwingine!! mnao tuchapisha humu!! tunawaona sana kuliko mnavo dhania hata wengine bila aibu wala kujua kuwa tunawaona mnakuwaga uchi! tutawapoteza!!
 
zile siyo risasi basi aidha ni mwehu au huna akili.
Mwehu na huna slili mwenyewe sasa unalazimisha niamini story isiyo na video? Leta video ikionesha wakipigwa risasi na si majeraha ya mikato ya mapanga na mikuki
 
Salaam Wakuu,

Kuna picha zinazoonesha Wananchi wa Tanzania Jamii ya Wamasai wakiwa na majeraha. Haijajulikana picha zimepigwa wapi saa ngapi.

Naamini Vyombo vya Usalama vitatolea ufafanuzi ili kuondoa taharuki katika Jamii.

MY TAKE:
Damu ya Mtu haiendi bure.

Pia soma:

Wamasai Ngorongoro: Spika ataka 'aliyechukua clip' ashughulikiwe, taasisi zilizosajiliwa nchini kufata

Bungeni: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa asema hakuna mgogoro kati ya Wafugaji na Serikali Loliondo

WANANCHI WALIOJERUHIWA NA POLISI KATIKA KIJIJI CHA OLOLOSKWAN KWA RISASI TAREHE 10 JUNI 2022

1 Ngormoj Masago Mwanamke Amepigwa risasi Mguuni na chini ya Tumbo
2 Partalala Parmwat Mwanaume Amevunjwa Mguu
3 Koote Kaura Mwanaume Amevunjwa Mguu
4 Sereman Lukeine Mwanaume Amevunjwa Mkono
5 Kiteleshon Masago Mwanamke Begani
6 Olengiyo Mwanaume Amevunjwa Mguu
7 Njipai Nginai Mwanaumke Amevunjwa mguu
8 Mtoto wa Denis Reya Mwanaume Amevunjwa mguu
9 Orkiliyai Saingeu Mwanamke Amevunjwa Mkono
10 Olesukuli Lukeine Mwanaume Kichwa

View attachment 2256224View attachment 2256225View attachment 2256226View attachment 2256227View attachment 2256228View attachment 2256229View attachment 2256230View attachment 2256231View attachment 2256232
View attachment 2256393View attachment 2256394
View attachment 2256336
View attachment 2256286
Yule Membe ana LAANA Juzi tu alisema hakuna atakeyeuawa kwenye utawala huu, Yako wapi?
 
Hii ni hatari kama serikali imefikia hapa, wakaishi wapi sasa
 
1654948549999.png
 
Kwann hamkutusaiidia wakati tunafurushwa kule Ihefu mbalali, katavi na ujiji? Kwann wamasai?
Haya hayawezi kuwa maelezo na sababu ya furaha na kushangilia kwingi unakokufanya juu ya jambo hili katika ukumbi huu.
 
hakukuwa na kelele kama hivi sasa. Bagamoyo ardhi nyingi tu imechukuliwa kwa ajili ya ujenzi wa bandari, hakukuwa na kelele kama hivi sasa; what is special about wamasai kwamba hawatakiwi kutikiswa?

Tuachane na hilo la "wanaenda kupewa waarabu", swali la muhimu ni serikali haina ruksa ya kubadili matumizi ya ardhi/rasilimali?
Hatuwezi "kuachana na hilo la 'wanaenda kupewa waarabu'" (in fact hata wawe wahindi, wachina, wazungu); hili ndilo swala la msingi kama kweli lipo.
Hatuwezi leo hii kuwaumiza wananchi wetu kwa sababu tu ya kuwafaidisha wageni, eti kwa sababu za uwekezaji. Ingekuwa hivyo, pasingekuwepo na sababu yetu kudai uhuru wetu ili tujiamlie mambo yetu yanayotufaa sisi wenyewe.

Kwa hiyo nasema tena, kama kuna uhusiano wowote wa kuwahamisha kwa mizengwe ndugu zetu wa kimasaai ili eneo apewe mwekezaji, nami nitaunga juhudi za mapambano kudai uhuru kutokana na huu ukoloni mpya unaokuja kwa mlango wa "uwekezaji."
Tanzania haina upungufu wa sehemu za uwekezaji, na in fact, uwekezaji siyo kipaumbele cha maendeleo yetu; maendeleo yetu ni sisi wenyewe. Viongozi wanakosa sifa za uongozi wanapodhani kuendelea kwetu kunaletwa na hao watu wanaokuja kununua utu wetu hapa na kutufanya kama wageni ndani ya nchi yetu.

Umeweka mifano ya maeneo yaliyochukuliwa na serikali na ukaitaja Bagamoyo kana kwamba watu waliondolewa bila stahiki zao?
 
Hiyo stahiki ni huruma ya serikali au haki yao? Mbona kuna wanaobomolewa bila kulipwa fidia hamsemi?
Wote wanaofanyiwa hivyo ni waovu. Wapi ambapo watu hawakupiga kelele kuhusu uonevu?
Kila atakae tawala ni katili na mroho kwa style yake. JPM na SSM wako sawa ila kila mtu na style yake.
 
Hatuwezi "kuachana na hilo la 'wanaenda kupewa waarabu'" (in fact hata wawe wahindi, wachina, wazungu); hili ndilo swala la msingi kama kweli lipo.
Hatuwezi leo hii kuwaumiza wananchi wetu kwa sababu tu ya kuwafaidisha wageni, eti kwa sababu za uwekezaji. Ingekuwa hivyo, pasingekuwepo na sababu yetu kudai uhuru wetu ili tujiamlie mambo yetu yanayotufaa sisi wenyewe.

Kwa hiyo nasema tena, kama kuna uhusiano wowote wa kuwahamisha kwa mizengwe ndugu zetu wa kimasaai ili eneo apewe mwekezaji, nami nitaunga juhudi za mapambano kudai uhuru kutokana na huu ukoloni mpya unaokuja kwa mlango wa "uwekezaji."
Tanzania haina upungufu wa sehemu za uwekezaji, na in fact, uwekezaji siyo kipaumbele cha maendeleo yetu; maendeleo yetu ni sisi wenyewe. Viongozi wanakosa sifa za uongozi wanapodhani kuendelea kwetu kunaletwa na hao watu wanaokuja kununua utu wetu hapa na kutufanya kama wageni ndani ya nchi yetu.

Umeweka mifano ya maeneo yaliyochukuliwa na serikali na ukaitaja Bagamoyo kana kwamba watu waliondolewa bila stahiki zao?
Kwani issue ni stahiki au watu kutotaka kuondoka? Maana sijaona watu wakisema wanataka fidia, zaidi ya watu kusema hawawezi kuondoka kwenye ancestral lands, kama vile ni mara ya kwanza watu kuondolewa kwenye ancestral land.
 
Hata isipokuwa mara ya kwanza, huwezi kubeza sababu hiyo inayotolewa na hao wamasai.

Swala la kuhamisha watu kiholela siyo jambo dogo.
 
CCM na damu za watu ni kama uji na mgonjwa.
RC John Mongela anatulisha matango pori eti picha hizo ni za miaka 3 au 4 iliyopita! CCM ni majanga, wamegeuza uongo kuwa imani yao!
 
Back
Top Bottom