Picha zinatisha: Ni picha za Wamasai waliojeruhiwa na wengine damu zinavuja

Picha zinatisha: Ni picha za Wamasai waliojeruhiwa na wengine damu zinavuja

Naomba kuuliza, wanaamishwa wamasai wote au wanapunguzwa pamoja na mifugo yao na kubakiza idadi ndogo ili kuendeleza sifa ya mbuga ambayo binadamu na wanyama huishi eneo moja, kama ilivyokuwa mwanzoni?
 
Wanaharakati wa Kitanzania mna njaa sana kubabeki zenu.
Sasa Mnapata faida ipi kwa kutumia irrelevant images kwenye ku push agenda zenu za kibwege bwege.
 
 

Picha zinatisha: Samia Suluhu anafungua nchi​

 
Siri Ndo Hii,
 
Naona matundu ya risasi!!! Historia inajirudia. Mzee Mwinyi ndio aliwaingiza waarabu Loliondo,Leo mwanae anawaongezea eneo zaidi huko Loliondo huku damu zinamwagika!!
 
si wamenyoosha mishale kwamba wako tayari kabisa, sasa tatizo nn hapo
 
Unakubali kuhama kwa hiari kabisa,serikal inatumia kod za wananchi kuwaandalia makazi yaliyo bora kabisa,wakati wa kuhama unafika unagoma unashika na sime,ungekua wewe u ngefanyaje?
Kwahiyo hiyo kwako ni sababu tosha ya wao kupigwa risasi??
 
Hili suala la Ngorongoro lina utata mkubwa sana ambapo hadi sisi wenye akili nyingi tunashindwa tusimamie wapi..🤔. Hapo Ngorongoro kuna makundi manne yanayoleta utata mtupu; wamasai, serikali, mwekezaji wa Loliondo na wanaharakati.

Serikali ina hoja za msingi sana kwanini watu wahame Ngorongoro. Ile hoja ya kulinda wanyama na hifadhi ya Ngorongoro isipotee ni hoja yenye nguvu sana. Kinacholeta utata ni kuaminika kwa serikali kwamba tayari imewajengea nyumba za kuhamia huko Handeni. Je ni kweli? Je, yale makubaliano ya Arusha yalihusisha wamasai wa Ngorongoro kweli au kuna mamluki waliowasemea wenzao wa Ngorongoro?

Wamasai wao hawana hoja zenye nguvu sana za kung'ang'ania kubaki Ngorongoro ila haki za binadamu zinawalinda. Huwezi kuwatoa kama unatoa mifugo porini. Lakini na wao wanafuata sheria za kukaa hifadhini? Tumeona wengine tayari washajenga mijengo ya balaa ndani ya hifadhi kitu ambacho sio sahihi.

Huyu mwekezaji wa Loliondo nae ni kero kubwa kwa wamasai. Ninawalaani wote waliompa hilo eneo kwa mkataba mbaya kuwahi kutokea hapa nchini. Inasemekana yupo nyuma ya huu mgogoro. Wanaharakati walioko against serikali wengi wao sio wazalendo zaidi ya kuwatumia wamasai kupiga hela za mabeberu.
Well Noted Mkuu NIMEKUELEWA!!!
 
Back
Top Bottom